Mtazamo wa kibiashara na kiuchumi

bigmukolo

JF-Expert Member
Mar 6, 2012
597
2,225
Hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kupata maendeleo makubwa kiuchumi duniani pasipo kuweka Akiba.Jiulize Mwezi January umeisha, Je! umeweka Akiba kutokana na kipato ulichotengenezaMwezi January kweli? Au ndo imeishia kulipa madeni na kupunguza Changamoto tu. Katika maswala ya uchumi na maendeleo kuna vitu vitatu ambavyo unapaswa kuvifahamu navyo ni;
i) Kipato
ii) Matumizi
iii) Akiba
Hivi vitu vitatu jinsi gani vinavyotumika ndivyo vitakufanya wewe ubaki na pesa uweze kufanya kitu cha nne ambacho kinaitwa KUWEKEZA.Mtihani mkubwa kwa watu wengi sana wanaotengeneza kipato ni kutoweka Akiba(savings).Yaani Kila Mwezi unaanza upya na zero balance. Huu ni ugonjwa Sugu na unawasumbua wengi sana vijana kwa wazee.

Moja ya sababu ya watu wengi kwanini wanaingia katika MADENI ni kwa sababu ya kutoweka AKIBA. Kutoweka akiba ni ishara ya wewe kwamba huweki mipango ya baadae yaani huna plan.
Kuna faida nyingi za kuweka akiba ambazo hazihesabiki. Maisha mazuri ya kesho yanategemea unafanya nini leo hivyo kama leo huweki akiba unatengeneza njaa ya kesho. Ata kama unapata sh 1000 kwa siku bado unaweza kuweka akiba ata sh 100. Kama ulikuwa huweki akiba anza leo kuweka akiba.

Akiba haiozi, akiba ni hazina yako, akiba ni amana yako. Kesho unayoitamani anza kuijenga leo kwa kuweka akiba na kuwekeza.Akiba itakupunguzia stress za kuwapiga VIRUNGU na VIBOMU marafiki kila siku hadi wanakukimbia wanakuona mzigo mwisho wa siku unaanza kujenga chuki. Sometimes vijana tunapobarikiwa kutengeneza kipato hata kama ni kidogo tunamatumizi mengi ambayo hayana ulazima, basi tujaribu walau kuchuja Kipi kifanyike kwa muda gani na kwa bajeti gani. Itatusaidia kusogea mbele taratibu taratibu sio haba, kwani haba na haba hujaza kibaba. AKIBA tusiichukulie poa,,,
 
It depends on how much u earn and responsibilities u have. Uwezi kuwa na familia ya watoto watatu alafu kipato chako kwa siku unambie unaweza kusave labda uwe mchawi. Uku baba yako analia shida uku Mjomba anaumwa acha wewe bwana.
.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom