Mtazamo wangu kwa mh. Edward lowasa

Mtazamo wangu kwa mh. Edward lowasa

hittler

Member
Joined
Jul 18, 2011
Posts
55
Reaction score
10
Napenda kuwatakia watanzania kheri ya mwaka mpya wa 2014. Kwa utafiti mchache ila wa kina juu ya waziri mkuu mstaafu Mh. Edward Lowasa nimegundua kuwa, ndiye mtu pekee anayeweza kuleta mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na kisiasa hapa nchini. Nchi imekuwa ikiyumba kwa mambo hayo matatu, si kwa uzembe wa Rais Kikwete ila kwa uzembe wa wasaidizi na washauri wa Kikwete. Kwa muda aliokuwa waziri mkuu tuliona mengi aliyofanya na ni hakika kama angebaki adi leo kama waziri mkuu tungekuwa tumeshafuta maadui wa kuu wa taifa hili yaani ujinga, maradhi na umaskini.

Ndugu zangu watanzania, tusisikilize maneno ya watu wasiopenda maendeleo ila tumwombee mh. Lowasa aweze kuja kutuongoza mwaka 2015 Mungu akipenda. Taifa linadidimia, vijana hawana ajira, wengi wamekwama kwenda vyuo vikuu kwa kukosa ada. Jibu pekee la haya yote ni Mh. Lowasa kuwa Rais wa tanzania.
 
Nasikia kuna ajira ya kumpigia debe huyu jamaa mitandaoni!Nimuone nani?maana bado sijajenga!
 
Unaweza ukapanua utafiti wako kidogo na kutueleza Lowasa amekuwa kwenye ngazi za uongozi za Taifa hili kwa muda gani, na mchango wake ni upi?
 
Uelezee kwa kina UTAJIRI wa Lowassa ambaye amekuwa kwenye ajira ya UMMA tangu alipomaliza shule.
 
Lowassa ataleta mvua ya kichina haya ni mabadiliko makubwa
 
Naamini kati ya watoto au wanafamilia wako kuna waliosoma shule za kata, au kufaidi mradi wa maji ya kutoka mto nile. Tusiwe wepesi kupingana na uwezo wa utendaji wa Mh. Lowasa.
 
Utajiri wa Lowasa ni wa muda tokea kwenye familia, hatakuwa na muda wa kutafuta biashara za familia kama wengine bali kuwakomboa wananchi, ata akina Sumaye, Sitta na Kina Membe ni matajiri wakubwa sana ila hawana uthubutu wa kiutendaji, wangewezaje kuona taifa linadidimia bila kumshauri rais? Lowasa aliweza kushauri na kutoa maamuzi, alafu ndugu yangu swala la utajiri Mungu ndiye anayepanga, usi mjudge mtu kwa alichonacho bali uwezo wake kiutendaji.
 
Naamini kati ya watoto au wanafamilia wako kuna waliosoma shule za kata, au kufaidi mradi wa maji ya kutoka mto nile. Tusiwe wepesi kupingana na uwezo wa utendaji wa Mh. Lowasa.
Ulimsikia Sumaye? Unajua kala ngapi kwenye mradi ule wa maji?
 
Yaan ukisikia mpuuzi ni ww tena No moja na huenda ikawa lowasa anakutumia 0654 mpya, kama alichakachua wazir mkuu na aliiba akajiuzulu mwnyw leo hii unampigia debe!"
 
Hivi SUMAYE na Lowasa nani kafanya kazi nzuri? dadavua hapa kutushawishi nani bora
 
Utajiri wa Lowasa ni wa muda tokea kwenye familia, hatakuwa na muda wa kutafuta biashara za familia kama wengine bali kuwakomboa wananchi, ata akina Sumaye, Sitta na Kina Membe ni matajiri wakubwa sana ila hawana uthubutu wa kiutendaji, wangewezaje kuona taifa linadidimia bila kumshauri rais? Lowasa aliweza kushauri na kutoa maamuzi, alafu ndugu yangu swala la utajiri Mungu ndiye anayepanga, usi mjudge mtu kwa alichonacho bali uwezo wake kiutendaji.
Ile Party ya tarehe 1 zilitumika shilingi ngapi? Zilitoka wapi? Kwa malengo gani? Eleza kwa kina utajiri wa Lowasa unatokana na nini. Usitudanganye kwa ving'ombe vya familia na Mungu kumshushia yeye utajiri.

Pili, tuambie Lowasa aliambiwa nini na Mwalimu alipochukua fomu ya kuusaka URAIS mwaka 1995.
 
Jibu pekee la haya yote ni Mh. Lowasa kuwa Rais wa tanzania.

tuwekee sera zake tusome tuone kama kweli ana lolote la maana, siyo kusema jumla-jumla tu utadhani sisi tunaosoma bandiko lako hatuna akili au hatufikirii
 
Hivi ni kweli anatetemeka mikono na hawezi kuandika...
 
Napenda kuwatakia watanzania kheri ya mwaka mpya wa 2014. Kwa utafiti mchache ila wa kina juu ya waziri mkuu mstaafu Mh. Edward Lowasa nimegundua kuwa, ndiye mtu pekee anayeweza kuleta mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na kisiasa hapa nchini. Nchi imekuwa ikiyumba kwa mambo hayo matatu, si kwa uzembe wa Rais Kikwete ila kwa uzembe wa wasaidizi na washauri wa Kikwete. Kwa muda aliokuwa waziri mkuu tuliona mengi aliyofanya na ni hakika kama angebaki adi leo kama waziri mkuu tungekuwa tumeshafuta maadui wa kuu wa taifa hili yaani ujinga, maradhi na umaskini.

Ndugu zangu watanzania, tusisikilize maneno ya watu wasiopenda maendeleo ila tumwombee mh. Lowasa aweze kuja kutuongoza mwaka 2015 Mungu akipenda. Taifa linadidimia, vijana hawana ajira, wengi wamekwama kwenda vyuo vikuu kwa kukosa ada. Jibu pekee la haya yote ni Mh. Lowasa kuwa Rais wa tanzania.

Hivi Watanzania tutaendelea kuwa w.a.p.u.m.b.a.f.u mpaka lini? Hivi umaskini wa nchi unaondolewa kwa kulipa Richmond milioni 135 kwa cku?, nasema hivyo kwa kuwa Richmond ilianza wakati akiwa waziri mkuu na hakuna hatua alichukua hadi alipokuja kuondolewa na tume. Cjui kwanini mijitu mingine inasahau haraka
 
lowasa atakua rais wa kwanza aliyeingia kwa nguvu zake ya kugawa fedha kama njugu kwa maana hiyo hafai kwanini anahangaika kiasi hiki anataka kutuuza kwa rostam
 
Hivi huyu Hittler hayaoni mapungufu ya huyo EL wake?
Kwanza afya yake imezorota sana na pia umri wake umeenda mno. Kama kuutaka urais aende Zimbabwe kwani watamchagua bila kupingwa!
Yaani vijana wasomi pamoja na huyu mleta uzi japo umri wake nashindwa kuukadiria wananiacha hoi kweli! Ina maana hamna ambition or goal la kuachieve katika maisha yako zaidi ya kuwapigia wazee chapuo la kuongoza! Aibu kweli hii! Ndo maana aliwawekea shule za kata ili kuifunga akili yako ka mbuzi wa kichaga ukose exposure na kusocialize na watu tofauti na wa kwenye kijiji chako.
Tatizo mnashangilia kila kitu but hamkutafiti kilichokuwa kwenye shule za kata (malengo).
Jipiganie mwenyewe achana na vikongwe. Ni wakati wa vijana amkeni!
 
Back
Top Bottom