Balaaa akiongea na nani. “Siku rahisi ilikuwa ni jana, leo ni siku ya mchezo na mchezo huu unasheria zake, usiucheze kama huzijui sheria hizo.” Mtu yule aliongea kwa sauti ya chini lakini ilisikika vema masikioni mwa Nyaswe, akageuka kumtazama aliyekuwa akiongea, lakini kasi ya kugeuza shingo yake ilikuwa nyuma ya kasi ya matendo ya mtu yule, ambae aliongea na kuinuka mara moja huku akiacha mgongo wake ukiwa mali ya macho ya Nyaswe, lakini sura haikuonekana na hilo ndilo lilikuwa lengo lake, hakutaka Nyaswe amuone lakini alitaka ujumbe ufike. Naam, ujumbe ulifika kama ulivyokusudiwa lakini mpokeaji alibaki kwenye kiwewe na asijue alitakiwa kufanya nini, maneno hayo haikuwa mara ya kwanza kukutana nayo, tofauti pekee ni kwamba, mara ya kwanza aliyasoma na mara ya pili aliyasikia kwa masikio yake. Mwili wake ulitetemeka, ngozi yake ikajikunja kwa baridi ya ghafla ambayo hakujua ilitokea upande gani katikati ya jua la utosi, yale machozi yaliyokuwa na juhudi za kulowesha mashavu yake, yalikatika na hayakumtoka tena, macho yalibaki na ukavu kama vile hayakuwahi kutiririsha mifereji ya majichumvi. “Majura!” Aliwaza huku akichukua simu yake aliyokuwa ameihifadhi kwenye titi la kushoto na kuibana vizuri na sidiria, akaingia sehemu ya kutuma ujumbe mfupi, akaandika maneno machache na kutuma, wakati huohuo tumbo lake liliunguruma mithili ya mgonjwa wa kuendesha. Hofu ilikuwa ni kubwa kuliko ujasiri. Hata mtoto wake aliyekuwa tumboni na juhudi za kupiga mateke, alitulia tuli, aliuhisi unyonge wa mama yake.
Baada ya kutoka viwanja vya mashujaa, Majura aliwasiliana na mtu muhimu sana kwake, mtu ambae mara kadhaa amekuwa akifanikisha utimilifu wa baadhi ya taarifa zake, mtu huyo kwake alikuwa ni chanzo cha habari zenye uhakika. Hata wakati ujumbe mfupi ulipoingia kwenye simu yake hakujali, aliendelea kuongeza kasi ili kumuwahi mtu huyo ambae alimwambia atamsubiri kwa dakika nne pekee, baada ya hapo asingeliweza kuonana nae kwa sababu alikuwa akiingia zamu ya mchana. Majura alitembea bila kujali kama alikuwa eneo la jeshi na ilihitajika umakini kwa kila tendo, ili kuepuka kuingia matatizoni. Hakuwa mgeni wa baadhi ya maeneo ya wazi ndani ya ile kambi kubwa iliyomeza hekta kadhaa za maeneo, ungeliweza kutenga muda wa kuizunguka kwa siku nzima na usiiguse hata robo ya eneo lote. Wakati akiwa amebakiza hatua chache kabla ya kuingia kwenye mgahawa wa jeshi, simu yake iliita. Haraka haraka akaitoa, jina lilikuwa ni la yule aliyekuwa akitarajia kuonana nae, akaipokea. “Kuna kitu hakipo sawa, naomba tuonane usiku nikitoka zamu.” Upande wa pili ulisema na kukata simu, Majura alibaki akiwa ameganda mbele ya mlango wa kuingilia mgahawani, haikuwa kawaida miadi kuvunjwa kwa sababu ya kuwahi kuingia zamu, mara kadhaa waliwahi kukutana na kupoteza zaidi ya dakika kumi au kumi na tano na mlengwa hakuwahi kuharakisha kama ilivyokuwa siku hiyo, kuwa zaidi mtu huyo hakuwahi kumwambia wataonana baadae. Mara zote hukutaka kwenye huo mgahawa wa jeshi, taarifa zote alizohitaji alikuwa akipewa hapohapo mgahawani na si sehemu nyingi. Kiunyonge kabisa aligeuka ili aondoke, akakumbuka kuusikia mlio wa ujumbe mfupi kabla hajapigiwa na mtoa taarifa wake, akairejea simu yake na kuifungua sehemu ya jumbe fupi. ‘Achana na hili suala, ni kubwa sana kuliko tunavyodhani. Nakusihi.’ Aliusoma ujumbe kutoka kwa Nyaswe Katarama. “Jambo gani linafichwa?” Alijiuliza huku akiandika ujumbe kwenda kwa mdogo wake alimuuliza ni kwa nini aachane na jambo hilo ikiwa lina utata? Sekunde chache baadae alipokea majibu ambayo hakuona kama yanaweza kumfanya aridhie alichoambiwa. ‘Nikirudi tutazungumza. Nafsi yangu haioni sababu ya kuwa na mashaka tena.’ Aliusoma mara mbili ujumbe huo, akatikisa kichwa kwa masikitiko. “Kitu gani hiki? Inawezekanaje mtu aliyekuwa na wasiwasi kuhusu kifo cha mumewe ghafla aseme haoni sababu ya kuwa na mashaka? Haiwezekani, lipo jambo.” Aliwaza huku akitembea kwa kasi kurejea kwenye viwanja vya mashujaa, alitaka kuzungumza na Nyaswe kwa mara nyingine, alitaka amshiwishi amwambie chochote alichokijua. Majura alikuwa kwenye hali yake halisi ya kazi, kwenye hatari ndipo alipoamini kuna habari anazotaka na hadi wakati huo kwa uzoefu wake, alishajua kuna tatizo lakini litakuwa na gharama kubwa endapo atataka kulijua, gharama ni kwa sababu ya aina ya taasisi iliyokuwa ikilikumbatia jambo hilo. Aliamini kama kutakuwa kuna tatizo basi, lazima limeanzia jeshini kwa sababu shemeji yake alikuwa ni mtumishi ndani ya jeshi. “Halafu!” Alisema kwa sauti aliyoisikia mwenyewe, akasita kuendelea na safari huku akikumbuka jambo; miezi michache nyuma aliwahi kukutana na jambo linalohusisha jeshi lakini aliamua kuachana nalo kwa sababu wakati huo alikuwa kwenye sakata kubwa la kuibua ufisadi kwenye ujenzi wa bandari kavu huko mkoani Dodoma, hata baada ya kufanikiwa kuibua ufisadi huo ambao ulitikisa nchi na kuwaacha baadhi ya viongozi wakiwa hawana madaraka, jambo hilo lilikuwa limeshakiacha kichwa chake na hakuliwaza tena hadi wakati huo alipolikumbuka. “Waliniachia namba zao.” Aliwaza huku akikagua kitabu cha namba kwenye simu yake. “Niliziweka wapi?” Alijiuliza huku akianza kupiga hatua kwa kuchukua uelekeo wa kutoka nje ya kambi, alighairi kurejea kwenye hafla ya kuiaga miili ya wanajeshi, alilipa uzito jambo alilokumbuka. Majura hakuwa mtu wa kuogopa kufuatilia jambo lolote lenye utata, hakuogopa vitisho wala kumwogopa yeyote ili mradi alikuwa akisimamia misingi ya kazi yake bila kuvunja sheria, aliamini Mungu alimleta Duniani kufukua ya sirini na kuyaweka hadharani ili walimwengu wajue yaliyojificha. Hakuogopa kuchukiwa na watu wachache aliokuwa akiingia migogoro nao, wala hakuwahi kuogopa vitisho vya mtu yeyote na mara zote alichojali ni kuwa na tahadhari yake binafsi, kwa kuwa aliamini si wote watamkatia tamaa na kumwacha atambe mtaani, ijapokuwa wengi hawakuifahamu sura yake na kwenye gazeti habari zake huzikuwahi kuandikwa kwa jina lake halisi, lakini aliamini wenye shida nae ni lazima watakuwa wanaijua sura yake halisi. Lakini hilo halikuwahi kumtisha wala kumkatisha tamaa. “Nimekumbuka.” Aliwaza baada ya kufika kwenye maegesho ya magari, akalifuata gari lake.
