Mtifuano Mkutano wa CCM - Dodoma

Hata kama tuna hasira namna gani dhidi ya CCM ni lazima tukiangalie chama hicho kwa mtazamo wa chama kinachoongoza nchi kwa sasa. Tatizo letu tunaombea CCM idhoofike yenyewe (Naturally) ili vyama vyetu viimarike kwa udhaifu wa CCM. Mtazamo wangu tuimarishe vyama vyetu ili uimara wake uidhoofishe CCM na kama nchi tufaidike.

Kama kuna mtu anadhani mapinduzi aliyofanyiwa Thabo Mbeki na Jacob Zuma ndani ya ANC umeiletea mafanikio Afrika Kusini anajidanganya!! Hawa hawa kina Julius Malema ndiiyo waliongoza mapinduzi haya na aliyekuwa mfadhili wa shughuli yenyewe Jacob Zuma naye tena anatishiwa na wanamapinduzi "wenzake" kupinduliwa.

Kama hasimu wa Kikwete ndiye atakuwa Mwenyekiti na tunakoelekea inaonekana kwa mara nyingine wanasiasa wanaamini Rais ajaye atatoka tena CCM Urais wa Kikwete tunataka kuuweka rehani na inavyoonekana hakuna nguvu ya kuhimili (Shock Absorb) dhoruba ya kuuweka rehani Urais wa Kikwete. Mwaka 1994 wakati Urais wa Mwinyi unatashiwa na kina Malecela na Kolimba alikuwepo Nyerere, leo yupo nani?
 
Mkuu Kigarama maneno mazito sana yafaa kila mwanajamvi anayepitia bandiko hili akalisoma mara mbili mbili.
 
Last edited by a moderator:

Ni kada mwenye maslahi kwenye kundi fulani tu ndani ya CCM ndiye atakayekubaliana na hoja za mchambuzi kwa leo hii..Hoja zingine zinaweza kuwa sahihi ila hapa ame speak his heart pengine ana maslahi katika kundi lenye taasisi ya urais na hivyo uwoga wake anaupeleka kuwa woga wa nchi..Sisi kama nchi tuko salama zaidi iwapo Rais atakuwa siyo mwamuzi wa mambo ya chama chake tena ndani ya CCM ambayo demokrais ipo grass roots tu ukizidi kupanda juu ni nepotism na consolidation of power ndiyo maana hata huyo mwenyekiti wataifa hana mtu anayegombea naye kiti...
 

Mapinduzi yalishafanywa na CCM wenyewe 2005 ila huu ni mwendelezo tu hakuna kipya so nyie wenye hofu na doubt kama hana maslahi ya moja kwa moja na mnatishika na mageuzi kwani you are uncertain of what the change will bring to your life..
 
Rushwa ccm ni kama kansa iliyokomaa mwilini! Hakitoki chama hiki!
 
Hapo kwenye red nimesoma kidogo nizimie...!!!
Du!! Ama kweli hii JF ina GT's na wewe umo na una haki kweli ya KUTOKUSHANGAA, maana kwa mtazamo wako ni kwamba mke wa tajiri akikamatwa ugoni basi imehalalisha kutokushangazwa ukimkuta mkeo ameleta mme mwingine ndani eti kwa sababu wewe hauna maendeleo yoyote sio tajiri (ni masikini), duu! na wewe umo GT wa JF.

 

Kimsingi nakubaliana na hoja zako ndio maana katika hoja zangu nimeweka certain conditions ambazo nadhani zikiwa met, zitasaidia hali kuwa shwari hata kama kofia hizi mbili zitatenganishwa; i hope ulinisoma kuhusu conditions hizo, na kama zitakuwa met, ni bora kutenganisha kofia hizo kuliko kubakia na hali ya sasa;

tatizo langu mimi ni kuzitenganisha bila kufanya mabadiliko yoyote; ndio maana nikasema iwapo conditions nilizotaja zitaendana na mabadiliko haya, sidhani kama tutaona watu wakikimbilia cheo hicho; watu wanakitaka kwa sababu ni ngazi muhimu ya kukwaa urais, sio ngazi muhimu ya kusaidia kujenga chama; thats the bottom line;
 

Ame, mimi na wewe ni mgongano wa mawazo tu, hakuna lingine; vinginevyo sina maslahi na kundi lolote ndani ya CCM zaidi ya kuwa mwanachama kwa miaka kumi na nane, kabla hata ya hawa wakubwa wanaotajwa tajwa sasa sijui lowasaa sijui kikwete sijui wakiwa hata hawavumi; na hawa wote lowassa, kikwete watapita tu na kwenda zao kustaafu na kuacha CCM ikiwa pale pale, ndio maana mimi huwa siwekezi kwa wapita njia, bali Taifa kupitia chama cha siasa, na kwa sasa ni CCM, and who knows, pengine kesho Chadema, CUF etc;

Ni muhimu kwa vijana kuchagua upande sahihi wa historia, na hilo ndio lengo langu kubwa kwani miaka kumi na tano ijayo hawa wote watakuwa pensioners tu huku mimi nikiwa bado nadunda, sasa kama nitafanya makosa sasa, nitaficha wapi sura yangu miaka hiyo; as much as i look like natetea sijui Kikwete sijui nani, ukweli ni kwamba natetea taifa langu, na kigarama kwenye bandiko namba 212, kaelezea vizuri sana kuhusu umuhimu wa kuangalia suala hili kwa maslahi ya taifa pamoja na ukweli kwamba yeye sio mwana ccm;
 
Hivi vipeperushi mbona vya chadema! Hawa jamaa ni wachochezi sana!
 

