Mtihani wa Dini Uondolewe kwenye Sylabus na kwenye Mitihani ya NECTA

Hoja iliyozungumza ni kukosekana utendaji wa haki na uaminifu ambayo muhusika aliaminiwa. hilo ufumbuzi wake sio kuondoa somo la dini, ufumbuzi wake ni kuwajibishwa na kuweka kiongozi muadilifu. Hii ni wakeup call kwa wahusika wajue kile kilichokua kikidaiwa muda mrefu kilikua ni madai ya msingi. Kama lilichofanyika ni kweli cha kuwafelisha wanafunzi kwa sababu ya dini zao kwa muda wa kipindi cha miaka isiyopungua kumi kwakweli hichi sio kitu cha kupuuza hasa ukizingatia kua hakuna njia ya kukilipa kwa thamani yoyote.

nipen muda wadau nitawapa data kamili juu ya UTENDAJI WA NECTA NA WATENDAJI WAKE,,,,NA KWANINI BARAZA LINASHUTUMIWA KWENYE SUALA LA UDINI NA UPENDELEO
 
Somo lenyewe lisiondolewe bali lisiwe sehemu ya kupata wastani wa kufaulu ili kuongeza division.

Kwani hata somo la dini wenzetu waislam wanafeli pia au halijaingizwa kwenye cylabas?
 
Wakuu tuache jazba....kosa lililofanyika limeshafafanuliwa kuwa mfumo ulotumika uliandaliwa kwa paper 3 zilizokuwa zikifanyika kabla ya format kubadilishwa mwaka jana kuingia pepa 2.

Watu tumekazania Udini na hata tunafikia mahali pa kutaka somo liondolewe...wengine Ndalichako ajiuzulu nk...yawezekana alohusika na kosa la kutokugagua ukokotoaji huo ni wa dini hiyo hiyo inayolalamika.Huyu ndalichako anayesulubiwa anahusika vipi na mfumo? Tatizo tunaingiza udini kila mahali...Wakuu wa shule zilizohusika walishaelimishwa juu ya kilichotokea na wameelewa lakini wengine (ambao nautilia shaka uwezo na elimu yao wako busy misikitini kuhamasisha maandamano.

Haka kanchi bana ... Sometimes ni kukosa kazi...Tuwaache NECTA wafanye kazi yao mimi nina uhakika pale ni moyo wa wizara ya Elimu (ambayo inaongozwa na Muislamu mwenzao) na Ikulu (ambayo pia inaongozwa na Muislamu mwenzao)...Kwa hakika kama kungekuwa nauchakachuaji wa makusudi nadhani wengine wangekuwa ndani sasa hivi..

niambie kwanini NUNDU NA CHAMI WAMEONDOKA MADARAKANI?????ndalichako kwanini asihusike na mfumo wakat yeye ndo katibu mtendaji???hadi anaulizia matokeo alikua hajui kuwa ni mfumo gani umetumika kukokotoa????kuhusu new format,,,ni kwamba NECTA walishatoa machapisho mbalimbali na kuyagawa kwenye shule zote,hii ina maana kuwa walishajipanga na mfumo mpya,,,,,hata kama alohusika ni mtu wa kukokotoa,,,ndalichako kama ilivokua kwa mawaziri walong'olewa anawajibika kwa kutokua makini kwenye baraza,,,,sasa hadi anaitisha press conference kutangaza matokeo basi alikua na taarifa,,,,,hapo amekuja na justfication tu mdau za ukokotoz,,,mwenye akili amemuelewa,,,,maana ishu ya ukokotoz ameitoa baada ya kelele za wakuu wa shule
 
Kwani hata somo la dini wenzetu waislam wanafeli pia au halijaingizwa kwenye cylabas?

hapana shine,,,,somo lipo kwenye muhtasari aka Syllabus,ila changamoto ilofanya tujue kufeli kwa watoto hiyo Islamic Knowledge ni UKOKOTOZ WA ALAMA(WASTAN),,,,,mbona walivokokotoa kwa mara ya 2 wamefaulu????na wamekiri kuwa walikosea(kwa maelezo yao necta)
 
kwa kuwa linaleta migogoro sana bora hata lisiwepo kwenye mtihani ya kitaifa.

liendelee kuwepo na wahuusika wawe makini tu,,,,si kwa somo hilo hata kwa mengine,,,,jaman si wote wanaofeli ni VILAZA,,,,kuna makosa ya kibinadam meeeengi sana yanafanyika NECTA
 
kufuatia shutuma wa baadhi ya madhehebu/dini kwamba watoto wao/dada/kaka/ndugu zao kwamba wamefelishwa au hakutendewa haki na necta, basi ni vizuri hii mitahi au somo lote kwa jumla likaondolewa katika sylabus yetu, kwa maana kila dhehebu litakuwa lina hisia kwamba wafuasiwa wao wameonewa kwa hili au lile. hivyo basi ili wote wawe katika usawa ni mitahani inayo fanywa na makundi yote ndio yaingie kwenye sylabus ya taifa, hayo mengineyo kila dhehebu lifuate huko huko kwenye mamlaka zao.
Mawazo yako Ningeyaona ya maana kama ungeshauri kuwa baada ya necta kusahihisha mitihani basi makaratasi yote ya mitihani na marking scheme zipelekwe mashuleni ili tuone kama kilichotangazwa ndicho wanafunzi wamepata? Hili ndilo la msingi. Kwani hata masomo hayo unayodai siyo ya dini hatuna imani na matokeo yanayotolewa na ushahidi wa hilo kila mwaka wanafunzi wanaoenda kudai wasahihishiwe ni wengi.
 
