Mtazamo wangu juu ya Makonda na TEF

Mtazamo wangu juu ya Makonda na TEF

Baada ya kwenda na askari clouds then taarifa aje ampe mkulu? Kwani yeye ndio kamtuma?

Ikiwa mkulu alidiriki kupiga simu akasema anawapenda shilawadu....hv hujiongezi aseee
 
Shida wanaotangaza kuzuia kuandikwa habari ni TEF ambao ni jukwaa la wahariri tena waliopo Dar tu tena bado ambao ni waajiriwa hvyo ugali wao unatokana na kuandikwa kwa Habari.

MCT nao hvyo hvyo ,UTPC nao sio kila mwanahabari ni mwanachama zaidi ya 80% ya wanahabari sio wanachama hvyo ni kikundi kidogo cha watu ndio wana jumuiya.

MOAT ambao ni wamiliki wao wanataka pesa na faida wao ni wafanyabiashara watalaani tu kamwe hutaona wakitoa matamko ama zuio la kipumbavu kama TEF ama MCT sababu mdau mkubwa mwenye Habari nyingi ni serikali.

Wengi tunashindwa kufaham Habari inaendeshwa na wadau na mdau mkubwa wa Habari ni serikali hvyo hata hayo matamko yao wahariri wachache ndio walioshiriki kutoa bila kutumia Busara na kushirikiana na Maboss zao MOAT.

Ahsante sana
 
[emoji23][emoji23][emoji23] wewe nawe ni mwanahabari...??safari bado ndefu na inawezekana kuna chombo cha habari kimekuamini kabisa,RC hawezi kua mvamizi eti hapo ndio umeonyesha umetumia kiungo tofauti kuwaza.

Yani hv ndo umechangia na kutoa hoja....duuuuh
 
Yani hv ndo umechangia na kutoa hoja....duuuuh

Yaani nitoe hoja kwako ambae naona kabisa hauja shughulisha ubongo wako kufikiri kabisa,mtu kama wewe ni kukumbusha tu uko ndani ya kichwa chako Mungu ameweka kitu ambacho unatakiwa ukitumie ukiwa unajenga hoja.
 
Eti nasikia haukuwa uvamizi, ilikuwa ni ziara ya kushitukiza🙄
 
Haha wewe eti " kuzui vyombo vya habari visitoe habari za makonda hakumkomiu makonda Bali unaekomolewa ni mwanachi" kaka ww una akili ww kwa hiyo TEF wajinga sana walipoamua hvyo?? Makonda mpenda kik na TEF walifanya hvyo makusudi sababu nguvu ya media ni kubwa sana... Afu eti labda alienda kuangalia usalama hahah hv kaka umesoma media law wewe ? Unajua sheria ya media house? Au we unapofanyia kazi watu wanaingia tu kama wapo toilet... Aijalishi makonda ata kama ni mkuu wa mkoa, cjui mwakilishi wa mkulu, cjui mwenyedhaman ya mkoa katika ulinzi cjui nini kitendo cha kuingia kwenye media house na siraha za moto naludia SIRAHA ZA MOTO ni kuvunja kanuni na sheria za media... Sababu media ni chombo salama Sasa siraha za moto zinahusiana vp na ww kuingia kwa mabunduki na polisi??.. umenikela Sana na uzi huu yaan nyie ndo waandishi uchwara aisee yaan vindumi vya kuwili tu..


Sent using Jamii Forums mobile app

Kwanza inaitwa Silaha na Siraha...Hlf Pili usikremishe kuwa hairuhusiwi kuingia na silaha kwenye media house tu...Kwa mfano ikitokea kwenye media kuna majambazi bado vyombo vya usalama havitaruhusiwa kuingia na silaha? Sheria imetoa option mzee.
 
Kwanza inaitwa Silaha na Siraha...Hlf Pili usikremishe kuwa hairuhusiwi kuingia na silaha kwenye media house tu...Kwa mfano ikitokea kwenye media kuna majambazi bado vyombo vya usalama havitaruhusiwa kuingia na silaha? Sheria imetoa option mzee.
Ushasema "ikitokea" sasa pale majambazi walitokea?? Je kuna hali yoyote ilihashilia kama usalama ni mdogo mpaka aende na bunduki? Vitu vingine tujiongeze jamani.. tatizo bongo nanyie watu amuelewi media ilivyo amjui nguvu ya media ndo maana unaongea shit tu.. mm kwa upande wangu.. mdosi alivamia 100% inasemekana daily naendaga bila askar why cku hiyo askar + bunduki= kuvamia tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba nitoe mtazamo wangu kuhusu suala linaloendelea kati ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Mkuu wa mkoa wa Dar-es-salaam Paul Makonda.

