Mtanzania ijue vizuri Escrow

Mtanzania ijue vizuri Escrow

Mbona mie sijaielewa escrow maana yake nini?
Nimeona uchambuzi wa kipuuzi tu na utetezi usio na sifa na sifa za kijinga eti azidi kuwaongoza maskini ambao sijakua ni wa kipato au akili kama za kwako na pia kiwalaumu na kuwaponda waliothubutu angalao kukufichulia uliyokuwa huyajui.
Siku nyingine jifunze namna ya kujenga hoja yenye mashiko vinginevyo nawe umetumwa kumsafisha mmoja wao kwani miradi ya kusafishana ni dili hapa bongo. Umeahidiwa ngapi manake naona ccm nayo unainadi? Pathetic!
utaelewaje wakati ulishakabidhi kichwa chako kwa ZITTO, LISSU NA KAFULILA
 
Kitabu kitakatifu ni kimoja tu. Kingine hicho ni shetani kujigeuza na kuwa mfano wa malaika wa nuru ambayo ndivyo alivyo!.

Mungu aligeuze fimbo ya Musa ikawa nyoka, shetani naye akawatumia wachawi wake kugeuza fimbo zao kuwa nyoka. Hata hivyo nyoka wa Fimbo ya Musa, ulimeza nyoka wote wa wachawi.

Nakuja.
kitabu gani ni cha kitakatifu pekee?
 
Hapa topic ni Ruge, Escrow na Singa,
Kuna Jukwaa la Dini kule chini, kama huna access waombe mods wakujumuishe huko

Mwambie aliyeanzisha mada, asiseme habari za Utakatifu kama ni hivyo. Maana amesema vitabu vitakatifu, nan nikaona nimweke sawa tu kwa kuwa aliskosea spelling. BAdala yake aseme kitabu kitakatifu kwa kuwa kiko kimoja tu duniani na wala si zaidi. Hivyo alitakiwa kuandika KITABU KITAKATIFU NA SI VITABU VITAKATIFU KWA KUWA SIYO VINGI NI KIMOJA TU.
 
MTANZANIA MWENZANGU IJUE VIZURI ( ESCROW)

Ndugu zangu watanzania napenda nichukue fursa hii niwakumbushe machache kuhusu hili sakata la Escrow maana tumedanganywa sana sasa tuseme inatosha maana ata vitabu vitakatifu vinaeleza bayana kwamba watu wangu wemeangamia kwa kukosa maarifa

Ndugu zangu ninavyojua bwana Rugemalira alikua mtanzania pekee aliyekua na haki katika fedha za Tegeta Escrow Kama mmiliki wa asilimia 30% za IPTL.

Akashawishiwa na serkali kumuuzia bwana Singa Singa kwa madai ya serkali ya awamu ya nne kwamba Singasinga ni mwekezaji mkubwa ataboresha mtambo, Rugemalira akakubali akamuuzia kwa makubaliano waliyofikia ya dola 75 million

Bwana Rugemalira akalipwa asilimia 10% na kuendelea kuisubiria asilimia yake 90% katika siku 60 kwa mjibu wa mkataba .

Cha ajabu sasa!!! Singasinga na washirika wake walikua hawana nia njema na Rugemalira na wala hawakua na mpango wa kumlipa hiyo asilimia 90% walichokua wanahitaji ni kumtumia Rugemalira kuzifikia pesa pale Bank kuu (B.O.T)

Kibaya zaidi Rugemalira anasubiria kulipwa pesa zake kumbe watu washabeba hizo pesa kutoka Bank kuu na kugawana wakiwa na mikokoteni, rumbesa na vifurushi pale STANBIC bank mimi nawewe tujiulize hii bank mbona watu hawaizungumzii na waliochukua pesa kwa mikokoteni, rumbesa n.k hawatajwi Zitto, Lissu na kafulila watwambie

Rugemalira kuona hivyo ndo akaamua kwenda mahakamani kushitaki nakumbuka aliwashitaki wafuatao:-
1. Gavana wa Bank kuu kwa kuruhusu kutoa pesa hizo
2.PAP
3.STANBIC kwa kupokea fedha hizo na
4.Bank moja ya wapakistani iliyopokea kiasi fulani Cha fedha hizo za Escrow

Hapa sasa ndugu zangu ndo kimbembe, fitini na paniki dhidi ya bwana Rugemalira kuona anaendelea kupambana kupata haki yake ndo zilianza, watu wakatengeneza chuki dhidi yake inasemekana walishirika wa singasinga walikataa kumlipa bwana Rugemalira na kupanga kumuondoa kwa njia nyingine wajuazo wao.

Lakini inasemekana Gavana wa benki akaogopa sana na kusema hawafikii popote na hiyo GRAND FRAUD kwa hiyo ni bora wakubaliane kumlipa Rugemalira haki yake ili mambo yaishie hapo.

Na ndo hivyo Rugemalira alivyolipwa fedha zake kwa amri ya mahakama ya tarehe 17/ 01/ 2014 ambayo hadi sasa imefichwa kwa siri kubwa je!! ?? Zitto kabwe na Lissu hawajui hili Mimi na wewe tujiulize na tutafakari kwa kina!!!??

