Mtei Express! Yachafua hali ya hewa kabla ya kufunga mwaka!

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,348
3,219
Katika hali ya simanzi na isiyotarajiwa na wengi basi la kampuni ya Mtei Express inayofanya roots kt ya Jiji la Arusha na Mkoa wa Manyara leo alasiri ilipinduka ktk barabara ya Arusha Babati eneo la Kisongo CMC area na kujeruhi watu zaidi ya 20 na hata hivyo kuna hofu ya watu kupoteza. Ilikuwa ni mteremko mkali kwa wastani na kubasti tairi ya mbele na ndipo akashindwa kulimudu na likapinduka kushoto mwa barabara kama unatoka Arusha kuelekea Manyara. Kwa kweli ndipo lile neno linakamilika ya kwamba "NI MAJALIWA YAKE MUNGU KUIONA MWAKA" na nikapenda kuwatakia majeruhi pole nyingi wapone mapema waendelee na ujenzi wa Taifa.

Source: Ni kwa aliyetoka eneo la tukio!
 
hata mie nimesikia habari hii
tunawaombea majeruhi afya njema wapone waungane na familia zao kwenye sherehe ya mwaka mpya 2012
 
Mida ya mchana nilikuta wakiliinua basi hilo habari ambazo sikuweza kuziamini maramoja zilisema kuwa watu 4 wali RIP Habari zaidi zinakuja soon
 
Mida ya mchana nilikuta wakiliinua basi hilo habari ambazo sikuweza kuziamini maramoja zilisema kuwa watu 4 wali RIP Habari zaidi zinakuja soon

Dud! Ama kweli lusfa anatawanya majeshi yake.

Shindwa pepo wa kuzimu! Shindwa! Shindwa na hata ulegee!! Hauna mamlaka kwa mji wa waliohai! Shindwa!

Waliopatwa na msiba poleni sana na MUNGU mwenye uweza awajaze nguvu ktk wakati huu mgumu! Na marehemu wote walale kwa AMANI ya Bwana!
 
hili gari si lilipataga ajali mwaka jana mitaa ya hedaru??tarehe hizi hizi mmesahau?
 
shetani ashindwe na alegee kwa jina la YESU,majeruhi wapone haraka.
 
Ifikie kipindi wamiliki wa mabus waache kufunga mbele tyre za bei chee zina bust ovyo ovyo
 
Ifikie kipindi wamiliki wa mabus waache kufunga mbele tyre za bei chee zina bust ovyo ovyo

Wanapenda tairi ya bei rahisi.

Pendekezo Mi naona kungetengwa kituo cha kuuza tairi ambayo special kwa magari ya abiria.

Ni wazo tu!
 
Magari haya nayo yanaenda kasi sana na polisi kila mara wanapokea rushwa kutoka kwa makondakta.

Inasikitisha!
 
Poleni wafiwa wote na majeruhi! Mtei ilishawahi kupinduka miaka ya nyuma eneo hilo hilo. Kweli kuiona na kuimaliza siku ni majaaliwa yake Mwenyenzi
 
Poleni wafiwa wote na majeruhi! Mtei ilishawahi kupinduka miaka ya nyuma eneo hilo hilo. Kweli kuiona na kuimaliza siku ni majaaliwa yake Mwenyenzi

Yani pale kwa wasio na matumaini watahaha sana!

Ole wao kwa wale wasiona matumaini!
 
Wanapenda tairi ya bei rahisi.

Pendekezo Mi naona kungetengwa kituo cha kuuza tairi ambayo special kwa magari ya abiria.

Ni wazo tu!

Wanajifungia mitairi ya kichina bei chee badala ya kufunga Bridge stone au Michelin unakula bus tairi za mbele zimepigwa Yong Ling alafu kipara sasa abiria mkishuka mnaomba Mungu hizo tairi zisijibu maana mmmh
 
Kwa kuwa mabasi yamekuwa yakipinduka na kujeruhi na mara nyingine kuua, napendekeza serikali ichukue hatua madhubuti kukomesha tishio hili la maisha ya raia wasio na hatia, ikiwezekana ipige marufuku matumizi ya mabasi kama si magari yote kwa usafiri wa abiria. lengo la ushauri wangu ni kuondoa tishio la kuuawa ama kujeruhiwa na mabasi/magari. serikali ichukue hatua kama ile ya kuzuia matumizi ya ardhi kwa wakazi wanaoweza kufikiwa na mafuriko yasababishayo majeraha uharibifu wa mali na maafa, poleni wafiwa na majeruhi, RIP marehemu
 
Unanikumbusha general tire, kuiua ni kujipotezea uwezo wa kudhibiti ubora wa matairi tuyatumiayo! ling long.....! du!
 
Unanikumbusha general tire, kuiua ni kujipotezea uwezo wa kudhibiti ubora wa matairi tuyatumiayo! ling long.....! du!

Nimegundua sisi waswahili hatuwezi kabisa kujisimamia lazima awepo mkoloni nyuma ndo tutaendelea
 
Kwa kuwa mabasi yamekuwa yakipinduka na kujeruhi na mara nyingine kuua, napendekeza serikali ichukue hatua madhubuti kukomesha tishio hili la maisha ya raia wasio na hatia, ikiwezekana ipige marufuku matumizi ya mabasi kama si magari yote kwa usafiri wa abiria. lengo la ushauri wangu ni kuondoa tishio la kuuawa ama kujeruhiwa na mabasi/magari. serikali ichukue hatua kama ile ya kuzuia matumizi ya ardhi kwa wakazi wanaoweza kufikiwa na mafuriko yasababishayo majeraha uharibifu wa mali na maafa, poleni wafiwa na majeruhi, RIP marehemu

Mkubwa!

Uko sahihi sana lakini mafisadi hawaoni wala hawasikii.

Tuna hasara na serikali legelege ya Jk!
 
Back
Top Bottom