Mtazamo wangu: Mbowe asistaafu 2023

mtimawachi

JF-Expert Member
Apr 1, 2020
2,017
3,037
Mwenyekiti wa chama cha chadema mheshimiwa Freemani Mbowe ametangaza kutogombea tena uenyekiti pindi tu awamu hii itakapokwisha(2023).

OMBI:Mbowe agombee tena 2023 na baada ya hapo awamu inayofuata ndo asigombee.

SABABU:
Chadema imepitia kipindi kigumu sana hasa awamu ya 5 lakini kutokana na uimara wa MBOWE ilitoboa

Licha kutangaza kutoshiriki uchaguzi mkuu 2025, bado ninaamini chadema kitabadili gia angani na hatimaye kitashiriki. Hivyo kama MBOWE atang'atuka basi chadema itaingia kwenye uchaguzi mkuu 2025 ikiwa dhaifu.

LAKINI uchaguzi mkuu ujao utakuwa kipimo kikuu kwa chadema kuona uungwaji mkono wao kutoka kwa wananchi MBOWE ni dhahiri amechoka na anahitaji kupumzika lakini siyo 2023.

Ni bora hata angejiuzulu LEO ili mrithi wake awe na muda mwingi wa kukijenga chama kuliko kukitelekeza chama mwaka 1 kabla ya uchaguzi mkuu.

NAJUA chama kama chama kina MFUMO IMARA isingekuwa shida,ila kwa mienendo ya siasa zetu CHAMA NI MTU,na mtu mwenyewe ni MBOWE.

KI-ITIKADI mimi ni CCM(mshabiki) na nipo TIMU MAGUFULI kindakindaki
 
Ni bora hata angejiuzulu LEO ili mrithi wake awe na muda mwingi wa kukijenga chama
 
Heshimu uamuzi wa mtu bhana! We vipi!! Au ndiyo unataka Kamanda naye aingie kwenye ule mtego mliomtegea magufuli, na mwisho wa siku Mwenyezi Mungu akamtwaa, kabla ya lengo lenu ovu kutimia?
 
Heshimu uamuzi wa mtu bhana! We vipi!! Au ndiyo unataka Kamanda naye aingie kwenye ule mtego mliomtegea magufuli, na mwisho wa siku Mwenyezi Mungu akamtwaa, kabla ya lengo lenu ovu kutimia?
Mkuu licha ya kwamba mimi ni mshabiki wa ccm lakini Mbowe lazima nimpe credit yake
 
Usiogope changes, hata kwenye maisha yako binafsi ukitaka kusogea next step yakupasa uwe tayari kwa mabadiliko, na kama unakiri ameshachoka basi nae amejiona amechoka, muache apumzike, Chadema ianze phase mpya.
 
Kawaida kila inapokaribia mwisho wa uongozi wa Mbowe, hujitokeza mtu au kundi la watu kujifanya wanamshaur ili aendelee kugombea tena, na baada ya hapo Mbowe hujifanya kubadili mawazo na kuendelea kugombea uenyekiti.

Kwahiyo hii haishangazi ukute tayari mleta mada ashatengenezwa ili aje kupima upepo na kuwandaa watu kisaikolojia, huku akijifanya ni mwana CCM na baada ya hapo kitachofata ni watu wengine wataopewa kilo kumi kumi za mchele kuanza kumtaka mwenyekiti aendelee kugombea uenyekiti hadi siku mola atamchukua.
 
Usiogope changes, hata kwenye maisha yako binafsi ukitaka kusogea next step yakupasa uwe tayari kwa mabadiliko, na kama unakiri ameshachoka basi nae amejiona amechoka, muache apumzike, Chadema ianze phase mpya.
Hofu yangu chadema imetoka kwenye uchaguzi mkuu ambao kwao haukuwa mzuri kwao,sasa wamepata wasaa wa kufanya siasa
ni muda mzuri wa kukijenga chama
 
Kawaida kila inapokaribia mwisho wa uongozi wa Mbowe, hujitokeza mtu au kundi la watu kujifanya wanamshaur ili aendelee kugombea tena, na baada ya hapo Mbowe hujifanya kubadili mawazo na kuendelea kugombea uenyekiti...
Mkuu huku mtaani hadi chadema(viongozi) wenyewe wananijua kwamba mimi ni CCM,na wakiwa na vikao wanakuja kuazima viti kwangu kama haviwatoshi na hata baadhi ya michango huja kuniomba na nawachangia,ki-ufupi tunaishi hivyo
 
Watakuwepo wagombea wengine nje ya Mbowe usijali.
Wapo wengi tu kwenye maono kama Mbowe.
 
Haya kaka.
 
Watakuwepo wagombea wengine nje ya Mbowe usijali.
Wapo wengi tu kwenye maono kama Mbowe.
Kama itakuwa hivyo vizuri ila nikiangalia kikosi kazi cha chadema naona kwenye nafasi mwenyekiti sio kipana
 
Back
Top Bottom