GE2025 Mtendaji Bodi ya Ithibati: Ni kosa la Jinai kufanya uandishi wa habari bila Ithibati, adhabu ni kifungo miaka mitatu

GE2025 Mtendaji Bodi ya Ithibati: Ni kosa la Jinai kufanya uandishi wa habari bila Ithibati, adhabu ni kifungo miaka mitatu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
889
Reaction score
2,863
Akizungumza leo kwenye Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Habari Kanda ya Mashariki Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 Wakili Msomi Patrick Kipangula Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari amesema kwamba kwa waandishi wa habari ambao hawana Ithibati na wakaendelea kufanya uandishi wa habari basi adhabu yake ni hadi kifungo cha miaka mitatu.

Hapana, kwa mtazamo wao wabunge ambao wanasimamia sera na mustakabali wa nchi nzima hawana umuhimu wa kuwa na elimu ukilinganisha na wana habari ambao wanaripoti yaliyojiri tu.
Habari ni zaidi ya kuripoti yanayojiri, ndiyo maana husomea, hakuna sehemu kuna kozi ya ubunge,mbunge ni muwakilishi wa watu,watu watachagua wammpendae
 
Kwa nini afanye kazi bila ithibati na anajua sharti athibitishwe!?
Profession ya uandishi ni pana mno. Kuna wale wanaosomea chuo kikuu, na kuna wanaopata uzoefu wa vitendo. Kuna waandishi ambao wanaandika kutokana uzoefu wa taaluma zao ( wapishi, madaktari, lawyers, wahandisi, viongozi wa dini, uzazi n.k.). Hao wote watakuwa wamevunja sheria wakifungua blog kuhusu fani zao? Au nimechanganya mada kwa sababu sielewi maana ya ithibati?

Amandla...
 
Ndiyo, watakua wamevunja sheria ikiwa hawajathibitishwa
 
Mimi nilijua wanatakiwa wajue kusoma na kuandika tu kama ndugu zetu wabunge
Ajabu ya tz,mbunge ajue kusoma na kuandika mwandishi habari ajue zaidi ya kusoma na kuandika!je huyu mbunge wa kujua kusoma na kuandika atawezakumwelewa?
 
Waliothibitishwa ndo akina Miladi ayo. Wanaogopa ogopa
 
Back
Top Bottom