classic! kuna watu wanataka tuamini tu bila hata kuhoji kuwa endapo tungefanya kila kitu ambacho IMF imetushauri kufanya tusingekuwa hapa tulipo. Well.. miaka 25 iliyopita tumefanya kila kitu ambacho WB, IMF, UNDP, UNICEF, ADB na wenzake wanayotaka tufanye je tunaweza kusema kweli hali yetu ni bora zaidi? Kufanya yote ambayo Mtei alishauri isingekuwa a panacea ya matatizo yetu kama taifa. Ingekuwa just that - tumefanya tuliyoambiwa na wakubwa kufanya hata kama hayakubaliani na misingi yetu kama taifa. Pamoja na heshima yangu yote niliyonayo kwa Mzee Mtei leo hii mapendekezo yake yamefanyiwa kazi kuanzia Mwinyi hadi Kikwete, ameridhika?
Hiyo UDOM ni govt bond ambayo NSSF imewekeza kwa serikali. hii inatisha NSSF kuinvest 48% kwenye govt bonds.Hivi UDOM inajengwa kwa mapato ya ndani? Nilifikiri ni mkopo wa ndani kwa kupitia NSSF, PPF etc...But also haya mashirika si mashirika ya umma ambayo ni mabaki ya sera za ujamaa?
Moja ya mambo mtei aliyo mshauri Nyerere ni kuacha kusubsidize haya mashirika kama NMC. Kuyaacha haya mashirika yaendeshwe na watu binafsi.
Mifano ya leo ni kuwa baharesa na wauza chakula wengine wanafanya kazi vizuri tu..
Leo hii TZ breweries wamefungua kiwanda kingine mbeya, wakati wa enzi zile usambazaji wa bia tu ulikuwa unawashinda...
Kama hii sera ingetekelezwa kipindi kile viwanda vyetu vingi vingekuwa hai na vinauza mpaka nchi jirani, sasa hivi viwanda vyetu vingi vinapiagana market ya ndani.
Mabadiliko ni makubwa sana yaliyoletwa na hii sera ya ubinafsishaji sio kwa viwanda tu hata kwa bank zetu, productivity imeongezeka.
Haya mashirika yako katiaka hali mbaya sana kifedha yaani yana pension deficit kubwa sana sijui itakuwaje uko mbeleni. watu wanasumbuliwa sana kupata pension zao.
Haya mashirika yanatakiwa ya binafsishwe ili yaendeshwe kwa ufanisi zaidi. Hizo hela zilizopotea ingekuwa private company watu wangekuwa wananyea debe siku nyingi. Siku haya mashirika yatakapokuwa mahututi ndio tutatafuta wawekezaji
haya mashirika yamewekeza katika miradi ya umma kwa ajili base rate kipindi cha balali ilikuwa juu sana, na kuinvest kwenye govt bonds ni safe kuliko kukopesha. sasa hivi ndulu amejitahidi mpaka base rate ikashuka kwa hiyo returns ni ndogo na hawa jamaa wamepunguza kuwekeza kwenye govt bonds.1. Kwa taarifa niliyonayo ni kuwa haya mashirika yana fedha nyingi mno hazina cha kufanyia na ndio maana sasa wanahimizwa sana katika kuinvest katika miradi mikubwa ya umma
2. Hi solution ya kukukimbilia kubinafsisha kila kitu inatisha. Hivi huko mnapocopy utume wa ubepari kama marekani nao wamethubutu kubinafsisha Social Funds?
Mnasahau Kwamba ni Mwalimu ndiye alimruhusu Mwinyi kukubaliana na IMF? There was no choice. Sasa kama mwishowe unakubali dawa, si ingekuwa bora kuikubali kabla ya kuingia ICU? Hali mbaya tuliyokuwa nayo miaka ya 78 - 85 ilitokana na kiburi kisichokuwa na msingi mzuri.Hivi kati ya nchi zilizokubali kuwapigia magoti hao proxies wa Washington Consesus ni ipi ambayo iliepuka huo umahututi?
