Mtatiro aishambulia Chadema Igunga

mtatiro aache kutumia masaburi kufikiri ajaribu kutumia na kichwa kidogo!
 
Chadema kwanini wanakwenda kwenye majukwa kusema CUF CCM B wao waendelee kunadii sera zao za kumwagia watu tindikali na kuwavuwa hijabu, Tayari Ulamaa wa Kiislamu wamewataka wawaombe radhi mnakakiwa kuwa makini kwa kuwaeleza ukweli sio kutumia siasa rahisi zitakija kuwagharimu baadae hizo jamaa zangu wa kilimanjaro
 
CDM hakina wanachama ilakina wafuasi na wa fuasi hawa wakonchi nzima .....ukitaka ushahidi nenda igunga kaulize upinzani wanaopata CCM to CDM ulitegemewa? na rekodi ya CDM ikoje katikajimbo hilo wakat iwa uchaguzi 2010? Utapata jibu sahihi ambalo nikwamba mtu yeyote asiyependa maovu ana itikadi ya CDM wala hahitaji kuwana kadi......na hii ukitaka kupata uhakika kaulize wenye akili kwanini siri za serikali zina vuja namna hii? na kwa nini siri za CCM wenyewe zinavuja namna hii?....

Utapata majibu mazuri kuwa kisiasa Tanzania tupo safi.......watanzania watakuwa namadaraka makubwa kuliko vyama kwasababu hiyo kukikataa chama kinachofanya vibaya itakuwa rahisi kuliko ilivyokuwa zamani .......

People's Power....
 
Mtatiro siku hizi ameishusha profile yake sana. sio yule aliyekua mjenga hoja siku za nyuma. naona kazi ni kupiga majungu tuu
 
hoja kukubalika au kusema uongo mbele ya Watanzania tujaribu kusema kweli uchguzi wa Igunga tutaona kama CDM kama kumwagia watu tindikali au mumvua Fatma Kimario hijabu ndio kushinda hayaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
 

Ugawaji wa viti maalum vya CUF mbona nao umependelea Zanzibar? Hapa inaonyesha Zanzibar wana viti vitatu wakati idadi ya watu kule ni dongo sana kulinganisha na Tanzania Bara. Je hapo kuna uwakilishi sawa wa wananchi?
 

Duh! hivi ni kweli huyu mgombea wa CDM alijitoa baada ya kupokea mlungula kutoka RA akabaki mahona pekee katika uchaguzi uliopita?

If this allegation were true cdm ni wanafiki sana
 
Hata kama ukikataa, ukweli ukisimama uongo hujitenga na mwenye macho haambiwi tazama. cuf na magamba ni wanandoa. Hili halina ubishi. Halafu gazeti la majira, uhuru, na yale mengine what do you expect??
Nalisikitiki sana majira jinsi lilivyokwisha toka hero to ziro pia namsikitikia sana Mtatilo safari yake kisiasa ni fupi sana,jamaa sijui huwa hawazi kwenda kwenye chama kilichofika mwisho? sidhani kama elimu yake inampa uwezo wa kufikiri
 
Mkuu mimi kuwahabarisha wanajamvi imekuwa kosa? Sikutaka kuedit chochote ili wanajamvi mumfahamu Mtatiro rangi zake zote

Pole sana, ukikubali kubeba mzigo wa bangi ukubali kushtakiwa nao hata kama si wako, ushahidi wa kuwa wewe unausafirisha tu na mali yako hauna nguvu kabisa maana kukubali kuusafirisha ni kushiriki madhara ya bangi.


Na kama unakubali kubeba mzigo wa kinyesi kwa sababu ya kwenda kuubwaga sehemu pia ukubali kunuka kinyesi.
 
We mtatiro weweee acha usharobalo.. Kwanza huwa hakuna tanzania zanzibar, bali taifa la zanzibar.
Hiyo mikoa Tanzania umetaja wabunge 4 tu. Taifa la Zanzibar umetaja wabumbe 3.
Sasa 3 + 4 = 7. Hao wengine watatu ni wawapi?
Nchi ya Zanzibar ina 984 sq km, ambayo ni ndogo mara 19 kwa mkoa wa Mwanza pekee wenye 19,592 sq km
Nchi ya Tanzania ina
946,316 sq km;
Mtatiro twambie mlitumia vigezo gani kutujanzia Wanzanzibar kwenye bunge letu la Tanzania wakati kanda ya ziwa peke yake mmeweka mbunge 1 ??????????
 

