Mtazamo wangu juu ya Makonda na TEF

Mtazamo wangu juu ya Makonda na TEF

dully santo

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2014
Posts
260
Reaction score
334
Naomba nitoe mtazamo wangu kuhusu suala linaloendelea kati ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Mkuu wa mkoa wa Dar-es-salaam Paul Makonda.

Naomba ieleweke kwamba haya ni maoni yangu binafsi , sijashurutishwa na mtu ila ni baada ya kufanya uchunguzi binafsi juu ya suala hili.

Kwanza kabisa nianze na suala lenyewe la Makonda kwenda Clouds bila taarifa na baadae vyombo vyote vya habari kuripoti kuwa “Makonda Kavamia clouds”. Uchunguzi wangu ulianzia hapa……Je Mkuu wa Mkoa anaweza kuwa mvamizi? Ikumbukwe kuwa RC ni mwakilishi wa rais katika ngazi ya mkoa lakini pia ndie Mwenyekiti wa Usalama wa mkoa, inakuaje akawa mvamizi?.

Je ikiwa alikwenda kwa ajili ya upekuzi katika eneo lile, atakuwa amekosea? Makonda angelikuwa ni mbunge tungekuwa tuna haki ya kumuita mvamizi lakini ni Mwakilishi wa rais ngazi ya mkoa na pia ni mwenyekiti wa usalama wa mkoa hawezi kuwa mvamizi.

Baraza la Habari linataka makonda aombe radhi….Swali la kujiuliza ni Je Makonda alifanya kosa gani? (Kumbuka kutokana na vyeo vyake hatuwezi kutumia neno mvamizi)….Nilichogundua juu ya hili, wanahabari wengi tunafuata mkumbo bila kufanya uchunguzi wa tukio lenyewe.

TEF walitoa tamko kuwa vyombo vyote vya habari visiandike habari zinazomuhusu Makonda mpaka pale atakapoomba radhi.

Wiki chache baadae Wahariri waandamizi wakaandaliwa warsha (seminar) na TANAPA ya wiki nzima wakaenda Tanga.

Haikupita muda Mheshimiwa Rais akawakutanisha huko huko Tanga Makonda na Ruge mbele ya kadamnasi na akowaomba wamalize tofauti zao.

Wiki chache baadae TEF wakaitisha Press na kusema kwamba wamemalizana na Makonda na habari zake ziandikwe kwenye vyombo vya habari.

Hivi mpaka hapa bado hamjagundua kitu? Mheshimiwa rais hakutaka yawe wazi yaliyotokea lakini sisi tunataka tufahamu kila kitu ilhali hawa ndio viongozi.

Kuna kitu kinaitwa ‘Privacy’ (Usiri/faragha) kila binadamu anacho hiki….anaficha yale anayoona hayapaswi kufahamika kwa watu wengine vivyo hivyo kwa serikali haiwezi kuanika kila tukio/ taarifa kwa wananchi wake. Ikiwa rais amesema yaishe ni kwa nini tunataka Makonda aombe radhi.

Naomba ieleweke kuwa hii radhi anayoombwa Makonda aitamke haipo kisheria isipokuwa ni busara…..Sasa kwa matukio haya yotee bado hujajiongeza?.

Kuzuia vyombo vya habari visitoe habari za Makonda hakumkomoi Makonda bali anaekomolewa ni mwananchi anaetaka kujua kiongozi wake anafanya nini kwani hata yeye kuna mengine hapendi yaandikwe, kwa hili la kutoandikwa habari zake kwenye vyombo vya habari kisa kikiwa ni tukio la Clouds, mimi binafsi nasema ‘NO’ ila kama kuna jingine sawa…….lakini pia hili suala la kuzuia Totally habari zake ni kumnyima mwananchi habari.

Ikitokea wananchi wakavishtaki vyombo vya habari watakuwa wana kosa? Mana wananyimwa habari……Naomba nimalizie kwa kusema kuwa hili jambo ni vema limalizike mana kama mpaka rais ameamua kuliingilia na kulimaliza sisi tunapaswa tuheshimu busara zake…….Ya Ngoswe muachie Ngoswe.

