Mtatiro ameokoa jahazi la tcd leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtatiro ameokoa jahazi la tcd leo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by marmoboy, Apr 16, 2011.

 1. m

  marmoboy Member

  #1
  Apr 16, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mjadala wa wazi wa katiba wa TCD uliokuwa uanze leo saa nne asubuhi na kurushwa live na ITV ulikwama.
  Washiriki wa mjadala walipofika walikuta lundo la polisi waliokuwa na maagizo ya kukataza kongamano hilo na mageti yote ya kuingia karimjee HALL yalizingirwa na polisi waliovaa sare na askari kanzu.
  Majira ya saa 2.00 asubuh alifika bwana kipeja ambaye ni ofisa wa programu za TCD akiambana na mkurugenzi wa kituo hicho bwana Loya,
  Matumaini ya washiriki yalianza kurudi baada ya ujio wao lakini yalitoweka pale walipochimbwa mkwara na OCD aliyekuwa akiongoza oparesheni komesha mjadala. OCD aliwapa barua kutoka kwa kova ikiwa na sababu za zuio la mjadala huo.
  1. Kuwa habari za kiintelijensia zinaonesha kutakuwa na uvunjifu wa amani.
  2. Kuwa TCD walipeleka taarifa polisi with shorter notice.
  3. Ujio wa rais wa somalia tanzania.
  4. Kuwa suala la katiba limeshamalizwa na bunge.
  Baada ya kupewa barua na maagizo hayo watendaji hao wa TCD walianza kunyong'onyea.
  Akatokea kamanda benson kigaila akakuta mambo magumu, akaingia kwenye gari na kuondoka na wadau wenzake.
  Ghafla akatokea FORMER UDSM PM and FORMER TAHLISO SECRETARY (Mtatiro) ambaye kwa sasa ni NAIBU KATIBU MKUU CUF.
  Mtatiro alianza kwa mkwara mzito na kuwataka washiriki wote wasitawanyike, askari kanzu walianza kumzingira lakini naye alikuwa na walinzi kadhaa, zikatokea purukushani kati ya walimzi hao na askari kanzu baadaye zikatulia.
  Baadaye mtatiro akatoa order magari yafunge barabara - ikafungwa na washiriki wa mjadala.
  Baadaye akampigia kova na IGP wakamuahidi kuwa suala hilo linashughulikiwa lakini wakamuomba awahamasishe washiriki waondoke na kuwa mjadala ufanyike jumamosi ijayo mtatiro akakataa,
  That guy is very strategic kwani alipowapigia simu wakubwa aliweka loud speaker na washiriki walisikia nadhani ile ilizidi kuwachanganya IGP na wenzie.
  Msimamo wa mtatiro ukawa tofauti na ule wa watendaji wa TCD ambao walishawashawishi washiriki kuondoka baada ya mkwara wa polisi.
  Bahati nzuri washiriki wakamsikiliza zaidi mtatiro,wakafuata steps zake.
  Baadaye askari kanzu wakaanza kumzonga mtatiro kuwa eti yeye ndio anahatarisha amani kwa kuwa TCD wamekubali mjadala uahirishwe, mtatiro akawaruka mita mia na bila kumumunya maneno akawaeleza kuwa PATACHIMBIKA wakimtishia, wakati mtatiro alisikika akiwapigia wahariri wa vyombo vya habari - baada ya nusu saa TV na magazeti zikasheheni, ngoma ikaanza kuwa hatari kama movie vile.
  Ghafla akaingia yule Prof Lipumba - mwenyekiti wa TCD.
  Lipumba akafika na msimamo mkali kuliko OSAMA, mkurugenzi wa TCD akafokewa kwa nini hakuwa na msimamo, Lipumba akawa ngangari
  kinoma ngoma ndio ikawa mbichi zaidi pale ambapo lipumba aliwasiliana na kova na mwema kwa simu, kova alipewa maneno mazito mno na lipumba akamwambia kama mjadala haufanyiki atajua kama kova yuko juu ya katiba,
  Hoja kubwa ya lipumba ilikuwa kwamba mijadala ya ndani ya ukumbi haitolewi taarifa polisi na kuwa polisi hawana mandate ya kuzuia au kuingilia kwa vyovyote kongamano hilo.
  Baada ya kova akapandiwa igp mwema hewani, hoja za lipumba zikamshinda igp na mwisho kova akapigiwa simu na igp na kuamrishwa kufungia mageti na kuondoa polisi ili kongamano liendelee.
  Majira ya saa 5 na dakika kadhaa kova akampigia mtatiro na kumjulisha kuwa igp ameruhusu mjadala uendelee.
  Viongozi wengine wa nccr na chadema na cuf wakawa wameongezeka kongamano likaanza muda huohuo.
  Baadaye ITV wakafika majira ya saa
  6.30 wakafunga mitambo yao na kurusha LIVE mjadala kuanzia saa 7 mchana.
  Washiriki walikuwa kama mia mbili hivi na mgeni rasmi alikuwa jaji warioba.
  Wachangiaji wa jumla kutoka katika vyama walikuwa;
  CDM - BENSON(alirudi baadaye),
  Cuf - Mtatiro,
  Nccr - Dr mvungi,
  LHRC na taasisi zingine walikuwepo.
  Zomea zomea ilitaka kuanza pale mabapo mchngaji temba (kada wa ccm) alipotaka kujivua magamba hadharani - lipumba akamnusuru.
  Kwa faida ya wale wasiofahamu TCD - TANZANIA CENTER FOR DEMOCRACY(KITUO CHA DEMOKRASIA TANZANIA) - Ni taasisi inayoundwa na vyama vyenye wabunge yaani CCM, CDM, CUF,NCCR,TLP na UDP.
  Taarifa zaidi zipateni kupitia TV leo jioni na hasa MLIMANI TV waliokuwepo tangu asubuhi sana.
  Nawasilisha.