Hebu vigezo walivyotumia cdm kuweka mke Slaa na wachaga wenzao kuwa wabunge wa viti maalum?
 
vipi wao si waligawana baada ya uchaguzi kwa makubaliano na ccm
 
hivi chadema wangepata viti zanzibar wangekataa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ?

wanajua kuwa uundwaji wa serikali ni utashi wa kikatiba baada ya kura ya maoni, kwa hio zanzibar wanafata matashi ya wananchi. na sio mkataba wa cuf na ccm
 
Uongo wako ndio hapo unapoingia utata mkubwa... Chadema ina wabunge 22 wa majimbo + 36 wanakuwa 58..!!. Aksante...

WanaJF tuendelee kuyapuuza haya magazeti uchwara kama Majira na huyu aliepost pia
eliesikia, mbona unakuwa kama asiesikia?!. Mbona alichosema Mtatiro ndicho ulichosema wewe, hoja ilihusu wabunge 36 wa kuteuliwa, hao 22 wa kuchaguliwa umewaleta wa nini?. na jumla ya wabunge wote 58 wa Chadema umewataja wanahusu nini kwenye hoja ya msingi?.

Japo siwashabikii CUF kwa sababu watagawana kura na Chadema katika vita vya panzi, hivyo faida ni kwa CCM, ila Mtatiro ana hoja ya msingi, kama ni kweli kati ya viti hiyo maalum 36, 16 wamepewa wana Kilimanjaro, then its obvious ni tatizo. Tatizo la manazi wa Chadema humu jamvini, mnajiaminisha chama chenu ni chama malaika wakati ni chama cha siasa kama vingine japo kimeleta tumaini jipya.

Mimi binafsi nilishawa wahi kuyataja baadhi ya maeneo yenye matatizo kwa Chadema, niliishia kutukanwa!. Kama ukiujua ukweli kuwa issue fulani ni tatizo na ukalisemea, hata ukibezwa haiwezi kukupa shida kwa sababu ukweli utasimama.

Kwa upande wa Mtatiro, kwanza mkubali msikubali ni mwanasiasa mzuri ila tatizo lake ni moja tuu, he is not very smart upstairs hivyo kujikuta anatumiwa tuu na CUF, ili kukifutia tuhuma za udini, alitakiwa amuulize Rwakatare. Kwa wale mliangalia kile kipindi cha Mchakato Majimboni, JJ.Mnyika alipoanza kampeni zake na kumaliza kazi pale pale, lazima mtakubaliana na mimi, Mtatiro ni mzuri kujieleza, ila siasa za sasa zinahitaji sio tuu uwezo wa kujieleza, bali pia inteligence na briliance upstais, vitu ambavyo Mtatiro hana!.

Sio haki kuliita majira ni gazeti uchwala unless unamaanisha gazeti makini ni Tanzania Daima pekee!, na pia sio busara kumpuuza kila anayepingana na Chadema humu jamvini, wapenzi na mashabiki wa Chadema msishabikie tuu ushabiki maandazi, kwa kumtukana kila anayetofautiana na Chadema humu jamvini, kama kuna hoja za msingi, jibuni hoja sio kuja na viroja!.

Pasco.
 
Hapa Mtatiro na mashaka na uwezo wake hivi hesabu ndogo 36+22= 48 kama kweli idadi hiyo aliyoitaja ni sawia mbona haelewi kuna idadi ya wabunge WCDM ni wakuchaguliwa 22 na idadi hiyo ya bungeni ni 48 sasa kwa akili ya matatiro hivi 48-22=36 Bila shaka Mtatiro akili yake imeanza kupoteza uelekeo.
 
hivi ni kweli kuwa cdm ni chama cha wachaga? nauliza maana hizi kashfa ni za muda sasa ni kweli wamegawana viti maalum vingi kwao? kama ni hivyo basi tuendako yatatokea matatizo makubwa kuliko yaliyopo sasa
<br />
<br />
Hata kama wabunge wote wakiwa wachaga,maadam wamechaguliwa na wananchi sioni tatizo.Je ni kweli wabunge wote CDM ni wachaga?Ukwel unaujua mwenyewe.
 
<br />
<br />
Well said mkuu,ila sina hakika na hiyo idadi ya wabunge 16.Je,hiyo ni idadi ya wachaga waliopewa viti maalum au ni idadi ya wawakilishi wa mkoa wa kilimanjaro.Kuna uwezekano mbunge akawa toka KLM lakini si muwakilishi wa KLM.Kama kuna mwenye kuwajua wabunge hao 16 hembu atupatie ili tuchambue vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…