Habari wakuu,
Watafiti kutoka chuo kikuu cha Bayreuth wamegundua kuwa mti uliopo kwenye mlima Kilimanjaro ni mrefu zaidi barani Afrika ukiwa na urefu wa mita 81.5. Miti 10 mirefu zaidi barani iliyopimwa tangu mwaka 2012 ina urefu kati ya mita 59.2 na 81.5 na upana wa mita 0.98 mpaka 2.55.
Kwa kawaida miti mirefu zaidi duniani huwa haipatikani barani Afrika.
=======
Wanasayansi wanasema kuwa wamegundua kile wanaamini kuwa ni mti mrefu zaidi barani Afrika. Mti huo uko bonde moja lililo Kaskazini Mashariki mwa Tanzania.
Wanasayansi kutoka chuo cha Bayreuth nchini Ujerumani, wanasema wanaamini kuwa mti huo unaopatiknan karibu na mlima Kilimanjaro ndio mrefu zaidi barani.
Mmoja wa wanasayansi hao alisema kuwa aliona mtu huo miaka 20 iliyopita, lakini ni hadi hivi majuzi wakitumia vifaa maalum walifaulu kupima urefu wake.
Mti huo kutoka familia ya Entandrophragma excelsum una urefu wa mita 81.
Wanasayansi nchini Tanzania bado hawajatoa taarifa yoyote kuhusu ugunduzi huo.
Wanasayansi waliogundua mti huo sasa wanataka ujumuishwe kwenye kumbukumbu ya miti isiyo ya kawaida duniani.
Chanzo: BBC
Siku chache baada ya wanasayansi kubaini mti mrefu zaidi barani Afrika katika Mlima wa Kilimanjaro nchini Tanzania sasa wataalam hao wamefanya ugunduzi mwengine kuhusu mti huo.
Wataalam hao kutoka chuo kikuu cha Beyreuth Ujerumani sasa wamegundua kwamba mti huo ndio ulio na miaka mingi zaidi duniani.
Kulingana na gazeti la Mwananchi nchini Tanzania, Mtafiti wa viumbe hai na mazingira kutoka Chuo hicho Dk Andrew Hemp ameelezea sifa za mti huo ujulikanao kama Mkukusu kuwa unaweza kuishi kati ya miaka 200 hadi 300, lakini ulioonekana nchini una miaka 600.
Mti huo unapatikana katika Kijiji cha Tema wilayani Moshi, na upo katika eneo lililopo kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (kinapa).
Dk Andrew amesema kwa mujibu wa utafiti mti huo una uwezo wa kuishi miaka hiyo kwa kutunzwa na kuhifadhiwa.
Kulingana na gazeti hilo la mwananchi ,Amesema kwamba katika utafiti walioufanya barani Afrika waligundua miti mirefu 31, lakini Mkukusu wa Moshi ndiyo mrefu kuliko yote na una umri wa miaka 600 hivi sasa ukiwa umevuka kiwango cha juu cha maisha ya miti ya aina hiyo.
Tayari Serikali imeiagiza Kinapa kuboresha miundombinu ya barabara ili kuweza kuufikia mti huo iwapo watalii watataka kwenda kuuona.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki amesema mti huo utasaidia kuongeza mapato kwa kasi kwa kuwa ni kivutio kipya cha utalii ndani ya mkoa huu.
Mhifadhi Mkuu wa Kinapa, Betrita Loibok amesema agizo hilo litazingatiwa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) ili mti huo uweze kuwa kivutio ndani na nje ya nchi.