  ,  .
   
 2. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Still long way to go..............


  50 yrs of independence but i dare to say "Not Yet Uhuru"

  Eti bunge limefunga mjadala wa katiba?? Au mimi nakosea maana nakumbuka kama nimesikia urejeshwe kwa wananchi ujadiliwe tena

  Au kwa serikali ya CCM wananchi ni wakina nani hao? Ni wale wa kule Ikungulyabashashi na Kinyanambwa B peke yao na sio wana-UDASA, TCD, CDM, CUF and the likes?


  Hakuna serikali iliyochoka kama iliyowachoka wananchi wake..............na hizi intelijensia zao kuna siku tutazigeuza INTELIJINSIA
   
 3. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Crap.
  Crap
   
 4. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Kumbe ndo sababu ya kukosekana umeme ktk maeneo mengi ya Dar kwa muda huo!! Duh serikali inaenda puta sasa. Hakyamungu!
   
 5. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wapambanaji nawapa hongera..
   
 6. K

  Kivia JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 278
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Bila jino kwa jino mambo hayaendi kwani polisi wote wana kadi za CCM.
   
 7. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mchaka mchaka...chinja,

  Aliselema aleeja, taratibu tutafika tu.
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Dah.hawa mbwa hawa........yaani kila sehemu wanataka kujifanya bila wao mambo hayaendi,haya sasa mjadala imefanyika,kikowapi KOVA.......muangalie kwanza.....
   
 9. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #9
  Apr 16, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Umenikumbusha enzi hizo primary, basi kama kiranja ni mnoko, e bwana anakuchapa, na lazima ukae kwenye mstari!! ahahahah
   
 10. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #10
  Apr 16, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Na laiti kaa pangekuwa na UMIMI hapo au kuitana yale majina tuliyozoea...kusingekuwa na mkutano!! aka kongamano sijui!!
  ni baadhi ya mfano tu.. bali kuna safari ndefu ya kwenda!
   
 11. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #11
  Apr 16, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  We marmoboy, hiyo title yako irekebishe, Mtatiro hajasaidia chochote ama we ndio mke wake
   
 12. mooduke

  mooduke JF-Expert Member

  #12
  Apr 16, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Mpaka kieleweke tunashukuru kwa taarifa mdau....

   
 13. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #13
  Apr 16, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Polisi wetu nao ni shida kweli yaani kila kitu ni kibali!
   
 14. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #14
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  CCM B walikuwa wanazuga tu hamna jipya hapo
   
 15. Painstruth

  Painstruth Member

  #15
  Apr 17, 2011
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duh!vvvvvvvvvvvvvvvvvv
   
 16. U

  Uswe JF-Expert Member

  #16
  Apr 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  kitufe cha thenki you kiko wapi?
   
 17. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #17
  Apr 17, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  intelejesia hadi kwenye makongamano hihatali jee? Wanashindwaje? Kwamafisadi wanaona tuu maandamano yaamani na makongamano mumezeekavibaya
   
Loading...