hakuna somo la dini katika sylabus zetu naomba mleta maada kasome vizuri, hivi "divinity" kiswahili chake ni dini?

di·vin·i·ty

1. the quality of being divine; divine nature.
2. deity; godhood.
3. a divine being; God.
4. the Divinity, ( sometimes lowercase ) the Deity.
5. a being having divine attributes, ranking below God but above humans:
Cha msingi ni kuondoa masomo ambayo dini moja inafanya nyingine haifanyi ili ikitokea makosa kama kwenye fisikia basi rungu ni kwa wote ili kuondoa dhana ya kwamba fulani anaonewa na mwingine anapendelewa, ni kingine cha msingi ni kwamba mtihani uliokosewa ulikuwa huo moja lakini imejenge dhana kwamba kitu hicho hcho kipo kwenye masomo mengine na ni miaka yote, kama si ujinga huu ni nini? Divinity?
 
kesho na keshokutwa likitokea tatizo kwenye commerce nayo tuifute?????
kosa likitokea kwenye commerce litawakumba wote wenye dini na wasio na dini, hivyo hakuna atakaye sema nimeonewa kwa sababu ya dini au rangi yangu.
 
Cha msingi ni kuondoa masomo ambayo dini moja inafanya nyingine haifanyi ili ikitokea makosa kama kwenye fisikia basi rungu ni kwa wote ili kuondoa dhana ya kwamba fulani anaonewa na mwingine anapendelewa, ni kingine cha msingi ni kwamba mtihani uliokosewa ulikuwa huo moja lakini imejenge dhana kwamba kitu hicho hcho kipo kwenye masomo mengine na ni miaka yote, kama si ujinga huu ni nini? Divinity?

mkuu naomba nikuhakikishie kabisa waliowafelisha hao waislamu ni waislamu wenyewe. mitihani husahihishwa na walimu wa masomo husika. mfano hisabati husahihishwa na walimu wanofundisha hisabati NECTA huwachagua walimu kulingana na masomo yao. kama somo la dini ya kiislamu linafundishwa mashuleni , walimu ambao kwa vyovyote vile ni waislamu na siyo wakristo nndiyo walisahihisha
 
I second with that. Wenye dini zao waongozwe kusimamia hayo mambo wenyewe, kama hawataki hiyo ngoma ndio iishie hapo, hakuna kubembeleza. Haingii akilini mimi mlipa kodi nisiyeamini nilipie 'maarifa' ambayo hayamek sense.
 
nipen muda wadau nitawapa data kamili juu ya UTENDAJI WA NECTA NA WATENDAJI WAKE,,,,NA KWANINI BARAZA LINASHUTUMIWA KWENYE SUALA LA UDINI NA UPENDELEO

acha majungu. unapoteza muda mwingi kuongea vitu husivyovijua. Nafuatilia sana unachoandika ni majungu na upuuzi husiokuwa na data. unachosha watu bure. Hakuna mwenye sera ya udini. Husijustify weakness zako. wenzako wako busy kusoma wasonge mbele we umekali majungu tu.
 
Matatizo mengine serikali inajitakia.

Serikali iwaachie mitihani yao maasikofu na mashekhe kila mmoja kwanamna yake ajipange na afanikishe mitihani yake kwa kadri ya mahitaji yake kwa dini yake na imani yake.

Wanafunzi wote wafanye mitihani ya kitaaluma kwa maana ya masomo ya elimu dunia, ya akhera wawaachie huko misikitini na makanisani. Inaamana ikitokea makosa yoyote basi yatakugusa watahiniwa wa imani zote, naikitokea imani fulani imeathilika zaidi basi hapo itabidi tumtafute mchawi.


Mambo ya dini ni magumu sana tena sana, na hakika masuala ya dini katika utendaji wa kiserikali unapoyachangamanisha utajaribiwa sana na wenye dini zao. Wapo watakao sema anafanya kazi kwa ufanisi na wengine watasema hafai anapendelea.

Tutafukuza makatibu wakuu san na hili sio muarobaini. Tatizo la (denominator) factor iliyotumika kupata wastani kimakosa sio kazi ya katibu mkuu hata kidogo, ni kosa ta kiufundi katika kukokotoa, katibu anaingiaje?

Kwa lengo la kuidumisha na kuipa amani yetu afya na kuimarisha mahushirikiano mazuri na mshikano wa kada mbalimbali za imani tofauti ndani ya taifa letu tukufu la Tanzania kwa upande wangu serikali ijitoe na iwaachie watu wa dini kuamua masuala yote yahusuyo mitihani ya dini.
 
Ukiwa na E ya physics inamaana kwenda chuo kuliko uwe na A ya smo la dini.
 
Back
Top Bottom