Dull Santo

(Mwanahabari)
 
Kuna kitu umesahau.
Makonda kama unavyojua alikuwa na bifu na gwajima.sasa makonda alikuwa na kipindi kilichomuhusu mwanamke ambaye inadaiwa gwajima kazaa nae.makonda akasubiri kipindi kirushwe akaona kimya.ndo kwenda huko clouds kuhoji kwanini kipindi hakijarushwa.
Kilichotokea huko mimi sijui.
Nilimsikia ruge siku ile alipo kuwa anatoa ufafanuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ruge anasema ogopa Mungu na Teknolojia.
Bado hujajifunza kitu, alitaka kujisafisha hadharani teknolojia ikakataa hivi kusema hivi

'Mengi yametokea,mengi yamesemwa, Leo nashukuru tulipofikia kama kuna MTU, taasisi nimeikosea Mimi ni binadamu naomba radhi,na wale ambao wanahisi walinikosea binafsi nimewasamehe. "

Kama binadamu unapungukiwa nn kutamka maneno hayo ambayo yanakila harufu ya uinjilishaji kwa MTU yeyote anayejihisi kuwa ana kiu ya kumtafuta Mungu.

Neno SINTOOMBA RADHI ni herufi 16 zenye kila sifa ya uadui,ugomvi na kutopenda suluhu.ni herufi zinazo shangiliwa sana na shetani, kama kweli tunampenda Mungu muda upo tusawazishe.
 
Namshukuru mungu na wazazi wangu kuwa kunisisitiza neno 'samahani' na uzito wake katika kuleta amani

Pole kwa wale wote wanaoona kusema samahani ni dhambi na udhaifu..

Binafsi namshauri tu mh. Makonda aseme tu samahani na maisha yaendelee, maana hatopungukiwa kitu...

Kama alivamia/alisingiziwa mungu ndiye anajua yote na ndiye atakayeonesha ukweli.
 
  • Thanks
Reactions: Dyf
Naomba nitoe mtazamo wangu kuhusu suala linaloendelea kati ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Mkuu wa mkoa wa Dar-es-salaam Paul Makonda.

Naomba ieleweke kwamba haya ni maoni yangu binafsi , sijashurutishwa na mtu ila ni baada ya kufanya uchunguzi binafsi juu ya suala hili.

Kwanza kabisa nianze na suala lenyewe la Makonda kwenda Clouds bila taarifa na baadae vyombo vyote vya habari kuripoti kuwa “Makonda Kavamia clouds”. Uchunguzi wangu ulianzia hapa……Je Mkuu wa Mkoa anaweza kuwa mvamizi? Ikumbukwe kuwa RC ni mwakilishi wa rais katika ngazi ya mkoa lakini pia ndie Mwenyekiti wa Usalama wa mkoa, inakuaje akawa mvamizi?.

Je ikiwa alikwenda kwa ajili ya upekuzi katika eneo lile, atakuwa amekosea? Makonda angelikuwa ni mbunge tungekuwa tuna haki ya kumuita mvamizi lakini ni Mwakilishi wa rais ngazi ya mkoa na pia ni mwenyekiti wa usalama wa mkoa hawezi kuwa mvamizi.

Baraza la Habari linataka makonda aombe radhi….Swali la kujiuliza ni Je Makonda alifanya kosa gani? (Kumbuka kutokana na vyeo vyake hatuwezi kutumia neno mvamizi)….Nilichogundua juu ya hili, wanahabari wengi tunafuata mkumbo bila kufanya uchunguzi wa tukio lenyewe.

TEF walitoa tamko kuwa vyombo vyote vya habari visiandike habari zinazomuhusu Makonda mpaka pale atakapoomba radhi.

Wiki chache baadae Wahariri waandamizi wakaandaliwa warsha (seminar) na TANAPA ya wiki nzima wakaenda Tanga.

Haikupita muda Mheshimiwa Rais akawakutanisha huko huko Tanga Makonda na Ruge mbele ya kadamnasi na akowaomba wamalize tofauti zao.

Wiki chache baadae TEF wakaitisha Press na kusema kwamba wamemalizana na Makonda na habari zake ziandikwe kwenye vyombo vya habari.

Hivi mpaka hapa bado hamjagundua kitu? Mheshimiwa rais hakutaka yawe wazi yaliyotokea lakini sisi tunataka tufahamu kila kitu ilhali hawa ndio viongozi.

Kuna kitu kinaitwa ‘Privacy’ (Usiri/faragha) kila binadamu anacho hiki….anaficha yale anayoona hayapaswi kufahamika kwa watu wengine vivyo hivyo kwa serikali haiwezi kuanika kila tukio/ taarifa kwa wananchi wake. Ikiwa rais amesema yaishe ni kwa nini tunataka Makonda aombe radhi.