Saa moja baadae alikuwa anapiga honi nje ya geti la nyumba yake, maeneo ya Mwananyamala, Kinondoni. Geti likafunguliwa na akaingiza gari, akaigesha mahali panapositahili na kulizima, akachukua mkoba wake na kutoka nao nje ya gari, mke wake akampokea. “Mbona kama unaharaka sana, kulikoni?” Aliulizwa. “Shajara yangu iko wapi?” Badala ya kujibu, akamuuliza mke wake huku tayari akiwa ameshaingia ndani, bila kujali sebuleni alikuwepo binti yake mdogo, akapitiliza chumbani akiwa hajahangaika kujibu salamu ya mwanae mwenye umri wa miaka mitano. “Baba Emilia, hata salamu ya mtoto unashindwa kupokea kweli?” Mke wake alilamika akiwa nyuma yake. “Sikumsikia, nisamehe.” Alijibu huku tayari mkono wake ukiwa juu ya kabati la nguo, sehemu aliyokuwa akihifadhi baadhi ya nyaraka zake. “Uliwahi kuichukua?” Alimuuliza mke wake aliyekuwa akimtazama kwa macho makali, hakuwa amependezwa na alichokuwa amekifanya mume wake, kuwapita bila salama ikiwa walikuwa hawajaonana kwa zaidi ya saa nane. “Mimi na wewe tuliwahi kutumia shajara moja?” Mke wake alimuuliza kwa kisirani. Majura alikaa kimya, mikono ikiwa bize kupangua hiki na kile hadi alipopata alichokitaka. “Lakini macho yangu na yako yanaona hiki chumba na vilivyomo.” Majura alimjibu huku akikaa kitandani na kuanza kupekua kurasa moja baada ya nyingine, akaufikia ukurasa aliyoutaka. “Mara zote namba za watu huwa unaweka kwenye simu yako, hizo ulizotunza kwenye shajara zinaziada gani?” Mke wake alimuuliza huku akikaa kando yake, macho yakiwa kwenye zile namba. “Hawa watu nilikutana nao nje ya ofisi, walitoka ofisini kumtafuta mwandishi anaeandika ukurusa wa moto, bahati mbaya ofisini hata iwe kwa ngumi, kamwe hawawezi kunikutanisha na watu bila mimi kuwa na taarifa zao. Wakakataliwa, lakini ni wakati nilipokuwa nikikkaribia geti la kuingia ofisini ndipo masikio yangu yakasikia malalamiko yao, nikawafuata.” Majura alimweleza mke wake. “Simu yako ilikuwa wapi wakati huo?”Mke wake alimuuliza. “Ilikuwa kwenye gari, lakini mkononi nilikuwa na hii shajara na nikazinakili namba zao.” Alijibu huku akiweka simu sikioni, simu ikaanza kuita upande wa pili. Iliita kwa muda mrefu hadi ilipokata, akapiga tena lakini ikabaki kuwa vile vile, simu haikupokelewa. Akaachana nayo, akanakili namba zingine na kupiga, simu haikuita mara mbili, ikapokelewa. “Naitwa Kassimu kutoka gazeti la Tulizo, nazungumza na Adela?” Majura alidanganya jina lake kwa aliyempigia. “Nipo msibani Tegeta.” Upande wa pili ulijibu kwa sauti ya chini sana. “Pole sana. Unakumbuka uliniachia namba za simu nje ya geti la kuingilia ofisi za Tulizo?” Aliuliza. “Nakumbuka ndugu yangu lakini tangia siku hiyo naishi kwa mashaka makubwa, yule mwenzangu niliyekuwa nae alifariki jana kwa kugongwa na pikipiki, alikuwa anatoka kituo fulani cha radio.” Upande wa pili ulijibu. “Alikuwa mtangazaji au?” Majura aliuliza. “Alitoka kwenye lilelile swala tulilokueleza, kiufupi ni hali mbaya mbele yangu, hata sielewi nifanye nini.” Adela alilamika kwa sauti yenye kuashiria uoga, alihofu juu ya maisha yake. “Naomba kuzungumza na wewe vitu vichache sana.” Majura alimwambia. “Siyo wakati huu, naomba uje nyumbani kwangu majira ya saa moja jioni, nitakuwa nimetoka huku msibani.” Adela alimwambia huku akimpa anuani ya makazi yake. “Sawa.” Majura alijibu huku akiondoa simu sikioni na kuikata, akageuza shingo na kumtazama mkewe ambae alikuwa makini kufuatilia mazungumzo yake. “Umeridhika?” Majura alimuuliza mkewe. “Kwani hamwezi kufanyia mazungumzo yenu sehemu nyingine tofauti na nyumbani kwake?” Mkewe alimuuliza kwa sauti kavu yenye viashiria vya wivu. “Hii ni habari na habari hutafutwa.” Majura alimjibu. Ukimya mfupi ukafuatia wakati Majura akipitisha macho kwenye kurasa za shajara yake. “Kitu gani mlizungumza?” Mkewe aliuliza. “Lini, leo au siku niliyopata hizi namba?” Majura nae akamuuliza. “Leo nimesikia kwa maana simu yako inasauti kubwa, namaanisha hiyo siku.” Mkewe alimjibu. “Wanadai wamepotelewa na watoto wao wa kiume.” Majura alimwambia. “Sasa watu kupotea si waende vituo vya polisi? Kwa nini wahangaike na magazeti, ni vema ukawashauri watoe tangazo la kupotelewa kama shida yao ni habari yao kuwa kwenye gazeti.” Maimuna Tabuse, mke wa Majura Katarama, alimshauri mume wake huku akimalizia kwa kugonganisha mikono yake, tabasamu la mshangao likiupamba uso wake. “Haiko hivyo mke wangu.” Majura alisema huku akiacha alichokuwa a anakifanya na kumtazama mkewe. “Kupotea kwa hao vijana kuna mazingira ya kutatanisha, walijiunga na mafunzo ya kujitolea huko jeshini, lakini wote Kwa nyakati tofauti waliwahi kumrejeshwa kwa kesi za utovu wa nidhamu.”Alimeza mate kulainisha koo, akaendelea huku mke wake akiwa makini kumsikiliza. “Baadae walipokea barua kwa wakufunzi wao zikiwa na maelezo ya kutakiwa kurejea kambini mara moja, jeshini ni amri na wao walitii. Lakini tangu walivyoondoka hawajawahi kurejea tena na huu ni mwaka wa pili, hakuna mawasiliano wala taarifa zao. Familia ziliingiwa na wasiwasi, wakaenda kuulizia kwenye kambi ya mafunzo huko Rufiji, lakini wanadai hawakuwa peke yao, watu wengine zaidi walikutana nao na wote walikuwa na kesi ya aina moja, wote walipewa jibu moja kwamba, vijana wao waliondolewa mafunzoni kwa sababu ya utovu wa nidhamu na haijawahi kutokea wakarejeshwa kambini kwa barua kutoka kwa mkufunzi, barua hutoka uongozi wa juu na hutolewa tangazo la pamoja na si kupewa mtu mmoja mmoja.” Majura alitua maelezo yake. Ukapita ukimya mfupi, Maimuna akiwa anamtazama mumewe, hatimae alipata la kusema. “Kwa hiyo wao wanahisi walipotelea jeshini?” “Sikuwahoji sana siku ile, nataka nianze leo ili nijue walipokuwa wamefikia na juhudi zao za kuwatafuta, ijapokuwa mmoja ameshafariki lakini aliyesalia ataniongoza kwa namna anavyojua, nikiona uzito na jinai iliyojificha, itanilazimu kuchimba zaidi.” Majura alisema. “Sawa, kazi njema.” Maimuna alimtakia kheri. “Lakini mbona kiunyonge?” Majura