Mtendaji wa Ikulu na ujenzi wa majumba huko Morogoro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtendaji wa Ikulu na ujenzi wa majumba huko Morogoro

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kiumbo, May 20, 2012.

 1. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ni mtendaji wa ikulu kwa jina Mbena malumbi anafanya kufuru huko morogoro maeneo ya bigwa katika barabara ya zamani ya dar-moro kutokea mjini moro.

  Yasemwayo na wananchi wa huko ni kuwa watu wananunuliwa kwa hela yeyote ile unataja wewe wakita enao lako na kukuhamisha hata kama una makazi tayari.

  Washajenga hotel kando ya mto inaitwa Chilakale resort na live band yao ni hali ya juu sana.

  Pia kuna ujenzi unaendelea kando ya huo mto mpaka kwenye milima ya uluguru majengo yanainuka kama uyoga na wananchi wakizidi kununuliwa kila kukucha.

  Niliuliza nani ndio mhusika wa haya yote anatajwa huyo mtendaji wa ikulu.

  Naomba kuuliza wanajamvi mwenye taarifa kuhusu huyu mtendaji wa ikulu na utajiri wa kutisha kama huu kaupata wapi ama kuna watu nyuma yake.

  Hifadhi ya mlima Uluguru karibia yote washaichukua kwa mida ya usiku unaona umeme ukuwaka mlimani wakati huku wengine kuna mgao.

  Naomba tasaidiane mwenye taarifa rasmi kuhusu huyu afisa wa ikulu atujuze.

  Source ni mimi mwenyewe mkazi wa Moro. Naomba radhi kama sikufuata utaratibu wa uandishi.
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  wacha wajenge ndo wakati wao huu......

  Kidumu chama cha mapinduzi
   
 3. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Badili tabia ni kweli ni wakati wao huu ila ukifika wakati wetu sisi watakimbia nchi hawa. Mtu ananunua mlima ambayo ni hifadhi ya taifa.
   
 4. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Maelezo yako yote kwenye huo uzi wako upo kimajungu sana, point ninayoiona hapa ni hii ya kujengwa kwenye hifadhi ya Taifa, lakini mtu kuwahamisha watu kwa maana ya kununua maeneo yao mbona ni jambo la kawaida sana. Kwa kifupi mimi nimeishi sana hapo Morogoro kigurunyembe eneo la bar ya Equator by then (1999) na wakati huo huyo jamaa ndo alianza kujenga, nakumbuka mwaka 2002 niliwahi kwenda hotel ile, ilikuwa inapokea wageni huku ikiendelea na ujenzi.

  Hoja yangu hapa nataka kukwambia kuwa huyo jamaa hajaanza kujenga juzi ameanza long time almost 12 yrs, hata kama ni wewe development ya eneo unalojenga lazima lionekane, na zaidi ina maana kwamba kwa kipindi chote hicho amehudumia wageni wengi kiasi cha kuzidi kujiwekeza zaidi!
   
 5. Raiamwematz

  Raiamwematz Senior Member

  #5
  May 20, 2012
  Joined: May 9, 2012
  Messages: 104
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kikubwa ni kujua tu amejenga hiyo hotel kwa kutumia vyazo vipi vya hela, je viko halali? Kuhusu huo Mlima, hapo siwezi kukubariana na wewe, kwani huo mlima sehemu kubwa ipo katika hifadhi asilia, na sio rahisi mtu kuinunua. Hivyo angalia vizuri juu ya hili, linaweza likawa sio sawa, kuitetea hoja yako.
   
 6. Jallen

  Jallen JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 497
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Acha wajenge wamebakiza miaka mitatu tu waondoke maana hawataiona tena Magogoni. Zaidi tutawahoji hizo mali walizipata wapi. Mwisho wao uu karibu.
   
 7. JAPUONY

  JAPUONY JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 374
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mbena ni Msaidizi wa JK.
   
 8. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Jingle bells jingle bells all the time awaaaaayyyy
   
 9. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  kwa wanao beza ni magamba nawajua. Je hizo mali na mamilioni ya hela anayomwaga ni halali ama si halali.
   
 10. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Ameona jinsi kijiji cha Msoga kilivyojengwa na yeye amemuiga boss wake!!Wanachukua vyao mapema wanajua hii ndio lala salama; lakini ole wenu mtakujatolewa kwenye mitaro mtakakokuwa mnajificha arobaini yenu itakapowadia!!!!
   
 11. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  chilakale resort imejengwa mwaka jana na ikafunguliwa pasaka mwaka huu..je hzi mali anamiliki kihalali.
   