Naomba ieleweke kuwa hii radhi anayoombwa Makonda aitamke haipo kisheria isipokuwa ni busara…..Sasa kwa matukio haya yotee bado hujajiongeza?.

Kuzuia vyombo vya habari visitoe habari za Makonda hakumkomoi Makonda bali anaekomolewa ni mwananchi anaetaka kujua kiongozi wake anafanya nini kwani hata yeye kuna mengine hapendi yaandikwe, kwa hili la kutoandikwa habari zake kwenye vyombo vya habari kisa kikiwa ni tukio la Clouds, mimi binafsi nasema ‘NO’ ila kama kuna jingine sawa…….lakini pia hili suala la kuzuia Totally habari zake ni kumnyima mwananchi habari.

Ikitokea wananchi wakavishtaki vyombo vya habari watakuwa wana kosa? Mana wananyimwa habari……Naomba nimalizie kwa kusema kuwa hili jambo ni vema limalizike mana kama mpaka rais ameamua kuliingilia na kulimaliza sisi tunapaswa tuheshimu busara zake…….Ya Ngoswe muachie Ngoswe.

Dull Santo

(Mwanahabari)
Tangu 2014 uko JF halafu bado una akili za aina hii??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ruge anasema ogopa Mungu na Teknolojia.
Bado hujajifunza kitu, alitaka kujisafisha hadharani teknolojia ikakataa hivi kusema hivi

'Mengi yametokea,mengi yamesemwa, Leo nashukuru tulipofikia kama kuna MTU, taasisi nimeikosea Mimi ni binadamu naomba radhi,na wale ambao wanahisi walinikosea binafsi nimewasamehe. "

Kama binadamu unapungukiwa nn kutamka maneno hayo ambayo yanakila harufu ya uinjilishaji kwa MTU yeyote anayejihisi kuwa ana kiu ya kumtafuta Mungu.

Neno SINTOOMBA RADHI ni herufi 16 zenye kila sifa ya uadui,ugomvi na kutopenda suluhu.ni herufi zinazo shangiliwa sana na shetani, kama kweli tunampenda Mungu muda upo tusawazishe.

Makonda anaongoza serikali ngazi ya mkoa...Ikiwa alipewa order na boss wake ataombaje yeye msamaha? Km umeshaona yy anadiriki kusema hawezi kuomba radhi unadhani nini kipo nyuma ya kauli yake?
 
Boss wake yupi?
 
Kuna kitu umesahau.
Makonda kama unavyojua alikuwa na bifu na gwajima.sasa makonda alikuwa na kipindi kilichomuhusu mwanamke ambaye inadaiwa gwajima kazaa nae.makonda akasubiri kipindi kirushwe akaona kimya.ndo kwenda huko clouds kuhoji kwanini kipindi hakijarushwa.
Kilichotokea huko mimi sijui.
Nilimsikia ruge siku ile alipo kuwa anatoa ufafanuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hata Makonda hili mwenyewe alilisema wakati anahojiwa na startv ila hakunyoosha maneno na hiyo ndio sbb kubwa ilompeleka pale ... nashangaa mle mada kasahau hayo
 
Akili ni nywele sa inawezekena zako hazikuwahi kuota kabisa au unavinyeleo tu!
 
Eti Rais kasema yaishe kwani ameshasema mangap na anasema kwa faida ya nani

iPhone 7 /A1786)
 
Kuna kitu umesahau.
Makonda kama unavyojua alikuwa na bifu na gwajima.sasa makonda alikuwa na kipindi kilichomuhusu mwanamke ambaye inadaiwa gwajima kazaa nae.makonda akasubiri kipindi kirushwe akaona kimya.ndo kwenda huko clouds kuhoji kwanini kipindi hakijarushwa.
Kilichotokea huko mimi sijui.
Nilimsikia ruge siku ile alipo kuwa anatoa ufafanuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app

.
 
Eti Rais kasema yaishe kwani ameshasema mangap na anasema kwa faida ya nani

iPhone 7 /A1786)

Anasema kwa faida ya wananchi mana wao hawafanyiwi haki na vyombo vya habari kutoandika habari za RC wa Dar hata km ni za maendeleo.
 
Back
Top Bottom