Uchaguzi 2020 MTANZIKO CCM: Hivi watachagua CHAMA ama watachagua mtu?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,796
CCM kama chama dola 2015 kilikuwa na hali mbaya sana...na upinzani chini ya muungano wa UKAWA ukaonekana tishio kubwa la kuimaliza na kuizika kabisa CCM kwenye ulingo wa siasa na kuwa chama dola

Karata ya kuleta mgombea aliyeonekana kuwa na nafuu kuliko wengine kuliipa CCM nafuu kubwa sana....Kwahiyo kuelekea kwenye kampeni za uchaguzi mkuu mwaka huo ile slogan maarufu ya CHAGUA CCCM...ikafa rasmi na badala yake ikawa CHAGUA MGOMBEA tajwa...!!!

Kwa mara ya kwanza chama dola kikawa na mgombea binafsi ndani ya chama mgombea binafsi ndani ya chama akawa binafsi hata baada ya uchaguzi.

Kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu chama huongozwa na ILANI ITIKADI NA SERA..Na hizi ndio huwa mrejesho wa kuomba ridhaa tena uchaguzi unaofuata kwa kuonesha mmetekeleza vipi ilani ya chama, mmesimamia vipi itikadi yenu na mmetafsiri vipi sera zenu...

Kwenye hili CCM kamwe hawawezi kukujibu kwa mfano kwenye ilani yao ya 2015-2020 ....Mojawapo wa jambo walilopanga ni kuwawezesha watu wa kusini kujenga reli mpaka Mbamba bay...matarajio ilikuwa ni kufungua milango ya bishara kwa wepesi wa kusafirisha mizigo mpaka bandari ya Mtwara yenye kina kirefu cha asili ambapo ingekuwa nia gateway mzuri kuelekea Msumbiji Zambia na kwingineko.

Mgombea binafsi ndani ya chama aliitupa chini na kuisigina ILANI yote na kutenda kinyume kabisa...Akafanya ambayo hayakuwa kabisa kwenye ilani kama Stigler's gorge project, SGR ,Ndege nknk...

Mara tu baada ya kushika hatamu za chama na serikali mgombea binafsi ndani ya chama akaanza na tumbuatumbua..hii ilionekana machoni pa wengi kama jambo jema..lakini lilikuwa na ajenda ya siri nyuma yake..kuwapa ajira watu wapya chini yake nknk

Tumbuatumbua na vyeti bandia vilileta madhila kwa familia nyingi...wengi kwa maelfu waliotumikia taifa kwa muda mrefu haki zao zilipokwa na zoezi la vyeti feki

Ajira zisizo rasmi na bila utaratibu zikawa nyingi...miradi mikubwa nje ya ilani ya chama na bila bajeti ikawa mingi...tukafika mahali pesa ikawa haitoshi..kilichotokea kwa wafanyabiashara kubwa kati na ndogo kinajulikana...ikawa ni kupigwa kodi kwa kwenda mbele

Mgandamizo wa kutaka mambo yaende yote kwa pamoja na bila fungu la kutosha vikamfanya kiongozi mkuu apate stress na kuanza kuwajibu wananchi vibaya badala ya kutengeneza akazidi kuharibu

Sasa ni wakati wa uchaguzi mwingine wananchi walisubiri kusikia ILANI ya chama imetekezwaje!? Changamoto ni zipi!? Tumetoka wapi tuko wapi na tunaenda wapi!? Kilichotokea kwenye kwenye uzinduzi wa kampeni sio mrejesho wa ILANI bali ni mrejesho wa ahadi binafsi na matarajio ya kujenga uwanja mpya wa michezo na kuongeza ndege!!!

Mwisho wa uzinduzi wa kampeni ikaonesha wazi chama hakikubaliki bado na mgombea binafsi ndani ya chama hana ILANI SERA WALA ITIKADI.

Wanachama wamebaki njiapanda ...hawajui wachague nini....!!!
 
Jawabu wanalo wajumbe,ila kukusaidia huku mitaani CCM haipo,wananchi wanajua wapi mwaka huu wanazipelekesha kura zao,mambo ya kumrudisha Sultani akiwachapisha bakora hazarani,wameshaisoma namba.

Wamekwisha kuhisi wakiirudisha CCM kwenye ufalme badala ya wanafunzi na raia kuchapwa bakora sasa itakuwa ni adhabu kwa nchi nzima kuchapwa vibiko hadharani vigogo wakichekelea kuwa ni jambo la kawaida.
 
Hakuna cha chama na mtu, ubabe tu bora liende.PM ana sababu gani kuteka ,kutesa wapinzani wake apite bila kupigwa!? Kiongozi mkuu, anahubiri ubaguzi maendeleo, rejea eti Bunda hakuna taa, barabara pia ya lami iliishia jimboni kwa Lugola, dharau kwa watumishi, biashara zimedumaa na kufa, huduma za afya umma bora liende huna pesa wewe kufa na maiti utailipia, nani anafuraha na utawala huu!??
 
Back
Top Bottom