Tetesi: Mtanzania Mbaroni Kwa kuiibia Serikali ya Marekani Bilioni 8!

  • Thread starter Kanungila Karim
  • Start date

Kanungila Karim

Kanungila Karim

Verified Member
Joined
Apr 29, 2016
Messages
5,023
Likes
4,503
Points
280
Age
22
Kanungila Karim

Kanungila Karim

Verified Member
Joined Apr 29, 2016
5,023 4,503 280
JohnNdungurumedicaidbillingarrest1.jpgMTANZANIA JOHN NDUNGURU, anayemiliki kampuni ya Mercy Services of Heath inayojishughulisha na kazi ya kuhudumia wagonjwa majumbani (Home Health Care) nchini Marekani, ametiwa mbaroni nchini humo na kufunguliwa mashitaka 12 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.


Kwa mujibu wa mtandao wa NBCWASHINGTON.COM, ulioandika habari hiyo Desemba 3 mwaka huu, Ndunguru anadaiwa kujipatia kiasi cha dola za Marekani milioni 3.6 (T.shs Bilioni 8) baada ya kuandika nyaraka za madai ya uongo akionesha kuidai serikali ya jimbo la Virginia kiasi hicho akionesha kampuni yake kuhudumia wagonjwa wapatao 59.


Tukio hilo limetokea wakati Jimbo la Virginia linajitayarisha kupanua mpango wa msaada wa tiba na hati za mahakama zinaonyesha kwamba idara inayoshughulikia huduma za tiba tayari imelipa Dola mil. 3.6 kwa kampuni ya Ndunguru.


Trina Greene, ambaye ni meneja katika kampuni hiyo, alisema wafanyakazi walishtushwa na habari hizo, lakini bado wako bega kwa bega na mkuu wao ambaye humwita Dr. John.

Green na wafanyakazi wengine walianza kuhisi dadlili za matatizo wiki iliyopita wakati ofisi yao ilipovamiwa na wapelelezi kutoka ofisi ya mwanasheria mkuu ambapo kompyuta 10 zilichukuliwa pamoja na masanduku 33 ya hati mbalimbali.


Hati za mahakama zinadai kwamba kulikuwa na saini ya daktari mmoja iliyoghushiwa na rekodi za watu kadhaa waliopata huduma hapo hazionekani zilipo.


Kampuni hiyo hutoa huduma kwa watu wapatao 90 na imeajiri wafanyakazi wapatao 100.


Ndunguru yuko rumande nchini Marekani baada ya kukosa dhamana.
 
Two dimension array

Two dimension array

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Messages
986
Likes
1,171
Points
180
Two dimension array

Two dimension array

JF-Expert Member
Joined Jul 25, 2018
986 1,171 180
Ok vzr sana......kazi na bata
 
Saint anne

Saint anne

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2018
Messages
275
Likes
202
Points
60
Saint anne

Saint anne

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2018
275 202 60
Ety ndo kidume,,,hahahaha..mkamsaidie Basi atoke salama
 
T

The Elephant

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2014
Messages
3,128
Likes
1,820
Points
280
T

The Elephant

JF-Expert Member
Joined Dec 18, 2014
3,128 1,820 280
Huo utaratibu hata huku kwetu haufai siku hizi

wale wafanyabiashara wa mafuta, sukari, chumvi ambao wamekuwa kama wachina wakiwa na viwanda vidogo vidogo ndani wakitengeneza mifuko bandia za kampuni mbali mbali za sukari kama Kagera na mtibwa sugar wenyewe wanasoma namba ndani

Mfuko wa sukari kilo 50 unakuta kilo 45, na 25 Kgs unakuta 23Kgs

Mafuta lita 20 utakuta lita 17.
 

Forum statistics

Threads 1,238,107
Members 475,830
Posts 29,311,026