Mwalimu aliamini kwa dhati katika ujamaa, iweje mtegemee akubaliane na ushauri wa kuwapigia magoti the very people ambao walifanya wazi kuwa nia yao kuu ni kuhakikisha kuwa ujamaa haufanikiwi.......Hivi hadi sasa baada ya kukubali kufakamia huo ubepari ni nini kimeongezeka zaidi ya ulimbukeni wa tabaka tawala?
omarilyas
Hapana. Mwalimu amefariki bila kukubaliana na IMF. Kwenye kikao chake cha mwisho hapa Washington aliwasuta na kuwaambia "have some humility."Mnasahau Kwamba ni Mwalimu ndiye alimruhusu Mwinyi kukubaliana na IMF? There was no choice. Sasa kama mwishowe unakubali dawa, si ingekuwa bora kuikubali kabla ya kuingia ICU? Hali mbaya tuliyokuwa nayo miaka ya 78 - 85 ilitokana na kiburi kisichokuwa na msingi mzuri.
Kama wewe ni mzima unaweza kugombana na daktari. Lakini mgonjwa utagombana na daktari?
Nchi nyingi za Afrika zimeanza tena kuendelea baada ya kufuata masharti ya IMF. Tanzania ni mojawapo.
Mwishowe Mwalimu alikubaliana na IMF. That is a historical fact.
Hapana. Mwalimu amefariki bila kukubaliana na IMF. Kwenye kikao chake cha mwisho hapa Washington aliwasuta na kuwaambia "have some humility."
I have no problem with history proving Mtei right. Katika hali yetu baada ya vita na Uganda na baada ya western countries to gang together under Reagan's pressure to force Tanzania to bend hatukuwa na choice. It was not a matter of Mwalimu kumruhusu Mwinyi kuwekeana mkataba na IMF. It was the prudent thing to do. But this did not change Mwalimu's belief that IMF' s prescription were not panacea.Mwinyi hakuruhusiwa na Mwalimu kuwekeana mkataba na IMF? Mwalimu hakukubali IMF inafanya vizuri. Ila alikubali Tanzania ifikie makubaliano na IMF. Angeruhusu hivyo mapema hatungeshuka kiasi kile.
Si lazima ukubali msimamo wa IMF ndio ukubaliane nao. Ukitaka kuwa jeuri basi uwe kweli mwenye uwezo wa kujitegemea. Kama lazima kusalimu amri, basi usichelewe mpaka ukazdiwa kabisa.
History has proven that Mtei was right.
Na Mussa Juma
GAVANA wa kwanza wa Benki Kuu Tanzania(BoT) na aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha katika utawala wa Baba wa taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Edwin Mtei amemtahadharisha Rais Jakaya Kikwete atakabiliwa na matatizo makubwa kama hatakuwa mkali na kuwachukulia hatua watendaji wake wanaotuhumiwa kwa ufisadi.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Mwananchi Jumapili nyumbani kwake eneo la Tengeru, mkoani Arusha mwanzoni mwa wiki hii, Mtei alisema baadhi ya wasaidizi wa Kikwete watasababisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kianguke katika uchaguzi mkuu mwakani kutokana na kuchafuliwa na tuhuma mbalimbali.
Mtei alisema wasaidizi wengi wa Kikwete hawaaminiki tena katika jamii, hivyo wananchi watapiga kura za hasira ili kuing'oa CCM madarakani.
Ni vyema Rais Kikwete akawatazama upya wasaidizi wake, kwani wengi hawamsaidii na kama ataendelea kucheka nao nchi hii inaelekea pabaya, hivyo lazima akubali kuchukua maamuzi magumu kama anataka mambo yawe mazuri, alisema Mtei.
Alisema hali inakoelekea nchi yetu imewahi kutokea katika nchi nyingi ambako viongozi wake wameondolewa madarakani kwa kushindwa katika uchaguzi kutokana na kucheka na wasaidizi wao wazembe na wabadhilifu, badala ya kuwachukuliwa hatua kali.
Mtei ambaye pia ni muasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alitoa mfano wa serikali ya chama tawala cha KANU, nchini Kenya kuwa kilikosa mwelekeo kutokana na viongozi wake kujaa tuhuma mbalimbali chafu.
Kuhusu watalaam kukimbia nchi, alisema inachangiwa na mfumo mbaya wa malipo ya kustaafu ambao hauwiani na mishahara yao.