Naomba ieleweke kwamba haya ni maoni yangu binafsi , sijashurutishwa na mtu ila ni baada ya kufanya uchunguzi binafsi juu ya suala hili.

Kwanza kabisa nianze na suala lenyewe la Makonda kwenda Clouds bila taarifa na baadae vyombo vyote vya habari kuripoti kuwa “Makonda Kavamia clouds”. Uchunguzi wangu ulianzia hapa……Je Mkuu wa Mkoa anaweza kuwa mvamizi? Ikumbukwe kuwa RC ni mwakilishi wa rais katika ngazi ya mkoa lakini pia ndie Mwenyekiti wa Usalama wa mkoa, inakuaje akawa mvamizi?.

Je ikiwa alikwenda kwa ajili ya upekuzi katika eneo lile, atakuwa amekosea? Makonda angelikuwa ni mbunge tungekuwa tuna haki ya kumuita mvamizi lakini ni Mwakilishi wa rais ngazi ya mkoa na pia ni mwenyekiti wa usalama wa mkoa hawezi kuwa mvamizi.

Baraza la Habari linataka makonda aombe radhi….Swali la kujiuliza ni Je Makonda alifanya kosa gani? (Kumbuka kutokana na vyeo vyake hatuwezi kutumia neno mvamizi)….Nilichogundua juu ya hili, wanahabari wengi tunafuata mkumbo bila kufanya uchunguzi wa tukio lenyewe.

TEF walitoa tamko kuwa vyombo vyote vya habari visiandike habari zinazomuhusu Makonda mpaka pale atakapoomba radhi.

Wiki chache baadae Wahariri waandamizi wakaandaliwa warsha (seminar) na TANAPA ya wiki nzima wakaenda Tanga.

Haikupita muda Mheshimiwa Rais akawakutanisha huko huko Tanga Makonda na Ruge mbele ya kadamnasi na akowaomba wamalize tofauti zao.

Wiki chache baadae TEF wakaitisha Press na kusema kwamba wamemalizana na Makonda na habari zake ziandikwe kwenye vyombo vya habari.

Hivi mpaka hapa bado hamjagundua kitu? Mheshimiwa rais hakutaka yawe wazi yaliyotokea lakini sisi tunataka tufahamu kila kitu ilhali hawa ndio viongozi.

Kuna kitu kinaitwa ‘Privacy’ (Usiri/faragha) kila binadamu anacho hiki….anaficha yale anayoona hayapaswi kufahamika kwa watu wengine vivyo hivyo kwa serikali haiwezi kuanika kila tukio/ taarifa kwa wananchi wake. Ikiwa rais amesema yaishe ni kwa nini tunataka Makonda aombe radhi.

Naomba ieleweke kuwa hii radhi anayoombwa Makonda aitamke haipo kisheria isipokuwa ni busara…..Sasa kwa matukio haya yotee bado hujajiongeza?.

Kuzuia vyombo vya habari visitoe habari za Makonda hakumkomoi Makonda bali anaekomolewa ni mwananchi anaetaka kujua kiongozi wake anafanya nini kwani hata yeye kuna mengine hapendi yaandikwe, kwa hili la kutoandikwa habari zake kwenye vyombo vya habari kisa kikiwa ni tukio la Clouds, mimi binafsi nasema ‘NO’ ila kama kuna jingine sawa…….lakini pia hili suala la kuzuia Totally habari zake ni kumnyima mwananchi habari.

Ikitokea wananchi wakavishtaki vyombo vya habari watakuwa wana kosa? Mana wananyimwa habari……Naomba nimalizie kwa kusema kuwa hili jambo ni vema limalizike mana kama mpaka rais ameamua kuliingilia na kulimaliza sisi tunapaswa tuheshimu busara zake…….Ya Ngoswe muachie Ngoswe.

Dull Santo

(Mwanahabari)
Kuna taarifa gani ya maana kwa kiongozi kama yule ambayo ina umhimu saana kwa mwananchi. Hana heshima, mwenye majivuno, mwenye kupenda makuu. Ni mhimu akawa mnyenyekevu
 
Ushasema "ikitokea" sasa pale majambazi walitokea?? Je kuna hali yoyote ilihashilia kama usalama ni mdogo mpaka aende na bunduki? Vitu vingine tujiongeze jamani.. tatizo bongo nanyie watu amuelewi media ilivyo amjui nguvu ya media ndo maana unaongea shit tu.. mm kwa upande wangu.. mdosi alivamia 100% inasemekana daily naendaga bila askar why cku hiyo askar + bunduki= kuvamia tu

Sent using Jamii Forums mobile app

We una uhakika gani km hakukuwa na ishu ya kwenda na silaha?

Narudia tena vitu vingine ni "Privacy" si kila kinachofanywa basi ukijue...hata baba/mtoto wako hawezi kujua vyote unavyofanya
 
Kuna taarifa gani ya maana kwa kiongozi kama yule ambayo ina umhimu saana kwa mwananchi. Hana heshima, mwenye majivuno, mwenye kupenda makuu. Ni mhimu akawa mnyenyekevu

Whaaat??? unasema hakuna taarifa ya maana? % kubwa ya matangazo kwenye vyombo vya habari yanatokea serikalini...Kuna vyombo vya hbr vinapata matangazo ya serikali tu...Hv nao wakigoma kutoa matangazo kwenye vyombo hv waandishi watakula wapi?

Kuna vyombo vya hbr vinapatkana Dar tu...hv nao vikisusiwa kupewa matangazo vitatoa wapi mapato?

% Kubwa ya hao viongozi wa TEF wanaishi dar...hv serikali nayo ikiamua kuonesha kususa na wao wataishije.

Mfano wanaweza kusumbuliwa tu....Lets say Order inatoka kuwa kila itakapoonekana gari ya m/kiti wa TEF isimamishwe na ikaguliwe kwa zaidi ya dk 30....tena kila siku....huoni km na yy atapata usumbufu?
 
Rais alishawapatanisha hadharani,kwangu mie mgogoro umeisha ila kwa wapambe waliokua wanafaidika wameumizwa sana.
Makonda anafanya kazi zake kama kawaida,ule wito wa kutaka ajiuzulu au ang'olewe,hao wapiga kelele wamechoka sasa hawana tena nguvu.
Makonda anatumia channel ten na Efm kuwapasha habari mbali mbali wananchi wa Dar es alaam,vyombo hivyo vinatosha kabisa kuwafikia walengwa kwa 90%,kilichobaki tufanye kazi zetu tusubiri mgogoro mwingine maana inauma sana kumuandama mtu,huku yeye wala hatikisiki wala hajali.
 
Rais alishawapatanisha hadharani,kwangu mie mgogoro umeisha ila kwa wapambe waliokua wanafaidika wameumizwa sana.
Makonda anafanya kazi zake kama kawaida,ule wito wa kutaka ajiuzulu au ang'olewe,hao wapiga kelele wamechoka sasa hawana tena nguvu.
Makonda anatumia channel ten na Efm kuwapasha habari mbali mbali wananchi wa Dar es alaam,vyombo hivyo vinatosha kabisa kuwafikia walengwa kwa 90%,kilichobaki tufanye kazi zetu tusubiri mgogoro mwingine maana inauma sana kumuandama mtu,huku yeye wala hatikisiki wala hajali.

Agiza mirinda nyeusi nakuja kulipa
 
Naomba tuongee hoja mkuu...nimeweka mtazamo wangu nawe ni vema uweke wako

Huna hoja yeyote uliyoweka hapo yaan wananchi tukashitaki kisa Bashite hapewi coverage wee jamaa acha dharau basi tumeshindwa kushitaki bunge live leo tukashitaki tupate habari za muhalifu
 
Ahsante sana mkuu Ingawa hujajadili hoja hata mstari mmoja zaidi ya kunishambulia mm na taaluma yangu ila nathamini mchango wako...Shukran.
Nijadili hoja isiyokuwepo? Hivi kwa uwezo wako hapo ndiyo unaona umetoa hoja!!!! Kwa kifupi umedhihirisha kwamba wewe ni kichwani mambo hayako sawa. Unatia aibu kujiita mwanahabari huku unasumbuliwa na njaa ya kichwa na tumbo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom