Mti mrefu Afrika wagunduliwa katika mlima Kilimanjaro nchini Tanzania

..........."Wanasayansi kutoka chuo cha Bayreuth nchini Ujerumani, wanasema WANAAMINI ni mti mrefu zaidi barani Afrika" Nimependa zaidi hii sentensi

Hivi Imani ni nini vile!!???, Mnikumbushe wakuu.
 
Imegundulika kwamba, mti mrefu kuliko yote barani Africa umepatikana katika kijiji cha Tema Mkoani Kilimanjaro. Mti huo ambao una urefu wa mita 81, upo ndani ya eneo la Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA).

Mti huo ni miongoni mwa miti mingine mirefu 31 ambayo haiufikii mti huo kwa urefu.

========

Mtafiti wa viumbe hai na mazingira kutoka Chuo Kikuu cha Bayreuth cha nchini Ujerumani, Dk Andrew Hemp ameelezea sifa za mti ujulikanao kama Mkukusu kuwa unaweza kuishi kati ya miaka 200 hadi 300, lakini ulioonekana nchini una miaka 600.

Akiuzungumzia mti huo ambao unapatikana katika Kijiji cha Tema wilayani Moshi, mtafiti huyo amesema mti huo ambao ni mrefu kuliko yote barani Afrika una urefu wa mita 81.5 na uko katika eneo lililopo kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (Kinapa).

Dk Andrew amesema kwa mujibu wa utafiti mti huo una uwezo wa kuishi miaka hiyo kwa kutunzwa na kuhifadhiwa.

Amesema kwamba katika utafiti walioufanya barani Afrika waligundua miti mirefu 31, lakini Mkukusu wa Moshi ndiyo mrefu kuliko yote na una umri wa miaka 600 hivi sasa ukiwa umevuka kiwango cha juu cha maisha ya miti ya aina hiyo.

Tayari Serikali imeiagiza Kinapa kuboresha miundombinu ya barabara ili kuweza kuufikia mti huo iwapo watalii watataka kwenda kuuona.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki amesema mti huo utasaidia kuongeza mapato kwa kasi kwa kuwa ni kivutio kipya cha utalii ndani ya mkoa huu.

Mhifadhi Mkuu wa Kinapa, Betrita Loibok amesema agizo hilo litazingatiwa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) ili mti huo uweze kuwa kivutio ndani na nje ya chini ya nchi.


Chanzo: Mwananchi
 
Sasa huo unatusaidia nini??? Vifutio vya utalii tunavyo kibao - na tumeshindwa kuvitumia kwa kuongeza idadi ya watalii. Sasa mti mmoja ndio utasaidia nini??? Mbuga za Wanyama tunashindwa kuzitangaza ili watalii waje - itakuwa mti mmoja kweli?
 
Mmmhh!!!,We jamaa,Unatusaidia nini???!!!,Hujui kuwa Watalii wengi watakuja kuutazama na sisi tutajipatia fedha za kigeni?.
 
tema ipo mbokomu unaingilia hapo kiboroloni kupanda juu.mti huu ndipo ulipo gunduliwa.
 
Haina budi kutangaza maajabu kama haya....
Maana kutokana na uharibifu wa Misitu ni ngumu sana kwa nyakati za sasa kupata miti mirefu kama hayo...Hongera kwa waliohusika kuhifadhi...
Nawatakia weekend njema
 
Habari wakuu,
Watafiti kutoka chuo kikuu cha Bayreuth wamegundua kuwa mti uliopo kwenye mlima Kilimanjaro ni mrefu zaidi barani Afrika ukiwa na urefu wa mita 81.5. Miti 10 mirefu zaidi barani iliyopimwa tangu mwaka 2012 ina urefu kati ya mita 59.2 na 81.5 na upana wa mita 0.98 mpaka 2.55.

Kwa kawaida miti mirefu zaidi duniani huwa haipatikani barani Afrika.

entandrophragma_flm4_2_13-0001.jpg


=======
Wanasayansi wanasema kuwa wamegundua kile wanaamini kuwa ni mti mrefu zaidi barani Afrika. Mti huo uko bonde moja lililo Kaskazini Mashariki mwa Tanzania.

Wanasayansi kutoka chuo cha Bayreuth nchini Ujerumani, wanasema wanaamini kuwa mti huo unaopatiknan karibu na mlima Kilimanjaro ndio mrefu zaidi barani.

Mmoja wa wanasayansi hao alisema kuwa aliona mtu huo miaka 20 iliyopita, lakini ni hadi hivi majuzi wakitumia vifaa maalum walifaulu kupima urefu wake.

Mti huo kutoka familia ya Entandrophragma excelsum una urefu wa mita 81.

Wanasayansi nchini Tanzania bado hawajatoa taarifa yoyote kuhusu ugunduzi huo.

Wanasayansi waliogundua mti huo sasa wanataka ujumuishwe kwenye kumbukumbu ya miti isiyo ya kawaida duniani.

Chanzo: BBC
Siku chache baada ya wanasayansi kubaini mti mrefu zaidi barani Afrika katika Mlima wa Kilimanjaro nchini Tanzania sasa wataalam hao wamefanya ugunduzi mwengine kuhusu mti huo.

Wataalam hao kutoka chuo kikuu cha Beyreuth Ujerumani sasa wamegundua kwamba mti huo ndio ulio na miaka mingi zaidi duniani.

Kulingana na gazeti la Mwananchi nchini Tanzania, Mtafiti wa viumbe hai na mazingira kutoka Chuo hicho Dk Andrew Hemp ameelezea sifa za mti huo ujulikanao kama Mkukusu kuwa unaweza kuishi kati ya miaka 200 hadi 300, lakini ulioonekana nchini una miaka 600.

Mti huo unapatikana katika Kijiji cha Tema wilayani Moshi, na upo katika eneo lililopo kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (kinapa).

Dk Andrew amesema kwa mujibu wa utafiti mti huo una uwezo wa kuishi miaka hiyo kwa kutunzwa na kuhifadhiwa.

Kulingana na gazeti hilo la mwananchi ,Amesema kwamba katika utafiti walioufanya barani Afrika waligundua miti mirefu 31, lakini Mkukusu wa Moshi ndiyo mrefu kuliko yote na una umri wa miaka 600 hivi sasa ukiwa umevuka kiwango cha juu cha maisha ya miti ya aina hiyo.

Tayari Serikali imeiagiza Kinapa kuboresha miundombinu ya barabara ili kuweza kuufikia mti huo iwapo watalii watataka kwenda kuuona.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki amesema mti huo utasaidia kuongeza mapato kwa kasi kwa kuwa ni kivutio kipya cha utalii ndani ya mkoa huu.

Mhifadhi Mkuu wa Kinapa, Betrita Loibok amesema agizo hilo litazingatiwa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) ili mti huo uweze kuwa kivutio ndani na nje ya nchi.
 
Tanzania Tanzania Tanzania, Hongereni kwa kuhodhi Mti ambao ni mrefu kuliko yote Barani Africa , ujulikanao kwa jina la jina la Entandrophragma excelsum wenye urefu wa mita 81.5, unaopatikana katika Mzunguko wa muinuko wa mlima Kilimanjaro mkoani Kilimanjaro. Mti huo umegunduliwa nov 2016 na watafiti wa kijerumani ambao wamefanya utafiti katika mlima huo kwa takribani miaka 20. Mti huo kwa sasa ndi mti mrefu barani africa, baada ya uliokuwa unashikilia record hiyo mti wa south africa wenyewe ulikufa mwaka 2006 na ulikuwa na urefu wa mita 81.5 kama mti huo wetu.

Watanzania wengi hawajui hii taarifa kwasababu viongozi wa serikali na maliasili walikuwa busy na faru john.
Watafiti wanadai mti huo unaweza kukatwa na wachaga waishio kando na msitu huo kwani hauko katika eneo ambalo ni protected, kwa hiyo ni jukumu letu sote pamoja na serikali kuulinda mti wetu wa kihistoria. Mti umeweza kukua vizuri kwa maana ardhi ya mlima kilimanjaro huo ina rutuba iliopitiliza na unyevu unyevu usioisha mwaka mzima, watafiti wamesema mti huo unakadiriwa kuwa na umri wa miaka 600 hadi 800.

Pia mti huu unashika nafasi ya sita duniani kwa kuwa mti mrefu kabisa, mi naona ni jambo la kujivunia kwa watanzania,

Mkitaka majibu zaidi chombo cha habari kitengeneze documentary, naatach picha, taarifa hii niliisikia nikiwa masomoni ujerumani, na nilishanga sikuiona katika vyombo vyetu.
jimti 3.jpe
jimti1.jpe
jimti2.jpg
jimti4.jpg
jimti 3.jpe
jimti1.jpe
jimti2.jpg
jimti4.jpg
jimti 3.jpe
jimti1.jpe
jimti2.jpg
jimti4.jpg
 
Hawa wazungu wanaokuja kutusifia sifia mi ninawasiwasi nao sana...yaan tafiti nyingine sidhani kama zina ukweli wowote
 
Yaani jaman tuna viongozi wana vyeti lakini akili hawana..Tanzania we have everything we need wao wanabaki2 kupigiana kelele vitu vya kipuuzi wanakera sana
 
Kilimanjaro kuna hadi mapango , kuna ziwa linaitwa chemka kuna water fall ipo marangu sema serekali ipo bize na akina upinzani huku wajanja wakila pesa kama hio chemka hadi wazungu wanakujaga tunaogelea na tunatizwa kiingilio wajanja wanavila
Yes, Chemka it's the best place to be.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom