Mti ufukuzao mbu

Hii imekaa kiporojo zaidi, acha tusubiri ushahidi wa picha ama aliponunulia huo mti

Inawezakana ni porojo maana sina scientific explanation. Lakini niliambiwa ni mti wa kufukuza mbu na mbu siwaoni. Hivyo tu . Picha zaja soon.
 
cha muhimu hapa ni picha au jina kamili la huo mti

Huyu jamaa nae anatuyeyusha mi nishamtajia jina huenda ni Cedrela sasa aki-google ataweza kuona kama ni wenyewe au la ili atuambie! Akisema akirudi nyumbani then kesho atuletee picha hii thread yenyewe itakuwa ishapotelea kwenye archive za Invisible
 
Miezi miwili iliyopita nilienda kununua miti ya kuotesha shambani . Mwuuzaji akanieleza kuwa mti fulani ni mzuri maana ni ant mosquito. Nikampuuzia lakini nikaununua -mmoja tu, na nikaupanda mwelekeo wa nyumba upepo unakotokea.

Huu mti umemea vizuri na supprisingly sijaona mbu tena. Je wana JF vipi mliwahi kusikia kitu hii? Ni ya ukweli. Tulikuwa jioni tunaspray dawa za kuua mbu lakini hamna mbuuuu .. Believe me. Jina la mti wenyewe silijui na wale jamaa wansema tu mti wa kufukuza mbu.

umenunua wapi,
tutajie basi,au
umekuja kuleta porojo...
 
Miezi miwili iliyopita nilienda kununua miti ya kuotesha shambani . Mwuuzaji akanieleza kuwa mti fulani ni mzuri maana ni ant mosquito. Nikampuuzia lakini nikaununua -mmoja tu, na nikaupanda mwelekeo wa nyumba upepo unakotokea.

Huu mti umemea vizuri na supprisingly sijaona mbu tena. Je wana JF vipi mliwahi kusikia kitu hii? Ni ya ukweli. Tulikuwa jioni tunaspray dawa za kuua mbu lakini hamna mbuuuu .. Believe me. Jina la mti wenyewe silijui na wale jamaa wansema tu mti wa kufukuza mbu.

embu angalia picha hii useme huo mti unafanana na huu au la? Kama haufanani na huu na mimi nidevelop interest ya kusubiri picha zako kesho
 
Attachments

  • Cedrela_odorata_foliage.jpg
    Cedrela_odorata_foliage.jpg
    68.7 KB · Views: 139
haaa haaa.....kiswahili tunaita mti kunuka, sio mbu tu unafukuza hata binadamu. I guess the species is Cedrela odorata (Spanish Cedar)
Cedrela_odorata_foliage.jpg

Kwetu ni kwetu, ulimaanisha huu? Maana huu ndiyo Cedrela odorat. Lakini una sura kama Muarobaini. Labda tupe data zaidi.
 
Mmh shakuwa dili jamaa hasemi aliponunua sijui asingeambiwa kama angeujua,haya ndio matatizo ya waswahili anaona akisema aliponunua watu watafaidi,huo ndio uchoyo wa sisi miafrika,ubinafsi kula kona
 
Mkuu akhsante kwa habari njema. Tutautafuta huo mti wa maajabu.

Kwa upande mwingine nawaza hawa watu wa kampeni ya ZINDUKA! Wangetuzindua na huu mti ukawa maarufu wangeokoa maisha ya wengi sana kwani siku zote kinga ni bora kuliko tiba!!
 
Cedrela_odorata_foliage.jpg

Kwetu ni kwetu, ulimaanisha huu? Maana huu ndiyo Cedrela odorat. Lakini una sura kama Muarobaini. Labda tupe data zaidi.

Kutokana na maelezo yake, binafsi mti ambao nafahamu una uwezo wa kufukuza wadudu 'na hata binadamu' kutokana na harufu yake ni Cedro. Miti hii inapatikana sana Kimboza morogoro na pia Usambara mashariki. Mbao zake ni nyepesi kiasi lakini haziliwi na wadudu kama mchwa. Cheki hii link ya Wikipedia uone matumizi yake hasa haya ya kufukuza wadudu ([ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Cedrela_odorata"]http://en.wikipedia.org/wiki/)Cedrela_odorata[/ame]. Lakini kwa vile mhusika hajaweza kuutambua kama tulivyoweka picha jana, labda anazungumzia mti mwingine, tusubiri picha zake leo.

Quote from Wikipedia
'Cedro heartwood contains an aromatic and insect-repelling resin that is the source of its popular name, Spanish-cedar'
 
Ulinunua wapi na mie nkautafute?
Siku za nyuma nlishawahi kuletea mche, nikaambiwa kuwa huwa unafukuza nbu.
Nilipoupanda ukafa, nikaagiza mche mwingine, na nikaomba maelekezo mazuri zaidi ya kuuotesha.aliyenipa akanimaliza kabisa nguvu,
akasema huo mti ni vigumu kuota mpaka uunuie maneno fulani kwa kuwa hufukuza wachawi pia,
kwa hiyo wachawi wanauangamiza kabla haujawa mkubwa.nikamua niachane nao.

Hapo mkuu umetoa kali. Yaani uliachana nao kwa sababu ulihofia wachawi nao watakukimbia? ha ha ha haaaaa!
 
Miezi miwili iliyopita nilienda kununua miti ya kuotesha shambani . Mwuuzaji akanieleza kuwa mti fulani ni mzuri maana ni ant mosquito. Nikampuuzia lakini nikaununua -mmoja tu, na nikaupanda mwelekeo wa nyumba upepo unakotokea.

Huu mti umemea vizuri na supprisingly sijaona mbu tena. Je wana JF vipi mliwahi kusikia kitu hii? Ni ya ukweli. Tulikuwa jioni tunaspray dawa za kuua mbu lakini hamna mbuuuu .. Believe me. Jina la mti wenyewe silijui na wale jamaa wansema tu mti wa kufukuza mbu.

Huna picha ya mti huo? Kaupige basi utuletee. That style, Tanzania tutaishiana na malaria. Ati na wachawi unafukuza? Kumbe usitegemee mchawi akushauri kuupanda kwako, atachea mwili wa nani akiukosa wa kwako?
 
Kwa faida ya wana JF na wananchi wote upige picha utuletee au wataalam wa mistu sijui
Nimechoka kuugua Maralia kila siku ..Zinduka Tanzania
 
Mkuu maelekezo ya mti huo tafadhali, hiyo ndo ZINDUKA! kama kweli huo mti unafanya kazi, tupande nchi nzima. Haiwezekani vita vya malaria vikapiganwa kwa chandarua cha olyset, wizi mtupu!!!!
 
Huyu hana mti wala jiti, hesabu zake tu zimemchanganyia kichwani zinamtuama atuletee hiyo thread.
ingekuwa kweli hata alipo nunua mpaka akapige picha! si aseme tu,ama nayo yahitaji mpaka akapige ilihali mti unafukuza mpaka flash za kamera????
aaaannggggggghhhhhhhhh!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom