"mtihani wa private candidates"

Isaack Newton

JF-Expert Member
Apr 15, 2013
535
224
habari wakuu!
mimi huwa najiuliza,kwa nini PC huwa wanafeli sana ukilinganisha na SC ambao huwa hawafeli kiasi hicho? au mitihani ya PC huwa inatungwa migumu sana? naomba kujuzwa kwa wale ambao washa wahi kufanya mtihani kama PC!
 
Mitihan mbona wakati mwingne wanafanya mmoja?mfano form6 mwk huu walifanya mmoja na bado wamefulia,in short ni kwamba pc huwa hawasomi ukilinganisha na msuli wa sc full stop!
 
Mitihan mbona wakati
mwingne wanafanya mmoja?mfano form6 mwk huu walifanya mmoja na bado
wamefulia,in short ni kwamba pc huwa hawasomi ukilinganisha na msuli wa
sc full stop!

kweli kabisa mkuu, ila kwa upande wa passmark nackia pc ni 50% tofauti na sc ambayo ni 41%.je ni kweli?
 
Mitihan mbona wakati mwingne wanafanya mmoja?mfano form6 mwk huu walifanya mmoja na bado wamefulia,in short ni kwamba pc huwa hawasomi ukilinganisha na msuli wa sc full stop!

Ndugu hacha iyo habar kabisa ,, nakumbuka tulivokua tunasooma sio mchezo kabisa. Sema ttzo lipo kwenye vituo vya mitaani Walimu wengi ni wale wale wanafunzi wa Form six ambao kila mmoja anajisifu alipas mtihani wa taifa.
 
Sasa kumbe umeshajua tatizo liko wapi, hata sisi tulipohitimi A-LEVEL na kukaa mtaani muda mrefu bila ajira tulibuni ajira ya kufundisha tuisheni kwenye vituo vya mitaani, sasa huo mkwara wake sio wa kitoto, wanafunzi wakifunga shule zao wakifika tu kwanza unawapiga mkwara wewe nani, ulisomea wapi na ufaulu wako ulikuwaje katika somo husika, basi wakitoka hapo siku ya pili wanakuja na wenzao maisha yakasonga mbele.

Sababu ya pili. Ni vigumu sana kwa mtahiniwa binafsi kufaulu kama hajui ni kwanini alifeli. Mtahiniwa binafsi anayejua kosa lake ni rahisi kutolirudia na huyo ana nafasi kubwa ya kufaulu mtihani.

Sababu ya tatu. Watahiniwa wengi unaowaona mitaani wakihangaika na kufanya mitihani kama PC, hufanya hivyo kutokana na shinikizo la familia au wazazi ambao wanajua umuhimu wa elimu, vinginevyo vijana wa siku hizi kama ingekuwa ndani ya uwezo wao wangependa waende kwenye kusomea kazi moja kwa moja VETA.

Sababu ya nne. Haiwezekani mtu aliyeshindwa kufaulu ndani ya mfumo rasmi huku akiwa huru na kazi yake ni moja tu kusoma na bado akafeli halafu unatarajia afaulu wakati ameshaanza maisha ya mtaani huku ameanza kazi na demu anamtegemea yeye na bado starehe inamsubiria yeye bila kufungungwa fungwa na mtu.
 
kweli kabisa mkuu, ila kwa upande wa passmark nackia pc ni 50% tofauti na sc ambayo ni 41%.je ni kweli?
Amekudanganya nani? WATAHINIWA WOTE NI SAWA MBELE YA BARAZA LA MITIHANI NA WOTE WANASAHIHISHIWA KWA KUTUMIA MARKING SCHEME MOJA NA WASAHIHISHAJI NI WALE WALE, GRADE NI ZILE ZILE.

Ukitaka kujua yote hayo Baraza la Mitihani sio kituo cha Polisi jaribu kutembelea ofisi zao pale Mwenge maeneo ya Bamaga au hata mtandao wao www.necta.go.tz uliza utajibiwa. Ondoeni dhana potofu tujenge taifa lenye wasomi.
 
