Uchaguzi 2020 Mtanzania tumia haki yako 28, Oktoba 2020

Mjasi1

Member
Sep 1, 2020
68
25
TUMIA HAKI YAKO YA KIKATIBA

Tarehe 28 Mwezi October 2020 ni siku muhimu kwa kila Mtanzania kwanini inakuwa ni siku muhimu? Ndio siku pekee ambayo inaendakuleta mabadiliko kwa Mtanzania kwakuchagua kiongozi atakayeona anafaa katika mustakhabali wa kuongoza Taifa, Jimbo hadi Kata . Pasipo ushiriki wa mtanzania ni wazi kuna kupatikana kiongozi usiye muhitaji .Kura yako inaweza kuleta mabadiriko chanya au hasi katika maisha yako kama utaitumia vizuri.

Pengine, inaweza ikawa siku inayochukuliwa ukawaida kwa wengine katika jamii zetu kuna athari zinazotokana na kutoshiriki kikamilifu katika kampeni za uchaguzi na kupiga kura. Kwanza nikupoteza haki yako kikatiba lakini huwezi kupata kiongozi yule unae muhitaji yamkini wengine hawana mlengo wowote wa vyama vya siasa lakini haikuondolei haki yako ya kumchaguwa yule unae muona anafaa kuwa kiongozi wako.

Kura ya mtanzania mmoja inathamani kubwa katika hatima ya kuamua kiongozi umtakae , ukweli nikwamba tunahitaji viongozi katika Kata zetu hadi Majimboni mwetu na Taifa letu. Tusije kulalamika bila ya kushiriki, muda wetu ndio sasa watanznia kutumia haki hii kikatiba kuchaguwa viongozi ambao tunahisi wanaweza kuleta maendeleo katika jamii zetu.Chonde chonde ewe baba,mama,Mjomba ,shangazi,kaka na dada uliye jiamdikisha katika daftari la kupiga kura tarehe 28 October twende kuchaguwa watu tuwatakao katika nafasi za Uongozi.

Hatuwezi kupiga kura pakee bila ya kusikiliza sera zinazonadiwa na wagombea wa nafasi hizo kutoka katika vyama mbalimbali vya siasa.Twende katika mikutano ya hadhara haijarishi una mlengo wa chama chochote au huna jambo lililojema nikusikiliza sera na kuzichuja ilikupata picha halisi ya vipaumbele vinavyotolewa kama vitakidhi kile unacho kihitaji kama mwananchi katika jamii yako . shime kijana, shime mtanzania tuinuke sasa wakati wetu ndio huu wakupata viongozi tunao wakusudia.KURA YAKO, SAUTI YAKO .Tarehe 28 Oktober si ya kukosa.

Makala kuelekea uchaguzi mkuu na Phabian Isaya.

Email:msangifabian@gmail.com,
 
Back
Top Bottom