Na katika hiyo furaha ya kupata fedha zake kutoka mikononi mwa wanyanganyi Rugemalira akaamua kutoa sadaka na mgao kwa watu mbali mbali wakiwemo viongozi wa serkali na dini akiwataka wafungue akauti benki ya mukombozi inayomilikiwa na kanisa katoliki je kuna kosa gani apo na pesa amepewa kwa amri ya mahakama kwa tafsiri nzuri hiyo pesa ni Mali yake.

Kibaya ni pale wanaoujua ukweli huu wanaamua kudanganya watanzania kwa kujipambanua na kusema waliopewe pesa na bwana Rugemalira ndio wezi kumbe waongo na wazandiki ukweli wanaujua na ndo maana Zitto alikataa kutia sahihi kwenye ripoti iliyowasilishwa bungeni na kamati sasa kwa nini asemi ukwelii!!! Mimi na wewe tujiulize!!??

Sasa hii ndo ngumu kumeza naomba Zitto na Lissu watutajie waliochukua fedha benki kuu na kugawana pale STANBIC wakibeba hizo pesa kwenye mikokoteni, rumbesa, vifurushi n.k ni akina nani hao tuwajue!!??

Vile vile niwape angalizo watanzania magazeti yasitupotoshe kazi kubwa kuandika waliopewa mgao na Rugemalira hii inaonesha watu waliohusika na kukwapua hizo pesa Bank kuu na kugawana pale STANBIC wanaendelea kujificha na kuhonga magazeti ili yaendelee kutupotosha watanzania alafu kwanini hii Bank ya STANBIC watu hawaizungumzii wakati hii benki ndo imehusika kutorosha pesa kutoka Bank kuu( B.O.T)

Mwisho nipende kumpogeza Raisi wetu kipenzi Cha watanzania hasa sisi maskini JPM kwa hizi hatua anazozichukua tunamshukru Mungu kwamba kupitia yeye tutayajua mengi na bahati nzuri JPM nimpenda haki sana na mwenye hofu na Mungu, Lissu anayejifanya kupinga kila kitu na kujiona yeye ndo mjuzi wa kila jambo mimi nasema kwa serkali hii tukufu atachelewa sana na unafiki wao ndo umefika mwisho hatudanyanyiki tena wanajifanya wanaguswa sana na hili swala kumbe nia yao ni kutupotosha watanzania

Mungu ibariki nchi yetu Tanzania
Mungu mbariki Raisi wetu JPM
Niwatakie siku njema
Magufuli Captain ( CCM mpya)
Acha kumuingiza mheshimiwa raisi /mwenyekiti wa CCM,kama unampenda Rugemalira don uchwara kampikie chai,hapa ni KAZI TU,Matapeli wa kimataifa kama Rugemalira hatuwashobokei,hata kidogo wametuumiza sana kwa dili zao za lumbesa ,umeme umekuwa anasa kwetu sababu yao,sasa bado Richmond,mitapeli yote kiama chao ki njiani.Kwanza wewe ndio unataka kutupotosha,swala lipo mahakamani kaka kwa hiyo hizo ngonjera zako ni sawa na kutupotezea muda hapa JF ,maelezo mengi ili umsafishe Rugemalira,bila shaka wewe ni mnufaika wa lumbesa na viroba kutoka pale Mkombozi
 
Cheo cha juu katika kusoma ni profesa, ukipata uprof inamaana umepanda katika kilele cha ilmu. Nataka kujua cheo apewacho mtu wakati elimu yake inashuka kutoka kileleni kurudi chini.


Na washawasha!
 
Mtu anaweza kutoa sadaka kwa pesa zote hizo kwa viongozi wa serikali ? hapo ni rushwa imetembea ila haijulikani kwa nini au yalikuwa ni malipo ya kusaidiwa kufisadi siku za nyuma.
Mtu tajiri anataka kutoa sadaka atatoa kwa taasisi au atajenga miradi inayosaidia watu wasiojiweza sio kutoa mamilioni kwa viongozi wa serikali.
Mtu hawezi tu kukupa pesa zote hizo zawadi - hapo tusifunikwe na pazia la ujinga wa kitoto.
 
utaelewaje wakati ulishakabidhi kichwa chako kwa ZITTO, LISSU NA KAFULILA
Njaa mbaya! Sasa huyo babu mnayemtetea hhumu ilihali kawapiga tangu ianze iptl, mtakuwa mnafikiri kwa makalio yenu zaidi! Ccm bwana, ni wapiga dili mfanoe haupo!
 
naomba Zitto na Lissu watutajie waliochukua fedha benki kuu na kugawana pale STANBIC wakibeba hizo pesa kwenye mikokoteni, rumbesa, vifurushi n.k ni akina nani hao tuwajue!!??

How come Zitto na Lissu ndo wataje? Awataje yule mwenye ''uchungu na rasilimali za Taifa'' kama kweli ana nia ya dhati ya kufukua kaburi lile. Yale majina ni top secret na inasemekana hata CCTV camera zilizimwa ile siku ili wazee wagawane vyao kwa raha mustarehe. Hata kama Lissu aliyapata majina yale, akiyataja hakuna atakayemuamini.
 
Mi hata sielewi. Vyovyote mtakavyoamua nipo nyuma yenu
 
Back
Top Bottom