aliuliza. “Sipendezwi na kazi yako kwa sababu mara nyingi nahisi unakabiliwa na hatari, wakati huu pia unataka kuanza kufuatilia jambo ambalo naona kabisa litakuwa zito kuliko uwezo wako. Unaweza kupambana na hawa watu wengine lakini siri za taasisi kama jeshi, siyo siri rahisi kuzibeba.” Maimuna alimwambia. “Yote kheri mke wangu, Mungu humuumba kila mwanadamu kwa namna yake, inawezekana niliumbwa kwa namna hii. Huwezi amini, hapa nilipo nahisi saa zinakawia kunikutanisha na watu wawili ambao nahisi taarifa zao zitanifaa, kibaya zaidi wote wameomba nionane nao usiku.” Majura alisema huku akimshika mkono mke wake, akapapasa taratibu huku akimtazama usoni. Maimuna akaachia tabasamu hafifu huku akikwepesha macho yake yasiendelee kutazamana na ya mumewe, aibu zenye upendo ndani yake zikamshika, faraja ya tulizo la macho ya Majura ilimwingia, akajilegeza na kudondokea kifuani kwa mume wake. “Anza kufikiria kuachana na hii kazi, tuwekeze sehemu nyingine na si kutegemea uandishi wa habari.” Maimuna alisema huku akiinua kichwa chake na kuyatupa macho usoni mwa Majura. “Ipo siku nitafanya hivyo.” Majura alitoa jibu ambalo hulitoa mara kwa mara kwa mkewe, lakini kiukweli ndani ya nafsi yake hakuwa tayari kuachana na kazi aliyoipenda kuliko kazi yoyote hapa Duniani, aliamini alizaliwa kuwa mwandishi wa habari za kiuchunguzi. Akiwa bado anazichezea nywele za mke wake, simu yake ikapokea ujumbe mfupi. Akaachana na zoezi alilokuwa analifanya, mkono mmoja ukaishika simu yake na kuondoa nywila, akaingia kikashani na kukutana na ujumbe kutoka kwa Sukununu. Halikuwa jina halisi la mtu huyo, mara nyingi kitabu cha kumbukumbu za namba kilijaa majina ya uficho hasa kwa watu waliokuwa wakimpa taarifa alizohitaji kwa uficho, na alijitahidi kumwelewa kila mtu aliyetunza namba yake kwa jina alilochagua yeye. ‘Futa namba yangu kwenye simu yako, tukutane Mlimani.’ Ujumbe ulisomeka hivyo, akarudia zaidi ya mara mbili na hatimae akapata jibu moja kuhusu Sukununu, kuna kitu kilikuwa kinaendelea kwake. Kwa nini? Kwa sababu awali walipanga wakutane kwenye mgahawa wa jeshi, lakini kabla hajafika mgahawani akakutana na ujumbe uliomtaka waonane usiku nyumbani kwa Sukununu, kabla wakati wa miadi haujatimia, anapokea ujumbe unaomwelekeza wakutane kwenye maduka ya Mlimani City. “Hajawahi kuwa mjanjamjanja namna hii.” Aliwaza huku akijaribu kuinuka, alishasahau mke wake alikuwa amemwegemea. “Taratibu basi!” Maimuna alilalamika huku akijitoa mwilini mwa Majura, mdomo akiwa kautupa juu na kifua kikipanda na kushuka kwa ghadhabu, alinuna. “Narejea hivi punde!” Majura alisema huku akiiweka simu mfukoni mwake. “Unarudi? Mh! Sasa hivi ni saa kumi kasoro, na usiku unaenda wapi sijui.” Maimuna alipingana na ahadi ambayo alijua haiwezi kutimizwa, aliongea kwa kisirani huku akipiga hatua kuelekea sebuleni, nyuma akimwacha Majura akikodoa macho, alijua mke wake alichukia lakini hakuwa na namna, alihitaji kupata taarifa za Sukununu kwa udi na uvumba. Alitoka hadi sebuleni bila kumsemesha mke wake, akamwaga mwanae ambae alikuwa akitazama katuni luningani. Kwa namna alovypokea ujumbe alijua Sukununu alihitaji kuonana nae kwa haraka, aliacha gari lake kwa kuwa alijua anaweza kukwama kwenye foleni, akaita pikipiki ya abiria na kuomba kupelekwa haraka Mlimani City, eneo maarufu ndani na nje ya jiji la Dar es laam. Safari ilipoanza alijipa muda wa kuitafakari tabia mpya iliyoanzishwa na Sukununu, tabia ya kumtumia jumbe zenye utata na kutaka waonane saa tofauti tofauti. “Alitakiwa kuwa kazini muda huu.” Aliwaza huku akiinua mkono wenye saa, akasoma majira na kukubaliana na mawazo yake. Hakushangaa kwa kuwa kazi aliyokuwa akiifanya iliwezekana mtu kubadilishiwa ratiba wakati wowote, au pengine mhusika alikuwa na tatizo na akaomba kuwa nje ya kituo cha kazi. Sukununu kama alivyokuwa akimuita, alikuwa ni mwanajeshi wa jeshi la umoja, alikuwa ni koplo usu kwa cheo chake. Majukumu yake ya kazi yalikuwa kwenye hospitali ya jeshi, akiwa mwangalizi mkuu wa mochwari. Kila kilichofanyika hapo lazima ripoti ifike mezani kwake, maiti ziliingizwa ama kutolewa ni lazima asaini hati ya uthibitisho. Sukununu na Majura walikutana wakati wa sekeseke la utata wa kifo cha mmoja wa wanasiasa machachari kupata kutokea nchini Tanzania, mwanasiasa ambae alitazamiwa makubwa siku za usoni, lakini nyota yake ilizimwa akiwa katikati ya mapambano na mapapa wa dawa za kulevya. Mwanasiasa huyo alisema alikuwa na orodha ya majina ya wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa waliokuwa wakijihusisha na uuzaji na usambazaji dawa za kulevya, jambo hilo lilimuibua hadi rais wa nchi ambae aliitaka orodha hiyo mezani kwake, ili afuatilie ukweli wake kupitia vyombo vya ulinzi na usalama, rais hakutaka orodha hiyo iende bungeni kama mwanasiasa huyo alivyokuwa ameahidi kuweka wazi majina ya watu hao kupitia Bunge, ili kila Mtanzania ajue. Wakati orodha hiyo ikiwa mikononi mwa rais, mwanasiasa huyo akainuka na nia ya kutaka kugombea uenyekiti wa vijana wa chama tawala, ukaibuka mzozo mkubwa kati yake na Katibu mwenezi wa chama. Hapo ndipo anguko la mwanasiasa huyo lilipoanzia, kashifa mbalimbali zikaibuliwa na magazeti mengi yakitumika kuanika kashifa hizo, kashifa kubwa zaidi ni ile ya kujihusisha kimapenzi na mwanasiasa kijana kutoka chama cha upinzani, kashifa hiyo ikapelekea kupewa taraka aliyekuwa mume wa mwanasiasa huyo. Siku chache baada ya taraka, aliugua ugonjwa usiojulikana huku magazeti yakijitahidi kuandika mengi ya kusadikika kuhusu kupotea na kuugua kwa mwanadada huyo ambae mbali na umachachari wake kisiasa, lakini alikuwa na haiba ya kupendeza kwa watu. Watu wakiwa bado wanajiuliza kuhusu maswahibu yake ya ghafla, nchi ikashitushwa na taarifa za kifo chake, miongoni mwa walioshitushwa na taarifa hizo ni Majura Katarama, ambae wakati huo alikuwa akimiliki Tovuti, hiyo ni baada ya kukosa kazi kwenye vyombo mbalimbali vya habari. Tovuti yake haikuwa ikifahamika na wengi, licha ya kujitahidi kuandika makala nyingi zilizogusa maisha ya watu wakubwa serikalini, alikuwa akiandika makala zenye mlengo wa maswali kuhusu mali walizomiliki watu hao na chanzo cha mapato yao. Sakata la mwanasiasa huyo likamfanya akeshe siku nne mfululizo akihangaika kutafuta majibu ya maswali ya watu juu ya ukweli wa orodha ya wauza dawa za kulevya, mahusiano nje ya ndoa yake na hatimae kifo chake. Kila alichopata aliandika na kuweka kwenye ukuta wa tovuti yake, idadi ya watembeleaji wa ukuta wake ikazidi kuongezeka, nae akataka kuwapa kile walichohitaji, akataka kupata ukweli wa kile kilichooneka kwenye mwili wa mwanasiasa huyo ambae taarifa zilianza kuenezwa kwamba, kabla ya kifo chake alitekwa na watu wasiojulikana na alipopatikana akawa na ugonjwa wa ajabu ambao ndugu walishindwa kujua ni kifafa ama kitu gani. Hapo ndipo Majura alipompata tabibu mmoja wa jeshi ambae hata kabla ya kumpa taarifa nyeti, alikufa kifo cha ghafla akiwa kwenye gari nyumbani kwake. Majura hakukata tamaa, akamtafuta na kumpata mhudumu wa mochwari ambae alikuwa ni askari wa kawaida, aliyekuwa akisimamia waoshaji maiti na wakati mwingine aliosha yeye mwenyewe, akafanikiwa kumshawishi kupata taarifa alizohitaji kwa kuwa mwili wa mwanasiasa huyo ulihifadhiwa hapo na alikuwa ni mmoja wa waliohusika na kuuweka mwili wake kwenye jokofu. Bahati mbaya ni kwamba, kabla hajaziweka kwenye ukuta wa tovuti yake, tovuti yenyewe ikashushwa mtandaoni na haikupatikana kwenye wavuti yoyote. Alijaribu kila namna kuirejesha, lakini ilishindikana. Hakukata tamaa, taarifa zake akaenda kuziuza kwa mhariri wa gazeti la Tulizo, gazeti ambalo halikuwa na siku nyingi tangu kuanzishwa kwake. Mhariri akazipenda lakini hakutaka kuziweka gazetini, alichokifanya ni kumuunganisha na mkurugenzi ambae alitoa ruhusa kwa afisa mwajiri, kumpa kazi kama mwandishi wa gazeti na alipewa ukurasa maalumu kwenye kila toleo, ukurasa ambao ulikuwa maalumu kwa habari za kiuchunguzi ambazo hazitakuwa kwenye gazeti lolote tofauti na Tulizo. Taarifa yake ya kwanza ilihusu vifo tata vya watu zaidi ya ishirini, ambao walifia ndani ya kanisa la mchungaji Wangwe Ngutu. Wengi waliaminishwa waumini hao walikufa wakati wa mkanyagano wa kugombea kukanyaga mafuta ya upako, lakini baada ya Majura kufanya uchunguzi wake na kuhakiki kutoka vyanzo mbalimbali vya taarifa, ilibainika walikufa kwa kunywa maji yenye sumu yaliyokuwa yakiuzwa na mchungaji huyo.
Majura Katarama akalipaisha gazeti la Tulizo, huku akiweka ukaribu zaidi na Jumanne Fadhili ambae alimpachika jina la Sukununu. Miaka ilisonga wakiwa kwenye urafiki wao ambao waliufanya wa siri, Jumanne hakutaka urafiki wake uwe wa wazi kwa kuwa alikuwa akitoa taarifa fulani kinyume na kiapo chake cha kazi, lakini mara alizokuwa akitoa taarifa kwa Majura, taarifa zake zikageuka kuwa msaada kwa raia wa kawaida ambao hawakuwa wakijua utata wa baadhi ya vifo ama magonjwa ya watu maarufu waliowapenda, hasa wakosoaji wa serikali. Jummane akapandishwa daraja na akapewa majukumu mapya ya kusimamia huduma za mochwari na wahudumu wake, lakini urafiki wake na Majura haukufa na waliendelea kuwasiliana kwa siri bila mtu kujua ukaribu wao, lakini hayo yalikuwa ni mawazo yao. Hawakuwa sirini kama walivyojidanganya, ilisubiriwa wakati sahihi wa kuoneshwa hawakuwa wakiwasiliana kwa siri ama vinginevyo. Ilianza siku ya hafla ya kuagwa kwa mashujaa waliofia Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Majura akifuatiliwa kwa ukaribu sana kwa kuwa alishafahamika ni yeye aliyekuwa akiandika makala za kiuchunguzi kwenye gazeti la Tulizo, akazuiwa kupiga picha ya mnato ama jongevu. Lengo la wazuiaji ni kutega mazungumzo yake na ndugu yake Nyaswe, waliamini kama atapata nafasi ya kupiga picha, hatoweka muda wake kumfariji mdogo wake. Mtego ukamnasa bila yeye kujua, mazungumzo yake yote na ndugu yake yalinaswa kupitia vifanasa sauti vilivyowekwa kwenye viti walivyokuwa wamekalia waombolezaji, hata wakati anaagana na mdogo wake, hesabu za wategaji zilikuwa mbele yake, wakajua anaenda kuwasiliana na Jumanne Fadhili, haraka Jumanne p.a.k Sukununu akaondolewa kwenye majukumu yake aliyokuwa akiyapokea kutoka kwa msaidizi wake, akaelekezwa kurejea nyumbani. Wakati Sukununu akiwa hana hili wala lile kuhusu kuondolewa kwenye zamu, akapokea ujumbe mfupi kutoka kwenye namba asiyoifahamu, namba hiyo ilimpa ujumbe wenye maneno machache sana lakini yenye maana na uzito mkubwa. “Kimbia” Aliusoma ujumbe huo, lakini alishindwa kuulewa, akijiuliza maswali kadhaa pasipo kupata majibu, kwa nini akimbie? Kamkosea nani? Au mtumaji alikosea namba? Hakutaka kukihangaisha kichwa chake kwa maswali ingali angeliweza kuwasiliana na huyo aliyemwandikia ujumbe, akauliza. “Kwa nini?” Sekunde chache baadae akajibiwa, “wewe na Majura, kimbieni.” Naam, alielewa na wala hakutaka kujizungusha kujua sababu ya kuambiwa hivyo, alichowaza ni usalama wake na mwenzake, haraka akatuma ujumbe kwa Majura wa kusitisha miadi kwenye mgahawa wa jeshi, wakati huo aliamua kuondoka kambini kwa njia aliyoijua yeye, akiwa amechagua kumwamini mtu aliyemwandikia ujumbe. Kwa nini? Kwa sababu mtu huyo kujua mahusiano yake na Majura, pia kutuma ujumbe muda mfupi baada ya kuwasiliana na Majura. Kuna jambo! Hakutaka kupuuza hata kidogo Kwa sababu alijua ni nini adhabu za wavujisha taarifa nyeti ziwe za taasisi ama za raia wanaopata huduma kwenye taasisi ya ulinzi wa amani na mipaka ya nchi. Alijua anahesabiwa kama msaliti katikati ya vita, adhabu yake ni kifo. Ndiyo, Jumanne alijua alitakiwa kuuawa ama kufungwa kwa sheria za kijeshi, hilo la kufungwa halikuwa kipaumbele bali kifo kilikuwa ni kipaumbele zaidi Kwa kila msaliti. Lakini mbali na hilo kuna jambo kubwa zaidi lilikuwa likiendelea na alikuwa akipata tetesi zake, jambo ndani ya idara za jeshi. Fukuto lilikuwa linafukuta kwa wakuu wa idara mbalimbali ndani ya jeshi la umoja.
