Mtego wa maandamano ya amani leo D9

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
374,279
Reaction score
866,683
Maandalizi muhimu yote yameshakamilika.. Na muda huu ninapoandika huu uzi watu wanaendelea kujongea maeneo ya makutanio
Zimetumika kila aina ya mbinu, elimu, maarifa na kuhamasishana ili maandamano haya yawe ya amani na kusiwepo uharibifu wa mali na miundombinu.. Vibaka na wezi wameshapewa onyo Kali!

LAKINI!!! Kuna mambo yanaweza kubadili kila kitu ndani ya muda mfupi kabisa
1. Mamluki wa ccm kupitia uvccm na wafadhili wao wanafanya kila mbinu kuharibu haya maandamano yasifanikiwe

2. Uchungu wa ghafla utakaowapata waandamanaji itakapotokea picha za marehemu waliopigwa risasi zitakapoonekana kwenye mabango na baadhi ya watu wakashindwa kuvumilia na kuanza kuangua vilio ama kupandisha!

3. Uchungu wa wafiwa watakaoanguka na kupoteza fahamu kwenye maandamano na kukosa huduma ya kwanza haraka

4. Police na wana usalama watakaojaribu kuwatawanya waandamanaji kwa kutumia mabomu ya machozi na mbaya zaidi risasi za moto!

5. Kitu kingine chochote ambacho kwa namna moja ama ngingine kitaleta distraction kwa waandamanaji na kuamsha hasira zao

Haya ni maandamano ya amani lakini yako very fragile kwakuwa yamebeba uchungu na maumivu ya muda mrefu.. Hivyo basi hayana tofauti kabisa na gari ya mafuta iliyopata ajali, cheche moja tu ya moto italeta madhara makubwa mno!

Tuombeane sana!
 
Nimeshaanda pyu pyu yangu nilio nunua burundi .Natoka na mbwa wangu wa kizungu nikijifanya nafanya mazoezi
 
Hii picha ya zamani si mpya mbona!
 
Nimeiona cruiser hapa kimara imebeba watu wawili na wamevaa jersey za YANGA na wanamitutu.sijawaelewa kabisa.Au timu ya YANGA siku hizi wanamikiki jeshi?
Wasimamishe uwaulize
 
Wewe uko wapi???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…