Well said;
 
Baada ya CCM kusambaratika kitafuata CHADEMA ambayo nayo inaharufu mbaya ya udini na umajimbo!
Anaponyolewa mwenzako we tia maji!
Mmh! Kwa response hii! Ninaamini ule usemi usemao "Ukweli unauma". Jipe moyo kadogoo, hata vikianguka vyama vyote ukweli utabaki kuwa CCM ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuanguka.
 
Wanaopiga Kura ya Mkiti JK wameshaingia Dodoma na kama nao watahogwa na Fisadi No.1 watamtikisa hasa na uenyekiti wake
Maana mtu huwezi kuwa Ujerumani kwa matibabu ukatumia remote wajumbe wa Shinyanga pokeeni 3m kila mjumbe eti mkataeni JK asiwe Mkiti tena kunakamatwa vipeperushi live suala hilohilo
Sasa maana ya Uenyekiti ni nini?
JKN aliweza agizwa toka Butiama ili tu amalize mzozo John hufai Kolimba au hata Lowasa hivi Ikulu kuna biashara gani? JKN angewauliza
Nashauri humu JF ni wachangiaji tu ila Kikwete ukicheza na mbwa atakufuata msikitini Piga ndita fyeka maadui zako na Chama km unataka kuongoza CCM au itakufia mkononi
 
Reactions: Ame
Dalili za jk kumbeba Membe ndio zinamponza, aangalie sana aweza nyanganywa kadi mhe rais lowasa ni mtu mwingine kabisa, kuna watu wanamtii kuliko kristo na mtume muhamad

kweli...?.
 
wrong approach!! hakunaga kitu kama hicho, na huu ndio udhaifu unaopigiwa kelele kila siku, kazi ya pccb na dpp ni nini? iweje jk akiri hadharani udhaifu mkubwa kiasi hicho?
 

Ofcourse huwezi kutenganisha kofia hizo bila kufanya marekebisho kwenye kanuni na katiba za vyama.Nafurahi sasa unaamini katika kutenganisha kofia hizo na kwamba kuna faida nyingi za hilo kuliko hasara.
 
Reactions: Ame
Ofcourse huwezi kutenganisha kofia hizo bila kufanya marekebisho kwenye kanuni na katiba za vyama.Nafurahi sasa unaamini katika kutenganisha kofia hizo na kwamba kuna faida nyingi za hilo kuliko hasara.
Faida zipo, as long as separation hiyo inaendana na changes au conditions nilizojadili au something close..., vinginevyo Ame na wengine wao wanataka mabadiliko ya mtu katika kiti, PERIOD;
 

Yaah its true the only difference is I know what will be the outcome (the reason why am cool) and you try to calculate the probability of the occurance for the future is very uncertain on your side....Soma tena post yangu ya easter 2011....This is a very calculated move and no one ambaye anaitwa fisadi atakaa aingie katika political circles za Tanzania..Wengine wanaakili nyingi sana na kudhani ni wajanja lakini we have got power to effect change..Watch and see the best is yet to come!
 

.........Kwa hali yoyote ile CCM inawabidi kutumia akili ya kujisawazisha kupitia mkutano huu, wanachama kama watatumia akili timamu watakinusuru chama chao lakini wakiangalia masilahi TUMBO wanakiangamiza Chama chao.......
kwani hao mafisadi hamuwafahamu jamani ... mnawafahamu ila mnaendekeza njaa na kutokujali.... mnafahamu kabisa kwamba huyu anakashfa hii na ile lakini mnasahau,....... mnamchagua! mnamjua huyu mwizi mnamchagua..... mnajua kabisa amesaini mikataba inayoliangamiza taifa nyinyi hamjali mnamchagua...... mmezoea kununuliwa kwa 2,000/= watu wazima mnakubali kuondoka majumbani mwenu kwenda kufungiwa katika chumba mkilishwa na kunyweshwa bia mbilimbli hamna aibu kisa mnalinda kura za mgombea wenu....... wapo wana CCM ambao hawatoe kura mpaka wapewe rushwa...... yaani kura yake haiangalii nani ni nani bali anayetoa 5,000/= ndio anampa kura yake........ mnatia kichefuchefu.......... acheni hizo......mnahongeka kirahisi sana .... sasa angalieni mnavyokiacha uchi chama chenu..... hivi mtalaumu upinzani au nyinyi njaa zenu ndo mnakidhoofisha CCM yenu? halafu mnatabia ya kuondoa wagombea wakereketwa wa mabadiliko kwa usemi wenu wa ajabu kuwa eti CCM ina wenyewe... na wenyewe ndio sisi mafisadi ......... kuna usemi usemao asiyejua kufa aangalie kaburi..... sasa yetu macho Kanu iko wapi Kenya, Unip iko wapi Zambia?
 
Hawa magamba muda si mrefu wataanza kuuana kinachotakiwa sasa hivi ni kuanza kuandaa chama kingine cha upinzani kitakacholeta changamoto kwa CDM(chama tawala kuanzia 2015) maana magamba watakufa kifo cha mende(miguu juu) muda si mrefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…