kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,083
Nimesoma ujumbe wa Julias Mtatairo ambao anasema kuwa Cuf wanapambana katika vita kali ya dhidi ya Lipumba, Dola, ACT pamoja na CCM. Tukiachana na vyama vya siasa alivyovitaja Mtatiro na Prof: Lipumba wanayehangaika naye nimeshangazwa kwa kuiingiza Dola katika mapambano yao.
Inakuwaje wanasiasa watanzania wanaposhindwa na kupatana baada kuparaganya huwa wanaisingia Dola, kama anavyotaka Mtatiro kuuaminisha umma kuwa ndio wanaowasababisha wao kugombana kwao?
inasikitisha sana mwanasiasa kijana kama kama Julias Mtatiro tena ni aibu kusema kuwa cuf wanapambana na Lipumba+Systeam+Ccm+ACThuku akitaka huruma ya wananchi ili waonekane kuwa wanaonewa katika mgogoro huo wakati ni uzembe wa Sharif Hamadi ndio uliwafikisha hapo.
Laiti kama Sharifu Hamadi asingeichelewesha barua ya kujiuzulu kwa Lipumba na kuitisha mkutano mkuu amabao ungekubali kujiuzulu kwake ndani ya muda muafaka haya yanayotukea leo yangetokea?
Mtatiro mara kwa kwa amekuwa akinukuliwa na vyombo vya habari au akiandika katika mitandao ya kijamii kuwa Lipumba alisutwa na dhamira yake na kuamua kujiuzulu, inakuwaje leo anataka kurudi Cuf, eti anatumiwa na systeam khaa?
Ni kweli kabisa kuwa Prof: Lipumba katika maelezo yake wakati alipokuwa akijiuzulu wadhifa wake, gwiji na galacha huyo wa uchumi alitanabahisha kwamba dhamira yake ilimsuta kuendelea kumuunga mkono Edward Lowassa aliyejiunga na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi-UKAWA ili kugombea urais wa nchi hii.
Msimamo wa Profesa Lipumba wa kutokuwa na imani juu ya Lowassa, aliyetoka CCM na kujiunga na CHADEMA ili agombee urais, haukuchipua tu mithili ya uyoga, bali ulianza siku nyingi tangu kipindi Lowassa angali CCM. Hivyo kudhihirisha maoni yake ilikuwa ni haki yake ya msingi na ya kikatiba. Na kuyasimamia hayo bila ya kutetereka ilikuwa ni ithibati ya ujasiri na kutoyumba kwake. Nani asiyemtaka mwenyekiti kama huyo? mwenye msimamo imara
Wanasiasa wengi, hasa wa upinzani, hivi sasa wanalalama kuwa demokrasia inaminywa hapa nchini kutokana na kuzuiliwa kwao kutoa maoni yao kupitia mikutano ya hadhara na makongamano juu ya vile wanavyoviamini na kuvisimamia.
Wanasiasa haohao, ndiyo waliyemshambulia na wanaoendelea kumshambulia mpinzani mwenzao Profesa Lipumba, kwa ‘kosa’ la kutoa maoni na misimamo yake juu ya kile alichokiamini.
Yaani walimtaka Profesa Lipumba aikalifishe nafsi yake kwa kutokuwa huru kutoa maoni, na misimamo yake ili tu wao wakidhi matlaba zao, halafu na wao wanaloloma kubinywa uhuru wao wa kutoa maoni yao mikutanoni.
Sasa kwa kuwa uchaguzi ulikwishamalizika, na kwamba Lowassa si mgombea tena, hivyo Profesa Lipumba akaonelea kwamba ili kuendelea kukiimarisha chama chake, ni vyema arejee kwenye kiti chake ambacho kwa yakini kabisa bado kina vumbi tangu alipokiacha kwa kukosa wa kukikalia na ukizingatia hakuna mkutano mkuu ulioitishwa kwa muda wa zaidi ya miezi sita tangu alipojiuzulu wala kujibiwa kwa barua yake, ilikuwa sahihin kwake kutengua uamuzi wake na si kosa nla kikatiba kwa mujibu wa chama chao hicho cha Cuf.
Maajabu yakaanzia hapo; baadhi ya upinzani hasa wasiokuwa wanachama wa CUF, wakaibuka na kujifanya wasemaji wa CUF kwa kumshambulia tena Lipumba kuwa hafai kurejea kitini kwa hoja kwamba Lowassa angali Chadema.
Yaani baadhi ya wafuasi, washabiki, wanachama, wakereketwa, wafurukutwa, na hasa wa Chadema, walioshindwa kumburuza na kumsujudisha kwao Profesa Lipumba ili aisaliti dhamira yake ya kutomkubali Lowassa, leo wanataka kuwaburuza na kuwasujudisha wana CUF wamkane.
Pamoja na figisufigisu zote hizo lakini Lipumba akaibuka kidedea leo hii wanasingizia Dola, kwa lipi haswa, kwanini Dola hawakumtumia Lipumba wakati wa Bunge la katiba ambalo yeye Lipumba alichangia kwa kiasai nkikubwa kukwamisha mchakato wa huo na hapo ndipo ilipozaliwa Ukawa na waje kumtumia leo?
Mwisho niwahusie wanasiasa hawa kina mtatiro wasiwe wanaisingizie Dola katika migogoro yao hususani idara ya usalama kwa kuwa tu idara hiyo haina desturi ya kujibu shutuma zozote wanazoshutumiwa na wanasiasa hao.
Idara ya Usalama kwa kushirikia na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vimekuwa chachu kubwa ya Aamani na utulivu tulionao leo, ambao nchi kadhaa duniani zinatamani kuwa Tanzaniaa yetu, ifikie hatua sasa wanasiasa waache kabisa kuzihusisha na migogoro yao vyombovyetu vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kutafuta umaarufu ambao usio na tija.
Hivi Mtatiro na wenzako mnatufanya wananchi watoto wadogo tusio na akili za timamu