Tatizo kubwa huwa ni maandalizi kabla ya mtihani kwa pc hawajiandai kikamilifu na husoma kwa mazoea tena mara moja moja sana lakini kama utaweka juhudi binafsi huku ukisahihisha makosa yako ya awali lazima ufaulu.
 
sasa kumbe umeshajua tatizo liko wapi, hata sisi tulipohitimi a-level na kukaa mtaani muda mrefu bila ajira tulibuni ajira ya kufundisha tuisheni kwenye vituo vya mitaani, sasa huo mkwara wake sio wa kitoto, wanafunzi wakifunga shule zao wakifika tu kwanza unawapiga mkwara wewe nani, ulisomea wapi na ufaulu wako ulikuwaje katika somo husika, basi wakitoka hapo siku ya pili wanakuja na wenzao maisha yakasonga mbele.

Sababu ya pili. Ni vigumu sana kwa mtahiniwa binafsi kufaulu kama hajui ni kwanini alifeli. Mtahiniwa binafsi anayejua kosa lake ni rahisi kutolirudia na huyo ana nafasi kubwa ya kufaulu mtihani.

Sababu ya tatu. Watahiniwa wengi unaowaona mitaani wakihangaika na kufanya mitihani kama pc, hufanya hivyo kutokana na shinikizo la familia au wazazi ambao wanajua umuhimu wa elimu, vinginevyo vijana wa siku hizi kama ingekuwa ndani ya uwezo wao wangependa waende kwenye kusomea kazi moja kwa moja veta.

Sababu ya nne. Haiwezekani mtu aliyeshindwa kufaulu ndani ya mfumo rasmi huku akiwa huru na kazi yake ni moja tu kusoma na bado akafeli halafu unatarajia afaulu wakati ameshaanza maisha ya mtaani huku ameanza kazi na demu anamtegemea yeye na bado starehe inamsubiria yeye bila kufungungwa fungwa na mtu.

kweli mkuu wengi hawajui kosa walilolifanya mara ya kwanza,pia hawakubali walifanyakosa,wanalaumu necta so ni vigumu kufaulu.ukikubali kosa unajifunza kitu ambacho ulikosea kikoje na hauludii tena.
 
Nna research yangu juu ya kwa nini ma prevate candidates wanafeli,ntaitoa hewani simda mrefu.
 
mkuu umenena, plan za huyu dada ni mzuri academically sema alikuwa na matatizo kipindi cha mtihani ndo imepelekea kwa kupata matokeo mabaya.vile vile nae anasema ukweli kuwa kuna baadhi ya makosa aliyafanya kwenye mtihani, hivyo amekiri kuwa akiingia shule,, msuli atakao kuwa nao ni mara tatu ya msuli wa kwanza!!
 
Nna research yangu juu ya kwa nini ma prevate candidates wanafeli,ntaitoa hewani simda mrefu.
Tunaisubiri kwa hamu mkuu labda itasaidia hawa watanzania wenzetu walio nje ya mfumo rasmi ili nao wanufaike na matunda ya juhudi zao katika kujielimisha.
 
Wanajamvi nina mdogo wangu anataka arisiti mtihani wa kidato cha nne mwakani 2016, ni shule gani nzuri yenye ufaulu mzuri kwa hapa DSM naweza kupata;

sifa
1. iwe ya boarding
2. trend nzuri ya ufaulu kidato cha nne
3. iwe mkoa wa DSM
4. ufundishaji mzuri wa masomo ya HISTORY, GEOGRAPHY, CIVICS NA ENGLISH

NOTE: Gharama cyo tatizo
naombeni msaada wenu katika hilo ili nijipange mapema,
ASANTENI
 
nimezipitia coment zenu wengi mpo sahihi na mna mawazo mapana ila siku hizi pc hawafail km zaman mfano mzuri ni mimi hapa nimerudia mtihan wa kidato cha 6 mwaka huu na nimepata matokeo mazur sana na kiujumla kituo chetu kilifaulisha karibia watahiniwa wote kwani tuliofanya mtihan tulikuwa 24 na 21 wote tumepata grade za kutupeleka vyuo vikuu cha msingi ni kujifunza kutokana na makosa mimi hapa nikiwa SC nilikuwa sikomai kiviile kazi yangu ilikuwa cameraman kwo muda mwingi nilishnda kuzunguka kutafta wateja, pili nilikuwa siingii darasani wala prepo kitu kilichosababisha niandike barua ya maelezo kwa academic wa shule kwani attendance ilionesha nna miez miwil sijaingia darasan, tatu nilikuwa sipend discussion na wenzangu kwo nilikuwa nakomaa kivyangu kwny kitanda changu, kingine nilikuwa napenda sana kuzurura town vitu vyote hv vilisababisha nipate matokeo mabaya lakin nilivokaa na kugundua makosa yng nikaamua kukomaa tena na nkatafta washkaj tukapiga siscussion za kutosha, msuli wa maana kias kwmb tumeingia kwenye paper tunajua tunaenda kuua kwani tulikuwa tuko vizur kila sehem
 
kama sio muanga utaongea mengi ,,mimi matokeo ya kwanza yalikuja cijafauru ,,ila nilivyo lisit hata sikujiandaa kama mtihani wa mwanzo ila nilifauru kilahisi tu ,,xo kwa mtu ambaye amerisit na akafel anitafute nimpe ujanja na maexperience
 
hata mimi nashuudia kutoka kwangu nilifanya mtihan wa six huku ni mfanyakaz na nilifanya vizuri sana kwa kupata one ya uhakika cha msingi uwe na malengo usijidanganye pc ni ngumu kwa hiyo unatakiwa usomE mara mbili ya SC
 
mtihani ni ule ule ccta, pc& sc wanapiga paper 1 na grade ni zilezile
 
Sasa kumbe umeshajua tatizo liko wapi, hata sisi tulipohitimi A-LEVEL na kukaa mtaani muda mrefu bila ajira tulibuni ajira ya kufundisha tuisheni kwenye vituo vya mitaani, sasa huo mkwara wake sio wa kitoto, wanafunzi wakifunga shule zao wakifika tu kwanza unawapiga mkwara wewe nani, ulisomea wapi na ufaulu wako ulikuwaje katika somo husika, basi wakitoka hapo siku ya pili wanakuja na wenzao maisha yakasonga mbele.

Sababu ya pili. Ni vigumu sana kwa mtahiniwa binafsi kufaulu kama hajui ni kwanini alifeli. Mtahiniwa binafsi anayejua kosa lake ni rahisi kutolirudia na huyo ana nafasi kubwa ya kufaulu mtihani.

Sababu ya tatu. Watahiniwa wengi unaowaona mitaani wakihangaika na kufanya mitihani kama PC, hufanya hivyo kutokana na shinikizo la familia au wazazi ambao wanajua umuhimu wa elimu, vinginevyo vijana wa siku hizi kama ingekuwa ndani ya uwezo wao wangependa waende kwenye kusomea kazi moja kwa moja VETA.

Sababu ya nne. Haiwezekani mtu aliyeshindwa kufaulu ndani ya mfumo rasmi huku akiwa huru na kazi yake ni moja tu kusoma na bado akafeli halafu unatarajia afaulu wakati ameshaanza maisha ya mtaani huku ameanza kazi na demu anamtegemea yeye na bado starehe inamsubiria yeye bila kufungungwa fungwa na mtu.

Kipengele cha mwisho mkuu nakuunga mkono. Nina mpwa wangu mwaka jana alifeli pc karudia mwaka huu. Majuzi kati nimepewa taarifa Ana demu na amezaa nae. Nikimpa senti za kujikimu kumbe anapelekwa kwenye familia. Naisubiri matokeo yake ya mwaka huu nione.
 
Back
Top Bottom