 12. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #12
  May 20, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Huyo Mlambena Malumbi anatisha kwa utajiri pale Morogoro na wala siyo majungu.

  Watu wana haki ya kuuliza mfanyakazi wa kawaida serikalini kama yeye anapata wapi huo utajiri wa kufuru.

  Ieleweke kwamba ule wakati wa kuwaona wahujumu/mafisadi wa mali za uma ndiyo wajanja unatakiwa uishe.

  Hawa watu wanatakiwa waadhibiwe kama wahalifu wengine.

  Haiwezekani mtu huyu ambaye ana nyumba za nguvu kila mtaa manispaa ya Morogoro na zote hazitumiki awe au mtu atuaminishe kwamba anapata pesa yake kihalali.
   
 13. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #13
  May 20, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Pesa halali inajenga nyumba ya tofali za udongo na tembe.
   
 14. K

  Kidogo chetu JF-Expert Member

  #14
  May 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,385
  Likes Received: 774
  Trophy Points: 280
  Hao ndio wenye Menoooo
   
 15. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #15
  May 20, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwa kuzidi kutoa data. Magamba wanabeza tu hu. Inatisha.mu
   
 16. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #16
  May 20, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Kwa nyongeza tu na kwa faida ya wanamajungu, mlimani juu ya eneo inapojengwa hotel hiyo kuna watu kibao wanaishi huko. Kuhusu uwezo wa kukenga; mbena malumbi amekuwa na mabasi madogo(coaster) kwa muda mrefu yanayofanya kazi kati ya dar na ifakara, sijui kigezo cha kuhoji ujenzi huu ni kua afisa wa ikulu(ambayo haijathibitishwa) au ni kujenga kwenye hifadhi ya mlima(hii siyo kweli)ama ni kujenga kwa kuhamisha watu(kwangu ni maendeleo), tuache majungu.
   
 17. g

  gotolove Member

  #17
  May 20, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama msaidizi hivi, bosi wake itakuwaje?
   
 18. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #18
  May 20, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Watanzania kwa kupenda kubebesha mambo kwa wakubwa hamjambo, alipojenga hotel kule chanika walisema ni hotel ya Sumaye, leo mnasema anasiamamia mali za kikwete/Rz1, mi siwaelewi. Nijuavyo ni kuwa hotel ya Moro imeanza kujengwa zaidi ya miaka 12 iliyopita, na kuwa huyu mtu anamiliki open investments, hayo mengine yenu.
   
 19. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #19
  May 20, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ni msaidizi wa jk tuu duu. Hiyo chilakale resort ipo bigwa darajani. Ule ni kama uwekezaji sio kawaida. Kuna rafiki yangu alikuwa na kaeneo pale na kibanda kapewa 100 mil cash. Huyo ni baadhi ya watu walimwagiwa hela. Na kuna wakati mama mkuu wa kaya alionekani huko juu mlimani kwenye majumba akiwa na vx v8 tinted. Huko kuna magari ya utalii km 20 mapya yameifadhiwa tu.

  Kuna tetesi za wenyeji kuwa kuna mbuga ya selulos iko huko matombo na madini flani wamarekani wamepewa ndio hio miradi anapamba moto. Ujenzi ukikamilika na uwanja wa ndege mdogo utajengwa huko mlimani. Haya yanasemwa na mafundi wanaojenga huko na wenyeji. Hili jambo msichulie kirahisi hivyo eti mradi wa vibasi ndio ujenge majumba ya mabilion mtedaji wa serikali sehumu nyeti kama ikulu.

  Walio moro watasema ukweli kuhusu yanayoendelea kwa sasa na utajiri wa mbena malumbi.
   
 20. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #20
  May 20, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  gama hiyo chilakale resort huikujegwa kwa miaka 12 wacha uongo lile eneo tulikuwa tunaokota maembe dodo pale na mmiliki na mjua mpaka akawauzia hawa jamaa mwaka jana na ujenzi ulianza mara moja. Kuna wafanyabiashara wa mabasi wangapi lakini hakuna faida ya mabillion kama huyu unavyomtetea labda nawe ni mnufaika. Yale yale ya kina maige na malori 2 faida 40,000 dola kwa mwezi. Ni uongo mtupu. Huyo abood hawezi fanya kufuru kama hiyo na utajiri wake wa mabasi ni biashara nyingine. Tembelea bigwa ukaulize wenyeji kuhusu huyo mluguru wao utapata mengi.
   
Loading...