"KIMBIA"a akiongea na nani. “Siku rahisi ilikuwa ni jana, leo ni siku ya mchezo na mchezo huu unasheria zake, usiucheze kama huzijui sheria hizo.” Mtu yule aliongea kwa sauti ya chini lakini ilisikika vema masikioni mwa Nyaswe, akageuka kumtazama aliyekuwa akiongea, lakini kasi ya kugeuza shingo yake ilikuwa nyuma ya kasi ya matendo ya mtu yule, ambae aliongea na kuinuka mara moja huku akiacha mgongo wake ukiwa mali ya macho ya Nyaswe, lakini sura haikuonekana na hilo ndilo lilikuwa lengo lake, hakutaka Nyaswe amuone lakini alitaka ujumbe ufike. Naam, ujumbe ulifika kama ulivyokusudiwa lakini mpokeaji alibaki kwenye kiwewe na asijue alitakiwa kufanya nini, maneno hayo haikuwa mara ya kwanza kukutana nayo, tofauti pekee ni kwamba, mara ya kwanza aliyasoma na mara ya pili aliyasikia kwa masikio yake. Mwili wake ulitetemeka, ngozi yake ikajikunja kwa baridi ya ghafla ambayo hakujua ilitokea upande gani katikati ya jua la utosi, yale machozi yaliyokuwa na juhudi za kulowesha mashavu yake, yalikatika na hayakumtoka tena, macho yalibaki na ukavu kama vile hayakuwahi kutiririsha mifereji ya majichumvi. “Majura!” Aliwaza huku akichukua simu yake aliyokuwa ameihifadhi kwenye titi la kushoto na kuibana vizuri na sidiria, akaingia sehemu ya kutuma ujumbe mfupi, akaandika maneno machache na kutuma, wakati huohuo tumbo lake liliunguruma mithili ya mgonjwa wa kuendesha. Hofu ilikuwa ni kubwa kuliko ujasiri. Hata mtoto wake aliyekuwa tumboni na juhudi za kupiga mateke, alitulia tuli, aliuhisi unyonge wa mama yake.

AmeyakanyagaLakini mbali na hilo kuna jambo kubwa zaidi lilikuwa likiendelea na alikuwa akipata tetesi zake, jambo ndani ya idara za jeshi. Fukuto lilikuwa linafukuta kwa wakuu wa idara mbalimbali ndani ya jeshi la umoja. Lilihusu nini? Hakujua!
Majura alimlipa dereva wa pikipiki na kuagana nae, akaingia viwanja vya Mlimani City na kuelekea ndani ya jengo upande wa maduka ya vitu mbalimbali, kama alivyoelekezwa. Alipiga hatua zake kwa uharaka huku akiwa makini kumzingatia kila aliyekuwa akipishana nae, alitarajia kumuona Sukununu akiwa miongoni mwa watu waliokuwa wakichagua hiki na kile, ama waliokuwa wakipishana kutoka duka moja hadi lingine. Alitembea kama mtalii, alikuwa akihamisha macho yake kutoka duka moja hadi lingine, lakini hadi anamaliza safu kwanza ya maduka hakuwa ameiona sura ya Sukununu. “Yuko wapi?” Alijiuliza huku akiinua mkono wake na kutazama saa yake, alikuwa ndani ya muda, hakuwa amechelewa. Aligeuza baada ya kumaliza safu ya kwanza ya maduka ya simu, akaanza kuelekea kwenye safu nyingine ya maduka ya vito vya thamani, alitembea taratibu huku macho yake yakiwa makini zaidi ya mwanzo, alimkagua huyu na kumkagua yule lakini hakuwa ameiona sura aliyoitarajia. “Hawezi kuwa ananitania, atakuwa hapahapa mlimani.” Aliwaza huku akiendelea kupiga hatua zake taratibu kama mtu aliyekuwa amezidiwa na kichomi mbavuni mwake, hakujali watu waliokuwa nyuma yake walioona anawachelewesha kusonga mbele, aliacha wampishe na kuendelea na haraka zao, lakini yeye hakuwa mteja wa duka lolote. Akiwa bado anahangaisha shingo yake huku na huko, akapigwa kikumbo kizito na mtu aliyekuwa nyuma yake, akapepesuka nusura ya kuanguka, alipoupata mhimili wake akageuka haraka akiwa ni mwenye jaziba, akagonganisha macho na mtu aliyekuwa amevaa barakoa nyeusi, kofia nyeusi na alivaa sweta. Alikuwa ni mrefu wa wastani, macho makali yakimtazama Majura. Mtu yule alinyoosha mkono kabla Majura hajasema lolote, mkono wake ukapokelewa kisha akaondoka bila kuongeza neno lolote. Baada ya kubaki na alichopokea kutoka mkononi mwa mtu yule ambae alimtambua kwa kimo na macho yake, alikunjua kipande cha karatasi na akakutana na mwandiko wa mtu aliyeandika akiwa na haraka, ulikuwa mwandiko uliotapanyika lakini alielewa kilichoandikwa, haraka akatupia mdomoni kile kipande cha karatasi baada ya kusoma, tumbo likaunguruma si kwa sababu ya njaa au ugonjwa, bali kwa hofu iliyomwingia ghafla baada ya kuelewa kilichoandikwa na Sukununu, haraka akachukua uelekeo wa kutoka nje ya jengo, shingo yake ikizunguka huku na huko kuhakikisha yupo peke yake kwenye kila hatua aliyokuwa akiipiga. Dakika mbili baadae alikuwa sehemu ya kuegesha magari, akaangaza huku na huko hadi alipoiona gari nyeusi aina ya Toyota Harrier, akaifuata. “Anaekufuata ametuona?” Majura aliuliza mara baada ya kuingia ndani ya gari. “Sina hakika lakini kuna mtu yupo nyuma yangu tangu nilipotoka kambini, kuna kitu hakipo sawa.” Sukununu alisema kwa sauti ndogo huku akielekeza macho yake upande wake wa kushoto, alimuona jamaa mmoja mrefu akiwa amefunika kichwa chake kwa kofia pana, lakini sura yake ilionekana. “Huyo hapo, anatutafuta.” Sukununu alimwambia Majura. “Kilichotuna kwenye mkanda ni bastola?” Majura aliuliza huku akitetemeka. “Ndiyo maana yake.” Sukununu alijibu. “Kwa nini?” Majura alimuuliza huku akitoa simu yake mfukoni. “Unataka kufanya nini?” Jumanne Fadhili, p.a.k Sukununu, alimuuliza huku akitaka kufanya jitihada za kumzuia asifanye alichokusudia. “Hawa watu lazima uwafahamu kabla hawajakudhuru.” Majura alisema huku akifanikiwa kupiga picha mnato, alimpiga mtu ambae walihisi alikuwa akihangaika kuwatafuta, alikuwa akihangaika kuangaza huku na huko kwa umakini, bahati nzuri kwao, walikuwa kwenye gari yenye vioo vyeusi kiasi cha kuzuia mtu aliyenje kumuona aliyekuwa ndani. “Nimemkimbia kwa muda mrefu sana na hayuko peke yake.” Sukununu alisema. “Kwa nini?” Majura aliuliza. “Kwa sababu nawasiliana na wewe.” Sukununu alijibu. “Wamejuaje?” Majura alihoji huku akishangaa. “Sijui kwa kweli lakini kabla sijaonana na wewe leo, nilitumiwa ujumbe na hii namba.” Sukununu alisema huku akimwonesja ujumbe aliotumiwa. “Mungu wangu!” Majura alisema huku mapigo ya moyo wake yakienda mbio, aliukumbuka ujumbe wa mdogo wake, alikumbuka kuonywa kuhusu kufuatilia chochote kuhusu mwili wa mume wa Nyaswe. “Sijasikia ulichokuwa unanitafutia.” Sukununu alihamisha mjadala, ili kurejea kwenye kile kilichokuwa kinawangaisha kukutana. “Luteni Jangala Maduhu unafahamu?” Majura aliuliza. “Huyu aliyekuwa akihudumu kambi ya wakimbizi kabla ya kupelekwa nchini Kongo?” Sukununu aliuliza ili kupata uhakika wa Jangala aliyekuwa akizungumziwa. “Ni huyohuyo.” Majura alijibu. “Si amefia vitani?” Sukununu alihoji. “Hapo ndipo ilipohoja yangu.” Majura alinyamaza huku akitupa macho alikokuwa akielekea mtu waliyehisi anawatafuta wao. “Mke wake amezuia kuiona maiti yake, hakupewa nafasi ya kuhakiki mwili wake. Mimi pia nimezuiwa kupiga picha tukio lolote kwenye hafla ya kuaga miili ya mashujaa.” Majura alitua. “Unaundugu na Jangala?” Sukununu aliuliza. “Ni shemeji yangu, mume wa mdogo wangu tumbo moja.” Majura alijibu. “Shujaa yeyote anaefariki na kuletwa pale hospitali, mwili wake hauguswi na mtu zaidi ya mimi na kijana mmoja au wawili kwa usaidizi wa hapa na pale. Kila kitu kinakuwa chini ya jeshi, ndugu wanapewa nafasi ya kuaga na kuthibitisha mtu wao. Miili hiyo hadi inafika huku, tayari ilishafanyiwa taratibu zote za maandalizi na hospital miili yao ililetwa kuhifadhiwa, kwa kumbukumbu zangu sikuona mwili wa mtu ninaemfahamu, hao mashujaa wengine walikuwa ni wageni kwangu kwa sababu walitolewa kambi tofauti na hapa makao makuu. Aliyetoka makao makuu ni Luteni Jangala Maduhu pekee na sikumbuki kama niliuona mwili wake, lakini jina lake lilikuwa miongoni mwa watu walioingizwa mochwari.” Sukununu aliongea kwa kirefu. “Uliuona mwili wa mtu mnene, mfupi?” Majura alihoji. “Ndiyo.” Sukununu alijibu. Ukapita ukimya wa sekunde kadhaa. “Kuna kitu gani kinaendelea hapo makao makuu?” Majura aliuliza. “Siwezi kukwambia kuhusu lolote linalohusu jeshi moja kwa moja.”Sukununu alinyamaza kidogo, kisha akaendelea. “Nakuomba tuache kuwasiliana kwa muda hadi nitakapokutafuta. Acha nipambanie uhuru wangu kwanza. Nataka niwajue hawa wanaonifuata na silaha ni kina nani na wanataka nini, pia nimfahamu aliyemwandikia ujumbe ni nani na kwa nini aliamua kunambia nikimbie!” Alitua. “Kwa nini usifuate ushauri wake?” Majura alimuuliza. “Lakini hakusema nikimbie peke yangu, na wewe. Je, utakimbia?” Sukununu aliacha swali kwa Majura, ambae alikaa kimya, alishindwa kujibu. “Kama hujawahi kuacha kuandika habari ngumu zinazoogopwa na wanahabari wenye roho nyepesi, basi siwezi kuwa mkimbizi kwenye nchi yangu. Wahuni wachache hawawezi kunikimbiza kama kuku, wacha nife, pengine ni wakati wa Mungu.” Koplo Jumanne Fadhili, aliongea kwa ujasiri, macho yake yakimtazama mtu aliyekuwa akizunguka huku na huko, akimtafuta. “Kuwa makini sana na hilo jambo ambalo pengine wewe unalijua kiundani kuliko mimi. Kutafutana silaha ni moja ya jambo la kuogofya.” Majura alisema. “Usisahau mimi ni msaliti, nimekuwa nikikupa siri zote unazohitaji kuhusu miili ya watu wanaoletwa hospitali ya jeshi. Hiyo pekee inaweza kusababisha mimi kufungwa au kuadhibiwa vinginevyo.” Jumanne alisema. “Lakini si kuwindwa namna hii, lipo jambo na hutaki kulisema.” Majura alimwambia huku akiwa na shauku ya kutaka kujua kilichokuwa kikiendelea, mbali na taarifa alizokuwa akipewa. Aliamini kama walishagundulika wanapeana taarifa, aliyevujisha alitakiwa kuadhibiwa kwa namna nyingine na si kuwindwa kama swala, ikiwa uwezo wa kumuita ofisini na kumkamata kwa namna yoyote ulikuwepo. “Tutazungumza nafasi ikipatikana, hapa tupo nusu shari nusu kheri.” Jumanne alimwambia huku akiruhusu kabali za mlango wa upande aliokaa Majura, ziiachie. “Lakini hapa tulipofikia kesho yetu ni leo iliyosalama.” Majura alisema huku akianza kuusukuma mlango. “Usijali, haitakuwa mbali sana kabla hatujaoanana tena na kusimuliana. Tunaweza kuhukumu kumbe ni wahuni wengine, wenye malengo mengine.” Jumanne alisema. “Hao jamaa unawafahamu?” Majura aliuliza akiwa ameweka mguu mmoja chini, alijiandaa kushuka kwenye gari. “Sijawahi kuwaona ijapokuwa wajihi wao unatosha kunitambulisha, ni watu wa kazi.” Jumanne alijibu huku akiwasha gari, Majura akashuka na kuubamiza mlango, akatazama huku na huko asimwone yule mtu aliyeambiwa na Sukununu alikuwa akimtafuta, akapiga hatua za haraka na kuondoka kwenye maegesho, moja kwa moja akaanza kuondoka huku nusu akikimbia na nusu akitembea, sekunde chache baadae gari ya Jummane Fadhili, p.a.k Sukununu, ilimpita kwa kasi kubwa.
Muda wa miadi ya usiku baina ya Majura na mwanamke aliyepotelewa na mtoto wake, ulikuwa haujafika na wala hakutaka kuharakisha ufike. Alipotoka viwanja vya Mlimani City moja kwa moja akaamua kuelekea zilipokuwa ofisi za gazeti la Tulizo, gazeti ambalo alikuwa akilifanyia kazi. Kwa kutumia usafiri wa pikipiki alifika ndani ya muda aliokuwa akiuhitaji, akiwa na lengo la kumwahi mhariri mkuu kabla hajarujusu kuchapwa kwa gazeti ambalo lilikuwa likitoka siku iliyofuata. Aliwasabahi wenzake aliowakuta chumba cha habari wakiendelea na shughuli zao, akaingia ofisi ya mhariri mkuu wa gazeti lakini alikuta ofisi tupu, hakujali, alitoka na kurejea chumba cha habari, akaenda kwenye meza yake ambayo hufanyia kazi zake. Akawasha ngamizi, akavuta kiti na kukaa wakati akisubiri mfumo wa ngamizi umruhusu kuendelea na alichokuwa akitaka kufanya. Mara nyingi ushindi wake kwa adui zake ni kuwahi kutoa taarifa fupi kwenye gazeti, aliamini hata siku hiyo alitakiwa kufanya hivyo ili kupunguza kasi ya watu waliokuwa nyuma yake ama nyuma ya rafiki yake, Jumanne Fadhili aliyependa kumtambua kwa jina alilompachika, Sukununu. Viashiria vya hatari vilishajitokeza, hivyo alitaka kuwa mbele ya muda kwa kutoa taarifa ya kidogo alichokuwa anakijua, huku akitaka pia atumie habari hiyo kuzindua watu wengine ambao alishasikia walipotelewa na vijana wao wakiwa kwenye mafunzo ya kujitolea, kwenye kambi mbali mbali za jeshi la akiba na baadhi ya kambi za jeshi la umoja. Baada ya ngamizi mfumo wa ngamizi kuwa tayari kwa matumizi, ilimhitaji kuweka nywila ili kuendelea, akaweka nywila alizotumia wakati wote, lakini aliletewa ujumbe wa kukosea nywila. “Mbona hakuna nyingine tofauti na hii?” Alijiuliza huku akiweka tena nywila zilezile alizotumia kila siku, lakini mambo yalibaki kuwa vilevile, ngamizi ilimkatalia. Akainuka, akamfuata mtu aliyekuwa kando yake, akamuuliza kwa sauti ndogo ambayo wengine hawakusikia. “Kuna mabadiliko yoyote yamefanyika kwenye hizi ngamizi?” “Hapana! Hakuna mabadiliko kwa siku ya leo, yangelikuwepo basi tungelipewa taarifa. Kulikoni?” Aliyeulizwa alijibu na kumalizia kwa swali. “Aah, hapana. Nadhani nimeghafirika kidogo.” Alisema huku akirejea kwenye meza yake, akaweka tena nywila alizozifahamu kwa tarakimu moja baada ya nyingine, silabi na ilabu moja moja hadi alichokusudia kilipokamilika, akaruhusu. “Haiwezekani!” Alisema huku akishuhudia akikataliwa, nywila alizoweka hazikutambuliwa na mfumo wa ngamizi aliyokuwa akiitumia kila mara, akainuka haraka na kuondoka chumba cha habari, akaelekea ofisi ya mkurugenzi. Baada ya kuingia alikuta watu wawili wakiwa wamekaa, walikuwa kwenye mazungumzo; mhariri mkuu na mkurugenzi mtendaji. “Leo unaingia ofisini bila taarifa?” Mkurugenzi alimuuliza. “Sijamkuta katibu wako.” Alijibu huku akiyatupa macho kwa mhariri ambae alikuwa kimya. “Kuna tatizo, naona upo macho juu tofauti na nilivyokuzoea.” Mkurugenzi alimwambia. “Nashindwa kuelewa kinachoendelea endelea kwenye ngamizi yangu, mfumo hautambui nywila zangu.” Alisema, lakini aliishia kumuona mkurugenzi akitazamana na mhariri mkuu. “ooh nadhani taarifa ilichelewa kukufikia, kulikuwa na maboresho kidogo ya mfumo wa ngamizi zote hapa ofisini.” Mkurugenzi alimjibu kwa sauti ya jeuri tofauti na kawaida. “Lakini wengine wanaendelea na shughuli zao, kwa nini ngamizi yangu pekee?” Aliuliza huku akimtazama mhariri aliyekuwa amejiinamia, hakuwa na furaha usoni mwake kama ilivyokuwa siku zote, hakuwa mchangamfu na mwingi wa maneno kama alivyozoeleka. “Hilo liache kwa mafundi, kesho ukija kila kitu kitakuwa sawa. Idara ya matengenezo italifanyia kazi.” Mkurugenzi alimjibu. “Bado nusu saa gazeti liingie kiwandani, nina habari muhimu sana ambayo ilipaswa kuonwa na mhariri kabla ya huo muda.” Majura alisema. Kwa mara nyingine, mkurugenzi na mhariri walitazamana, nyuso zao zilionesha kuna jambo lakini midomo yao ilichagua kulinyamazia. “Hadi muda huu tayari gazeti lipo kiwandani, nadhani taarifa yako ipandishwe keshokutwa, bado ile taarifa ya maji ya sumu kutoka mgodini, hadi kwenye vyanzo vya maji haijamalizika, nadhani tupo sehemu ya mwisho.” Mhariri mkuu alimjibu pasipo kujihangaisha kumtazama, alimjibu kwa sauti iliyopwaya. Majura alikaa kimya akiwatazama kwa zamu, wote wawili walishindwa kumtazama usoni. “Kuna nini?” Alijiuliza huku akiondoka bila kuaga, akatoka nje ya ofisi akiwa na uhakika kuna kitu kilikuwa kinaendelea pale ofisini na mkurugenzi hakutaka kumwambia. Kwa nini? Hakuna aliyempa jibu, lakini alichokuwa na uhakika nacho hadi wakati huo ni kwamba, alikuwa amepewa majibu ya kudanganywa na viongozi wake, hakukuwa na maboresho yoyote ya kimfumo yaliyofanyika kama ambavyo jirani yake alimwambia, aliamini taarifa ya jirani kuliko taarifa ya mkurugenzi wake. Kwa nini? Kwa sababu ni wiki moja ilipita tangu maboresho hayo tafanyike na maboresho yakifanyika, hakuna ngamizi yoyote inayosusia nywila ya mtumiaji pasipo kubadilishwa. Alibadilishiwa nywila, kwa nini? Na ni nani aliyembadilishia? Kwa sababu gani? Alijiuliza maswali mengi bila kupata majibu, akaamua kuondoka ofisini, muda nao ukizidi kuelekea magharibi.
Kunduchi, nyumba namba mia moja, Majura alisimama nje ya geti akiwa ameshika simu yake, baada ya majaribio kadhaa ya kumpigia mwenyeji wake kutofanikiwa, simu yake ilikuwa imepoteza uwezo wa kupiga wala haikuwa aikipokea, mtandao ulikuwa chini. Kitu kizuri kwake, nusu saa iliyopita alikuwa amefanya mawasiliano na mwenyeji wa nyumba ile, bahati mbaya daada ya kukaribia kuifikia, simu yake ikaangusha mtandao, hakujua sababu ila zaidi ya kuamini ni hitilafu za mitandao aliyokuwa akitumia. Kwa kuwa alikuwa na uhakika alikuwa hajakosea anuani, akaamua kugonga geti tofauti na makubaliano na mtu aliyetakiwa kuonana, mtu huyo alimwambia anatakiwa kupiga simu punde akishafika, na si kugonga geti ama kuita. Hakujua kwa nini alipewa masharti kiasi hicho, alikubaliana nayo, bahati mbaya kwake simu ikashindwa kutimiza jukumu lake la msingi. Aligonga geti mara tatu pasipo kusikia dalili za mtu kuitikia, akagonga tena mara ya nne na ya tano lakini majibu yalibaki kuwa vilevile, akakumbuka alivyosisitizwa kupiga simu akiwa nje ya geti, akaona si busara kuendelea kugonga ingali mhusika alishamwambia ni kitu gani alitakiwa kufanya, akapiga hatua na kuanza kuondoka taratibu huku akiitazama simu yake ilivyomsaliti, mtandao bado haukuwa imara kwa matumizi. Akiwa hatua kumi mbali na geti la nyumba namba mia moja, masikio yake yalisikia geti likifunguliwa, akageuka na kumuona mwanamke mfupi wa kimo, mwili mnene kiasi akiwa kwenye pajama. Alimkumbuka. “Nilikwambia upige simu.” Adela alisema kwa sauti ambayo haikutoka sawasawa, lakini ilisikika masikioni mwa Majura Katarama. “Kuna tatizo limejitokeza kwenye simu yangu, haipigi wala haitumi ujumbe mfupi.” Majura alisema. “Karibu.” Adela alisema huku akitazama huku na huko kwa wasiwasi, Majura akapiga hatua na kumfikia, akaingia kama alivyoombwa na mwenyeji wake. Nyumba nzuri ilikuwa mbele yake, gari la kisasa likiwa limeegeshwa kando. “Karibu ndani” Adela alisema huku akitembea kwa kasi kuuelekea mlango wa kuingia ndani, akafungua na kumkaribisha mgeni wake. Majura alipita bila kusema lolote, alikuwa kimya akimtazama mwanamke mzuri akiwa ndani ya vazi la kulalia, lenye kuuchora mwili wake kwa kiasi kikubwa. “Upo peke yako hapa nyumbani?” Majura aliuliza baada ya kuona mwenyeji wake akiwa hajali kuhusu vazi lake mbele yake, alitarajia kupokelewa lakini si kwa namna ile. Pajama halikuwa vazi la kupokea wageni nyakati za usiku, lakini hakushangaa sana, ndivyo mambo yalivyo kwenye jiji la Dar es laam, kila mtu hufanya jambo kwa namna yake. “Nipo peke yangu.” Adela alijibu kwa sauti ya kutetemeka mithili ya mtu aliyekuwa akipigwa na baridi la tumbo, macho ya Adela yalionekana kuwa mekundu, uso wake haukuwa na haiba ya furaha. “Pole kwa msiba wa..” Majura hakumalizia kauli yake, Adela akamtisha. “Rafiki yangu na mshirika mwenzangu wa biashara.” “Unahisi kuna lolote?” Majura aliuliza huku akiweka simu yake tayari kwa ajili ya kurekodi mazungumzo yake na mwenyeji wake. “Sijui.” Adela alijibu kifupi huku akiwa anatazama pembeni, Majura aligundua jambo, tangu aingie pale ndani Adela alikuwa hamtazami usoni na alikuwa hajiamini. Alihisi pengine kifo cha mwenzake kilimchanganya, lakini kwa nini asijiamini ikiwa anaweza kujiamini kuvaa pajama mbele yake!. “Tunaweza kuendelea na kilichotukutanisha hapa?” Majura aliuliza. “Najihisi siko sawa, tunaweza kuzungumza kesho?” Adela aliuliza huku akijitahidi kumtazama mgeni wake, machozi yakiwa yanaanza kutiririka. “Kuna nini? Mbona unalia?” Majura alimuuliza maswali mfululizo huku akishindwa kuelewa kilichokuwa kikiendelea kwa Adela. Adela aliyekuwa akiwasiliana nae kwenye simu alikuwa ni mkavu wa sauti, mwenye kujiamini na shauku ya kufanya mahojiano, lakini Adela aliyekuwa mbele yake alikuwa ni mwenye wasiwasi na mwenye huzuni ama majuto ya jambo fulani. “Ondoka hapa haraka!” Adela alisema kwa sauti ya chini huku akifuta machozi, aliinuka kwenye sofa na kukimbilia mlangoni, akafungua mlango haraka na kumgeukia Majura. “Ondoka haraka!” Adela alisema. Haikuwa sauti ya ukali bali yenye kuashiria hatari. Majura hakutaka kujiuliza sana, alishahisi mambo si mambo tena na pengine kulikuwa na jambo nyuma ya wasiwasi wa mwenyeji wake, akainyakua simu yake iliyokuwa juu ya meza na kuiweka mfukoni, akakimbilia mlangoni lakini haikuwa kama alivyotaka iwe, kundi la watu zaidi ya sita lilikuwa mbele ya mlango; mmoja alikuwa na kamera, wengine walitulia wakimtazama. “Wewe ndiye unamsumbua mke wangu?” Mmoja alichomoka katikati ya wenzake na kusimama karibu yake, alikuwa mtu mzima wa kukadiria miaka kumi hamsini na ushee. Majura aligeuka kumtazama Adela aliyekuwa bado ameganda katikati ya mlango na pajama lake, machozi yakiwa dimbwi dibwi usoni mwake. “Hapan..” Majura kabla hajamaliza alichotaka kusema, konde moja likatua kwenye papi za midomo yake na kumpasua vibaya; halikuwa konde moja pekee, yalifuata makonde mengine mfululizo huku lugha kali ikitoka mdomoni mwa mume wa Adela. “Yani huna haya, unakuja kwangu usiku na mnatoka mkiwa hivi! Mke wangu kwenye vazi hili inaashiria mmetoka kuzini!” Mzee alifoka kwa ukali huku akiendelea kuvurumusha makonde kadri alivyoweza, wakati huohuo jamaa mwenye kamera alianza kupiga picha mnato kwa namna alivyoona inafaa. Wengine walisimama kando wakishuhudia kilichokuwa kikiendelea. “Msinipige picha!” Majura alifoka kwa hasira, alihisi kuonewa. “Ongea na mimi mwanaharamu mkubwa wewe.” Mzee alimfokea. “Sijazini na mkeo!” Majura alisema huku akifanya jitihada za kumdhibiti yule mzee, likawa kosa. Wale jamaa waliokuwa wamejigeuza mashuhuda, wakaingilia na kuanza kumshushia kipigo bila huruma, walijua kupiga na walijua wanapigaje, hawakuwa wapigaji wa kawaida kama alivyokuwa mume wa Adela. Katikati ya kipigo, mmoja akawahi kuufyatua mkanda ulioshika suruali ya Majura, ikaenda chini.
Nipo hapa mkuu, nakusoma vizuri.NB; riwaya hii haitauzwa popote, itawekwa hapa kwa kadri ya kudra za Mungu.
Wale wanaopenda kulalamika alosto na lugha nyingine dhaifu, niwakumbushe mapema, pengine Uzi huu hautawafaa kwa sababu, utaenda kwa kadri ya kupatikana muda wangu binafsi. Mnaotunga kuibiwa na kutapeliwa, niwaombe, acheni Uzi huu uende bila propoganda hizo. Sote tunaopenda kufurahi, kuburudika hivyo, maoni ya wahifidhina wachache yasisitishe burudani ya wengine.
Uzi huu unawafaa zaidi wale ambao ni wasomaji halisi na wapenda riwaya wa kweli.
Ukimaliza kusoma weka alama nijue nasomwa, itanikumbusha deni nililoweka kwako, nami nitakuwa najitahidi kupata muda wa kuweka vipande kwa niendeleavyo kuandika.
Kweli ameyakanyaga😆Ameyakanyaga
Hiyo baadae imekuwa........🤔😊Tuwepo hapa. Baadae kidogo tunaendelea
Bado nipo.Tuwepo hapa. Baadae kidogo tunaendelea