Tanzania kuna wasomi wazuri, lakini wanaikimbia nchi kwa sababu mishahara yao ni midogo sana na wakistaafu hawana uhakika wa maisha mazuri, tofauti na wanasiasa, alisema Mtei.
Alisema kuna mambo mengi ya msingi ambayo yanapaswa kufanywa na Rais Kikwete, ikiwemo kuwa na mijadala ya kitaifa itakayosaidia kutoa suluhisho kwa matatizo yanayoikumba nchi, ili kuondoa tabaka kwa Watanzania wachache wanaoneemeka na rasilimali za nchi, huku kundi kubwa likibaki katika hali ya umasikini.
Mtei alisema Mwalimu Nyerere, aliweza kuongoza vema kutokana na kuwa mkali na hakusita kuchukua hatua dhidi ya kiongozi yoyote alipopata tetesi kwamba, anahusika na ubadhilifu.
Mwalimu alikuwa anatuita na kutueleza kwamba,Tanzania kuna watu zaidi ya milioni 20 (wakati huo) wenye uwezo wa kushika nafasi za uongozi, hivyo yoyote kati yetu kama sio msafi atatoka na aliwaondoa wengi, alisema Mtei.
Mwanasiasa huyu mkongwe, alisema si vizuri Rais Kikwete kuwa na msaidizi ndani ya serikali au chama ambaye anatiliwa shaka na wananchi.
Ndio maana wakati wa Nyerere, viongozi wengi walikuwa wanakimbia nchi, kwani ikibainika tu kuna dosari ni lazima mhusika atachukuliwa hatua haraka, alisema Mtei.
Alisema ni aibu, hivi sasa unasikia kuna kiongozi ana fedha nje ya nchi zenye utata,lakini hakuna hatua zinachukuliwa; jambo ambalo halikuwahi kutokea wakati wa Nyerere.
Wakati ule Benki Kuu ndiyo ilikuwa inahusika na uchunguzi wa fedha nje ya nchi na tulipobaini kuwa mtu fulani ana fedha nje, tulikuwa tunampa taarifa mwalimu na yeye alikuwa mkali sana na kuchukuwa hatua haraka, alisema Mtei.
Alisema baaada ya kupitishwa Azimio la Zanzibar lililoua Azimio la Arusha, hakuna tena miiko ya uongozi na viongozi hawana woga wa kufanya biashara jambo ambalo pia ni hatari kwa taifa.
Nampongeza Rais Kikwete kwa kubaini hili na kutoa utaratibu wa mtu kuchagua moja kati ya siasa na biashara, hili ni jambo zuri na katika nchi hizi masikini ni lazima kuwepo miiko ya aina hii, alisema Mtei.
Akizungumzia kashfa ya ununuzi wa mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya Dowans, Mtei alisema wakati wa Nyerere jambo hili lisingewezekana hata kujadili.
Wakati ule kama kampuni yako au shirika likibainika tu linajihusisha na rushwa katika masuala haya ya manunuzi kulikuwa na faili jeusi la makampuni na ikiingizwa humo huwezi kupewa kazi yoyote ya serikali bila kibali maalumu cha waziri wa fedha, alisema Mtei.
Alisema kwa suala la Dowans ni wazi, kampuni hiyo ina uhusiano na Kampuni ya Richmond hivyo kuingilia katika mjadala wa kununua mitambo ambayo tayari iliwahi kutiwa doa ni jambo lisilopaswa kupewa nafasi hata ya kujadiliwa.
Akizungumza mfumo wa maslahi ya watumishi wa umma; alipendekeza kuwa Rais Kikwete aunde tume maalum ya kupitia mishahara na marupurupu yote ya watumishi wa umma.
Hivi sasa hakuna uwiano katika malipo, kuna watu wanalipwa fedha kwa siku moja ambayo ni malipo ya mshahara wa mwezi wa mtumishi mwingine jambo ambalo lazima litazamwe, alisema Mtei.
Alifafanua kwamba, hata mfumo wa malipo ya wastaafu unapaswa kurekebishwa ili ulingane na malipo ya wastaafu wa ngazi za juu serikalini.
Tunapaswa kuwa na mfumo ambao utamwezesha mstaafu kuishi maisha mazuri na sio kufa baada ya kustaafu, alisema Mtei.