Nadhani bado hujapata kifungua kinywa mama! Hapo ni kuonyesha watu wanajadiliana kutengana wakiwa bado wako chini ya mwamvuli wa muungano, je muungano ukivunjika si itakuwa balaa!?
JK kaleta mambo! Kila mtu sasa ni mzandiki! Yote kwa yote siyo mimi bali ni kauli za wapemba wenyewe! Waunguja nao wanalia nchi yao kuvamiwa na Wapemba!wwe ni muongo, mnafik, mzandik, hakuna sehmu yyote wapemba wanadai Pemba yao cku zote wapemba wamekuwa mstari wa mbele kuidai Zanzibar, wwe unachuki na wapemba kwa sababu waliodai hayo mamlaka ni waunguja badilisha kichwa cha habari kisomeke unguja wanataka mamlaka yao, kwa cc wazanzibar tunasema hao ni wahuni wa ccm na mamluki wa Tanganyika wala hawatupi shida kuelekea mamlaka kamili ya Zanzibar, wanataka kututoa nje ya mada but wamechelewa hzo ndo siasa za ccm zimepitwa na wakati waendelee kutoa povu lkini 2015 tunataka Tanganyika na Zanzibar zenye mamlaka kamili bila chama cha majambazi aka ccm inawezekana.
​Kwani hukuwahi msikia marehemu Nandonde akidai Mtwara kujitenga na kuungana na Msumbiji!Tusiendekeze upuuzi kama huu. Ni lazima tuelewe kwamba umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Tukiendekeza hili la leo, kesho na keshokutwa tutasikia Mbeya, Iringa, Rukwa na Ruvuma nao wanataka kujitenga na kudai uhuru kamili.
Wewe wacha uongo, ni wapi FaizaFoxy alipomtukana Nyerere? Mimi sikubaliani na mambo mengi sana ya Nyerere lakini siwezi kumtukana yeye wala wewe.
Akipingwa Nyerere nyinyi mnaona ni matusi? wacheni ulimbukeni.
Nyerere alikuwa binadamu kama wewe na mimi na yeye mwenyewe kakiri kuwa alikuwa na makosa na hakuwa malaika. Sasa wewe kama nani wa kuniona mimi nisiyekubaliana na siasa na utawala wake kuwa nnamtukana?
Hata hili mnaloliongelea la Pemba kakosea sana, soma vizuri wanavyoongea utajuwa kuwa hili linaongelewa ndani ya Muungano na kabla ya Muungano.
Ni kipi cha ajabu mnachokiona hapo? wakati hayo aliyosema Nyerere hakuyaota wala si ya ajabu yalikuwepo, Upemba na Uzanzibari haukuanza leo wala jana, ni asili. Kama mlikuwa hamjui muelewe hayo.
Wala hakuna cha maana isipokuwa inadhihirisha kuwa Nyerere hakuwa na muono, anasema nje ya muungano wakati hayo yanaongelewa ndani ya muungano, huo muono uko wapi hapo?
Mimi nadhani haya yamepitwa na wakati tunatakiwa tukae tujenge taifa letu siku zote wosia wa baba na mama ni muhimu katika familia hivo WOSIA WA NYERERE NA MZEE KARUME Ni MUHIMU
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Let Zanzibar Go, Tumechoka na Vitimbwi Vyao, tuachane nao na tujenge Tanganyika yetu.
Historia inaonesha kuwa Tanganyika hatujawahi kuwa na Ubaguzi kabla na hata Baada ya Uhuru na Muungano.
Wewe ndiyo unaleta utani!. Mwl. Nyerere kwenye swala la Zanzibar kujitenga hakujenga hoja kwa kuona mbali, bali alitumia historia kwa njia ambao ionekane kama anajenga hoja kwa kuona mbali wakati alichokuwa anafanya ni ku-rewind historia na kumbusha tu ambao hawakuijua au waliosahau.
Ukisoma vizuri hii article atagundua kuwa matatizo yalikuwepo na yaliendelea kuwepo chni ya kapeti kwa vile kuyatoa nje ni kupambana na kosa la uhaini ndani ya katiba ya nchi. Kamuulize Mzee Aboud Jumbe na Maalim Seif Shalif Hamad watakueleza nini maana ya hiki ninachokisema
Tusipende kutoa sifa na pongezi kwenye jambo ambalo halistahili.
Ni ajabu na kweli! Kwa hiyo Waunguja wanataka watawale Zanzibar wenyewe milele!!??Tatizo ni wapemba Dk Shein na Maalim Seif kupewa hako kainchi,waunguja awakutaka kabisa hao wapemba wapewe hiyo nchi kwa sababu awakushiriki mapindunzi.Vinginevyo ni upepo tu utapita.:A S-confused1:
Serikali 4?
Tusiendekeze upuuzi kama huu. Ni lazima tuelewe kwamba umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Tukiendekeza hili la leo, kesho na keshokutwa tutasikia Mbeya, Iringa, Rukwa na Ruvuma nao wanataka kujitenga na kudai uhuru kamili.
Baba wa Taifa aliona Mbali sana,dhambi ya ubaguzi haiishi kamwe.. kumbe Pemba na Unguja sio wamoja tena, na hawajawai kukubaliana kuwa pamoja.
Muda sio mrefu tutashuhudia Pemba ikiwa ngome kuu ya Allshababi.
Ili kuikoa Zanzibar dawa ni Serikali moja Ya Tanzania.!
DHAMBI YA UBAGUZI,ni sawasawa na Kula nyama ya mtu!WAZANZIBAR wanaendelea kula nyama ya WATU!