Mtatiro hautabaki salama CUF Prof. Lipumba akiondoka!

Mtatiro hautabaki salama CUF Prof. Lipumba akiondoka!

Yaani kuna watu mishipa ya aibu ilishakatika kitambo sana,hivi huyu mzee na mbwembwe zake zote zile leo hiyo anathubutu kurudisha sura yake CUF?
Hakujiondoa CUF alijiuzuru uenyekiti.
 
Lipumba alishaacha cheo cha uenyekiti nini kimemfanya arudi tena?Lowasa alimfadhili kula kitu Kikwete akapata urais,mbona alimtosa EL?Kitwanga alimshawishi Magufulu kuchukua form ya urais,mbona magufuli kamtumbua uwaziri?
Huna hoja ya Mtatiro kumuita Lipumba msaliti ni kweli msaliti.Katikati ya vita unakimbia,vita imeisha na ushindi lukuki wa majimbo unarudi tena kambini.Kwa sisi wanajeshi Huyo process uchwara ni wa kunyongwa
[USER=206398]TataMadiba Ben Saanane[/USER]
Vita ipi? ya kumuingiza Lowasa ikulu?
 
Ok Lipumba amefanyia mamb mengi CUF, lakini kosa lake ni kujiuzulu kwenye uenyekiti licha ya kuombwa abaki na yeye kujiuzulu, tena kipindi cha uchaguzi halafu leo anataka kurudi tena kuwa mwenyekiti, angeacha na kuwa mwanachama wa kawaida kujitunzia heshima
Na CCM mbona mmevalia sana njuga hili suala la Lipumba na mnamuunga mkono kwa nguvu sana wakati hayo ni mambo ya CUF, kulikoni?
Kwa sasa ni wanachama wa CUF ndio wanamtaka...ngoja tuone kwa mujibu wa sharia na katiba ya CUF itakuwaje?
 
image.jpeg


ANDIKO MAKINI LA HABIBU MCHANGE.

Siasa bwana wakati mwengine hovyo kabisa.
Eti Leo JULIUSMTATIRO aliyechukuliwa na Lipumba baada ya kuhitimu UDSM na Hekaheka za serikali ya wanafunzi DARUSO na kutelekezwa na Mnyika na Chadema anamwita LIPUMBA msaliti!

..Duh kweli shikamoo Siasa,
Lipumba huyu huyu aliyempa Ukurugenzi wa sheria na haki za Binaadamu cheo kilichokuwa kikishikiliwa na Mbarala Maharagande Leo amemsaliti aliyemteua na kumpa mshahara kama njia ya kuwatia moyo vijana waliokuwa vyuoni wakifanya harakati.

Yaani #LIPUMBA aliyempa MTATIRO unaibu Katibu Mkuu wa CUF from nowhere akimtosa WILFRED LWAKATARE na kumpa muhitimu wa chuo kama chachu ya kuwatia vijana wengine Siasa bila kuwa na uzoefu wowote katika Siasa Leo amegeuka MSALITI mbele yake? ...

Kweli ukiwa unafanya Siasa uwe na ngozi ngumu aisee.
Ndio mana siasa inahusianishwa na uongo uongo na maneno mengi
Ukianza kuongea saaana unasmbiwa usilete siasa hapa. Ukiwa kigeugeu unaambiwa usilete siasa hapa.

Na Ndio mana naelewa Sasa kwanini Mtatiro aliweza kuandika makala tuliyoipenda Sana ya NJAAMPAKAmakanisani akiwalaumu viongozi wa Dini wanaopokea pesa za Lowassa lakini baadae akasimama kidete kumnadi huyo huyo Lowassa.

Nazidi kuelewa aisee. Siasa haihitaji uwe mkweli, ni kuongopa tu mwanzo mwisho ukisema ukweli inakula kwako.
Ni kama yule aliyewashauri watu wa Arusha wamzomee Lowassa kwa sababu ni Fisadi lakini alipohamia Chama chake akasimama kumnadi.

Ama yule mchungaji aliyesema "atakayemuunga mkono Lowassa akapimwe akili "...miezi michache baadae akawa mpiga debe wake Mkuu na fulana zenye picha yake akavaa.

Mwishowe watu wenye akili timamu watawadhalau wanasiasa kwa Unafiki wa namna hii.

Ndimi
Habib Mchange
 
Tena mnafiki sana
Na kwa taarifa yake
Hatakuja kuwa mbunge never
 
Yaani #LIPUMBA aliyempa MTATIRO unaibu Katibu Mkuu wa CUF from nowhere akimtosa WILFRED LWAKATARE na kumpa muhitimu wa chuo kama chachu ya kuwatia vijana wengine Siasa bila kuwa na uzoefu wowote katika Siasa Leo amegeuka MSALITI mbele yake? ...
Acha umbea bhana, alimpa kwani ni pipi? Acha siasa zako za kijinga
 
Huyu huyu habibu alie isaliti chadema ilio mlea leo anajiona bora kuliko mtatiro,mmmmhh kweli nyani haoni makalio yake
 
Ameshaingia kundini, ameng'atwa na 'vampire' kwa hiyo amekuwa mmoja wao. Hawezi kuyakumbuka tena alipotolewa.
 
Kweli siasa za Tanzania bila unafiki hutoboi.!
 
Mchange nae ataishia tu kuvaa matisheti ya ACT yani chama kama gereji bubu..akitoka ACT sijui ataenda wapi hadi huruma yani eti kisa Lipumba alimsaidia Mtatiro amtetee Lipumba anapoenda kinyume na chama..inabidi ajitafakari mara 2 mana yeye ndo anaonekana mnafiki
 
hahahahahah

aisee kumbe ACT na lipumba lenu moja?

hahahahahaha

Guys be a little bit serious ...ni chama gani makini kinaweza kuvumilia upuuzi aliofanya lipumba? Wanachama 476 wamemkataa na 14 wanamtaka
 
View attachment 385796

ANDIKO MAKINI LA HABIBU MCHANGE.

Siasa bwana wakati mwengine hovyo kabisa.
Eti Leo JULIUSMTATIRO aliyechukuliwa na Lipumba baada ya kuhitimu UDSM na Hekaheka za serikali ya wanafunzi DARUSO na kutelekezwa na Mnyika na Chadema anamwita LIPUMBA msaliti!

..Duh kweli shikamoo Siasa,
Lipumba huyu huyu aliyempa Ukurugenzi wa sheria na haki za Binaadamu cheo kilichokuwa kikishikiliwa na Mbarala Maharagande Leo amemsaliti aliyemteua na kumpa mshahara kama njia ya kuwatia moyo vijana waliokuwa vyuoni wakifanya harakati.

Yaani #LIPUMBA aliyempa MTATIRO unaibu Katibu Mkuu wa CUF from nowhere akimtosa WILFRED LWAKATARE na kumpa muhitimu wa chuo kama chachu ya kuwatia vijana wengine Siasa bila kuwa na uzoefu wowote katika Siasa Leo amegeuka MSALITI mbele yake? ...

Kweli ukiwa unafanya Siasa uwe na ngozi ngumu aisee.
Ndio mana siasa inahusianishwa na uongo uongo na maneno mengi
Ukianza kuongea saaana unasmbiwa usilete siasa hapa. Ukiwa kigeugeu unaambiwa usilete siasa hapa.

Na Ndio mana naelewa Sasa kwanini Mtatiro aliweza kuandika makala tuliyoipenda Sana ya NJAAMPAKAmakanisani akiwalaumu viongozi wa Dini wanaopokea pesa za Lowassa lakini baadae akasimama kidete kumnadi huyo huyo Lowassa.

Nazidi kuelewa aisee. Siasa haihitaji uwe mkweli, ni kuongopa tu mwanzo mwisho ukisema ukweli inakula kwako.
Ni kama yule aliyewashauri watu wa Arusha wamzomee Lowassa kwa sababu ni Fisadi lakini alipohamia Chama chake akasimama kumnadi.

Ama yule mchungaji aliyesema "atakayemuunga mkono Lowassa akapimwe akili "...miezi michache baadae akawa mpiga debe wake Mkuu na fulana zenye picha yake akavaa.

Mwishowe watu wenye akili timamu watawadhalau wanasiasa kwa Unafiki wa namna hii.

Ndimi
Habib Mchange

Kwani USALITI maana yake ni ipi hasa? Unafanywa na watu gani? Haujui kuwa hata yule mwanamke uliyemtolea mahali na ukafunga naye ndoa ikiambatana na sherehe kubwa halafu ikaja kutokea ukamsaliti na huo utaitwa USALITI?
Huyo Mwandishi anapaswa kwanza akjifunze maana ya USALITI, siyo mnatuletea maandiko ya wato ambao ni narrow minded.
 
Kuna watu wanauelewa mdogo sana kwakweli,Watu wa namna ya Habibu ndiyo wanatuharibia hii nchi.

Kwahiyo Habibu alitaka kwakuwa Prof. alimpokea Mtatiro na kumpatia uongozi hata kama anafanya ujinga aendelee kumpigia magoti tu na kunyenyekea,huo ni ujinga.

Huyu Habibu naona ni mweupe sana kichwana!.
 
Wanasiasa wa Tanzania wote ni wanafiki na wachumia tumbo.....na wengine wanatafuta hizo nafasi za uongozi kwa manufaa yao na sio kwa maslahi ya umma......

Bado tuna safari ndefu sana kupata ukombozi kwani tuliowaamini na kuwapa dhamana ya kutukomboa kwanza wameamua kuyakomboa matumbo yao kwanza......

Unafiki umetamalaki kwenye ulingo wa siasa za nchi hii hata hajulikani yupi mkweli na yupi muongo kwani wote wanaongea lugha zinazofanana..........
 
Hajitambui huyu Mkuu, wanataka kumshambulia Mtatiro bila ya kuwepo sababu zozote zile za msingi. Lipumba ni msaliti tu na mganga njaa.

Acha umbea bhana, alimpa kwani ni pipi? Acha siasa zako za kijinga
 
Back
Top Bottom