Mti ufukuzao mbu

Mfamaji! samahani naomba kuuliza walikwambia ukikua unakuwa mkubwa kiasi gani, ie. mwambe, na je waweza pia kuupanda kwenye vyungu vya maua kama mizi ziz yake sio mikubwa?

Wanasema ukiuacha utakuwa mkubwa lakini unaweza kuucontrol ukawa mfupi wa kivuli. Unaweza ukaupanda kwenye chungu cha maua na ukauweka popote kama plant . Ukiutoa ukaupanda kwenye udongo wa kawaida utakuwa mti.
 
I mean kama kwa majirani kuna mbu ilhali kwako hamna tunaweza tukafikia muafaka kwamba mti umesaidia.....kama kote hakuna mbu then itakua sababu nyingine.

Kweli. Lakini sitaki niutetee tu huu mti for I have no other reason than to share my experience with you people Kwanza wauzaji wanauuita mti wa kufukuza mbu. Halafu nimeona effect yake kama mimi. Kabla ya kuupanda mze mbu kibao .Tulikuwa tunapulizia dawa na maneti juu. Sasa hivi nafungua dirisha full .
 
Kwa mujibu wa 'risachi' ya kwetunikwetu huu mti hauwezi kumea maeneo ya pwani (inahitaji sehemu za mwinuko)!
 
Wakuu heshima mbele!

Kwa mtazamo wangu mbu wa Dar ni sugu sana. Si kama wa Arusha, ikizingatiwa hali ya kule ina ka-ubarid kidogo. Hivyo mbu wa huko ni mdebwedo kiasi. So wakipata harufu fulan flan ambazo hawazipendi wanalewa na kutimua mbio.

Kwa hapa bongo balaa tupu. Mammbu ni mabishi. Ukiyapiga dawa ya ku-sprei ndo kwanza yanashangilia!
Mi huwa nawasha feni fulu spidi na kuyachapa haya mammbu usiku kucha na upepo. Nikiamka monii yametapakaa sakafuni hoi, mengine bado yanapumua. Ukiyaacha baada ya muda flan yanaamka na kula kona.

Kwa kifupi mbu wa Dar ni wabishi, huenda tukiupanda hapa Dar mbu watauzingira na kupata stimu kabla ya kushambulia binadamu.

Wale wanaopiga mara kwa mara ruti za Dar-Arusha hebu nunueni tuone demo. Usijekuta pia huo mti haukui ktk hali ya hewa ya Dar!
Ni hayo tu
 
Ndugu acha ujinga tumekwambia tupigie picha napo unajizungusha tu,pia tumekwambia tuambie mahali uliponunua huo mti bado umekuwa husemi sijui lengo lako lilikuwa lipi,huo ni ushamba wa enzi za ujima ,basi kaa na huo mti wako roho ikutue
 
mkuu umenichekesha. Kwa kweli mbu wa dar soo. Kuna kipindi fulani niliingia room na kukuta mbu kibao kwenye kona ya chumba wakipiga "pushap" wakijiandaa kwa msosi wao wa usiku.
 
Ndugu acha ujinga tumekwambia tupigie picha napo unajizungusha tu,pia tumekwambia tuambie mahali uliponunua huo mti bado umekuwa husemi sijui lengo lako lilikuwa lipi,huo ni ushamba wa enzi za ujima ,basi kaa na huo mti wako roho ikutue

Mkuu hebu soma (angalau kidogo) mabandiko ya Mfamaji.....
Picha ameshabandika na aliponunua amepataja... napendekeza Mfianchi umwombe radhi Mfamaji
.
 
Kwa mujibu wa 'risachi' ya kwetunikwetu huu mti hauwezi kumea maeneo ya pwani (inahitaji sehemu za mwinuko)!

Hili nafikiri nalo ni swala la kuzingatia...mwezi wa kumi na mbili nilichukua miti kama kumi hivi mizuri sana toka Kilimanjaro nikaipanda hapa Dar. Hivi sasa imebaki miwili nayo ipo mashakani:( Nilipoongea na mtaalamu akaniambia hiyo miti haikubaliani na hali ya hewa ya Mji huu. Inaitwa Thika Palm
 
Ndugu acha ujinga tumekwambia tupigie picha napo unajizungusha tu,pia tumekwambia tuambie mahali uliponunua huo mti bado umekuwa husemi sijui lengo lako lilikuwa lipi,huo ni ushamba wa enzi za ujima ,basi kaa na huo mti wako roho ikutue

Wewe wa wapi? Au ndio umeamka usingizini. Ujinga unao wewe usiyesoma sred.
 
Duuuu mshakaji itabidi na mimi niutafute, maana mbu nawachikia vibaya sana, maleria haikubaliki
 
kwetu kijijini hipo jamani ila jina na tulikuwa unakatamajani yake unajipaka kama upo mahali mbu wanakusumbua inafukuza ata ukilala unajipaka au unakata kitawi or majani unaweka kwenye kona moja kwishinei mbu akuna kabisa
 
.....indigenous knowledge, sometimes worth understanding!
 
Duuuu mshakaji itabidi na mimi niutafute, maana mbu nawachikia vibaya sana, maleria haikubaliki
Domo Kaya hii avatar yako nikiiona tu mwili unanisisimka!! uliitoa wapi hii?? Kwa jinsi avatar yako ilivyo wala huhitaji hata mti wa kufukuza mbu manake wenyewe wakikuona tu lazima watimue mbio.
 
sheee mi nimezimia kwanza baada ya kuiona, hayo meno mawili tu yamenimaliza,walaah mbu hapo hata akiacha plasmodia wote wanakufa kabla hawajasambaa
 
Kwenye hii thread nimeeleza unapatikana wapi na picha yake kama wengi walivyotaka. Ni Arusha jamani karibu vitalu vyote ipo.
 
kwetu kijijini hipo jamani ila jina na tulikuwa unakatamajani yake unajipaka kama upo mahali mbu wanakusumbua inafukuza ata ukilala unajipaka au unakata kitawi or majani unaweka kwenye kona moja kwishinei mbu akuna kabisa
Kwenda zako na Kiswahili chako cha Kihaya. Kwa nini pasipostahili "H" wewe unaweka, na panapostahili huweki.
 
Back
Top Bottom