Mtikila amshutumu rais, polisi, usalama

Status
Not open for further replies.
KUna mtu ameniambia kwamba, Mtikila aliandaa ile taarifa kwa nia ya kuwabana wafadhili wake waliompeleka Tarime waongeze dau na hakujua kwamba itavuja na kufika mikononi mwa watu wengine. Ndio maana anachanganyikiwa na kuanza kumshambulia hadi JK. Hao waliomtuma wamemwambia JK na Mengi ni marafiki sasa akasahau kwamba hao wanaomlipa Jk ni Mwenyekiti wao, akamtukana.

Waliomtuma wameanza kumsakama wakisema, "wewe huaminiki inawezekana umewasiliana na mtu wako wa zamani na kumbe ulikuwa umekwisha kumpa huo waraka" sasa kibarua ama 'mgodi' kama anavyouita yeye umeharibika na na kwa kuwa uchaguzi wa Tarime umekwisha hatopata tena dili na asubiri "mgodi" mwingine uteme kama si mwaka 2010
 
Mimi naona kuna Mengi ya kujifunza kwa siasa za Tanzania.

Napendekeza vijana wanaochipukia katika medali za "Sayansi za jamii na zinazofanana na hizi" wafanye study kujifunza hawa watu na ideologia yao kwa mustakabali wa Taifa.

Mtu anaweza kuwa na Thesis "Rise and Fall of Rev. Mtikila: Lesson for multipartism politics in Tanzania" na nyingine nyingi zinazofanana na hizi. wadau mnaweza kuongeza.

Haya yasipofanyika, itakuwa ni kuvinyima vizazi vijavyo uelewa wa yaliyotokea katika harakati za siasa za kuiletea nchi hii maendeleo yake. Ukweli unabaki kuwa watu mbalimbali wana michango yao "Hasi au Chanya", wakiwemo kina MTIKILA. Tusipokuwa na utaratibu wa kuhifandhi na kuitafiti kwa undani basi, vizazi vitakuwa vinarudia haya haya yanayofanywa na wanasiasa uchwara kwa kupewa vijisenti na kuliangamiza Taifa.

Natoa changamoto kwa wasomi wetu!
 
Mtikila ni mwendawazimu na pia ni ndumilakuwili. Alistahili kudharauliwa na kutosikilizwa na umma wa Watanzania tangu pale alipoanikwa hadharani kwamba aliomba michuzi kwa fisadi Rostam.

nadhani kwa upande wa malipo yake toka CCM umeleta ttz hapa, strategy zao hazijafanya kazi maana na uchochezi wote ule aliotumwa na CCM lkn bado CHADEMA wamechukua... sasa kwa CCm tunavowajua kwa kupiga mapanga wameona hawana haja ya kumlipa afterall hawajashinda.... na wamekuwa hawana hofu nae kwa kujua kuwa watz bado watamuona ni kichaa tu hata kama akilalamika hadharani
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom