MTANZANIA: CCM mnahangaika na Lowassa, CHADEMA wanachanja mbunga!

MTANZANIA: CCM mnahangaika na Lowassa, CHADEMA wanachanja mbunga!

Ni binadamu wachache sana wanaoweza kusema ukweli hadharani dhidi ya mabosi wao wanaowalipa mshahara kila mwezi kama ilivyo kwa Balile.
 
Hili gazeti siku hizi limekuwa la kipiganaji kidogo eeh?Makubwa mwaka huu.
 
kama uandishi wenyewe ndo huu bora usirudi kabisa ni hii miezi 4 tu uliyotaja. Unasema eti ulikuwa unatekeleza kazi ya kulijenga taifa, si kweli ulikuwa unatumikia tumbo lako na familia yako. Nimesoma makala yako ni ndefu ila ni pumba mwanzo mwisho. Wewe sijui ni mwandishi gani. Najuta kupoteza muda wangu kwa utumbo wako. Ungekuwa wa kike ningekuambia uende ukaolewe na lowassa hata kama ni nyumba ndogo/ya pebeni.
 
Rostam anajaribu kujiweka sawa na jamaa zake msipomwangalia vizyri balile mnaweza mkafikiri ni mwandishi wa habari kumbe kibaraka tu.
Ushindwe na ulegee.
 
Nimeisoma makala ya Deodatus, imenifurahisha sana, na wala sina hofu ya matusi ya kawaida kutoka kwa wasiotaka kusoma ukweli na kujadaili hoja, badala ya kuanza kuhoji mwandishi ameajiriwa wapi, nilifikiri mtu angeenda kwenye hoja na kusema aliyoyasema balile siyo kweli, lakini yote ni 100% accurate.

Nape anafanya siasa za visasi, na hata leo hii akiwa faragha na ndugu zake anamtukana Kikwete sana, siyo siri, kwahiyo wanaoweza kutukanwa hadaharani wa lile kundi linalolipiziwa kisasi cha 2005, ni Lowassa na Rostam.

Sitta ninamuheshimu, lakini haamini kwenye CCM na siku zote alifanya kazi kukivuruga, anaamini kwenye siasa ya vurugu na uana-harakati, na kwa umri wake hana cha kupoteza.

Leo CCM wanasema tatizo la kupungua kura ni Kagoda/Radar/Richmond/Dowans??? Je mtu yoyote mwenye akli ukijiuliza ni kweli hiyo??? Hapa Deodatus akaenda kutuambia ukweli wa kwanini kura zilipungua, kwa mammbo yanayohusu maisha ya watu ya kila siku na serikali kushindwa kutimizia wananchi wake, lakini pia tukumbuke hii ndiyo kampeni ambayo ilfanywa 'kifalme'kwenye historia ya CCM, maana yake Baba, mama na mtoto, kwa kisingizio kwamba viongozi wote wengi9ne wamekosa mvuto wa kuomba kura, hii nayo ni kweli iliwakasirisha viongozi wengi sana wa CCM mikoani na mawilayani.

Na kama tunakubali Kagoda/Radar/Richmond?dowans ndiyo matatizo, Kagoda inasemekana na kuthibitika na ndiyo maana Waziri Meghji aliondoka Wizara ya fedha kama mnakumbuka, kwamba fedha zilikwenda CCM, kwanini ahukumiwe mtu mmoja kama ni uwajibikaji wa kweli?? Kesi ya Radar imeshaisha Uingereza na walitoa ruling kwamba hakuna rushwa na Chenge hana kesi ya kujibu. Ukija kwenye Richmond/Dowanas, haka ndiyo kasinema kazuri sana, tulitumia fedha za walalahoi kwa mabilioni kuchunuguza ili tumpate Lowassa, ikashindikana na baadaye wananchi wakapewa adhabu ya kutokuwa na umeme kwa miaka minne sijui ili mradi isije kumsafisha Lowassa, leo amekuja Hillary Clinton ameenda kufanye press conference mbele ya mitambo na kuisisifia na sasa tunanenda kuwasha na kutumia umeme. Kwa tafsiri yangu ningekuwa kiongozi, ningeomba radhi watanzania na kusema sasa ndiyo THE END ya sinema ya Richmond/Dowans/Symbion. Kwa kweli imetosha sasa.

Kwahiyo hongera sana Deodatus Balile, na kama tunamtukana, tumjibu kwa hoja! Nawasilisha
 
Ni vizuri kusoma hizi chambuzi ambazo ni dalili kuwa CCM iko taabani, imekosa dira na kiongozi wa kurudisha katika msingi wa kuanzishwa kwake. Mwandishi naye anachambua kwa uegemezi wa kumtetea mtu fulani au maslahi fulani ndani ya chama. Tutaona mengi mwaka huu.
 
Muangalie huyo dogo nape akiwa ccj, kweli umenena, hata kwenye familia yako baba hata uwe mlevi vipi ila kama watoto wanakula na kushiba , wanaishi nyumba nzuri, wanasoma shule nzuri na wankula vizuri hatakuchukia hata siku moja, serikla ya sisiem ilishindwa kuwaletea maisha bora kama ilivyowaahidi ndiyo maana na si Rostam au chenge tatizo ni kikwete na akina nape wake
Ni vizuri kusoma hizi chambuzi ambazo ni dalili kuwa CCM iko taabani, imekosa dira na kiongozi wa kurudisha katika msingi wa kuanzishwa kwake. Mwandishi naye anachambua kwa uegemezi wa kumtetea mtu fulani au maslahi fulani ndani ya chama. Tutaona mengi mwaka huu.
 
Kwenda zako mmbinafsi mkubwa wewe! Huna chembe ya aibu kujaribu kuwateteaa hao mafisadi! Tuko hapa tulipo na umasikini mkubwa kwa sababu ya mafisadi hao wakubwa!
Usivyo na adabu unatukana watu hovyo hovyo! Kisa umepewa pesa kusemasema hovyo! CCM mna nini cha kuwaambia watz kama sio kutudidimiza kwenye umasikini! Leo hii tunazidiwa na Rwanda licha ya mauaji na vita vya mda mrefu! I hate CCM and I hate nyie vibaraka unatumia majukwaa ya wahariri kuendelea kusambaza uongo na j=kujustfy wizi wenu!
 
Huyu mwandishi si makini, ameongozwa na hisia zaidi. Hebu fikiria, anatumia neno "Sitanii" mara 8 kwenye makala moja. Huu sio uandishi makini.

Kuhusiana na mada, watu wake (Mwandishi) wamewekwa kwenye kona na siku za kutimiza "azma" ya kujivua gamba zinakaribia kwa kasi, anajaribu tu kuwanusuru. Hana mamlaka ya kimaadili kuzungumzia machungu ya watanzania (bei ya sukari, mafuta, n.k) maana alikuwa na nafasi ya kufanya hivyo mapema sana, lakini akaamua kukaa kimya kwasababu haikuwa kwa maslahi yake na anaowawakilisha. Matatizo ya waTZ yasitumika kama ngao ya "mikuki" wanayorushiana wanasiasa.
 
Wanajamii mimi nina swali moja tu,

Ikiwa kama Serikali iliyopo madarakani ni ya CCM, na ikiwa CCM ikaamua kuwafukuza au kuwanyan'ganya kadi za CCM hao wanaoitwa mapacha watatu, na kwa kutumia vyombo vyake vya Kiusalama, ikawafanya hawa mapacha watulie. Je kutakuwa na tatizo lolote? Hawa mapacha 3 ni nini zaidi ya maisha ya Watanzania takribani millioni 46?
 
Kwanza namsifu mwandishi kwa kuwa na ufahamu wa mambo ndani ya wanamagamba ila NAMLAUMU SANA KWA KUTUDANGANYA HAPA MWISHONI na kuonyesha dhahiri RA, EL, AC wanalaumiwa bila sababu . Hi biasness ni kubwa na ina negate kila alichoandika huko juu. Deo Babile onyesha msimamo acha kuwa kama POPO mkuu au unaogopa kumwaga unga?
 
Kwanza namsifu mwandishi kwa kuwa na ufahamu wa mambo ndani ya wanamagamba ila NAMLAUMU SANA KWA KUTUDANGANYA HAPA MWISHONI na kuonyesha dhahiri RA, EL, AC wanalaumiwa bila sababu . Hi biasness ni kubwa na ina negate kila alichoandika huko juu. Deo Babile onyesha msimamo acha kuwa kama POPO mkuu au unaogopa kumwaga unga?

Unamsifu kwa sababu haumjuhi, huyo anaitwa Deodatus Balile, ni mwandishi mahiri sana na alikuwa ni mhariri wa Tanzania daima, baadae Rostam Aziz akamnunua kujiunga na kampuni yake ya Habari corporation, na yeye sasa hivi ndio mhariri mtendaji wa gazeti la mtanzania.
Kwa kifupi Balile taaluma yake aliiacha pale freemedia na kule Habari corporation akaenda na tumbo. usitegemee uchambuzi wowote wa maana wa kisiasa kutoka kwa mwandishi huyu. ni puppet.
 
Badala yake amekirukia Chadema, anakwenda Rukwa anaeleza mambo ya aibu mbele ya jamii. Anatumia ishara za vidole viwili wanavyonyoosha Chadema kutamka maneno nisiyoweza kuyaandika gazetini. Hii ni dalili ya kutojiheshimu. Ni dalili ya kuwa na kiongozi asiye na chembe ya maadili katika jamii.

Chadema sasa wanatumia udhaifu wa CCM kuwa na viongozi chepechepe wa aina ya Nape na Chiligati wenye kuropoka kisha wakafungwa gavana midomo yao kujenga chama chao. Wanachanja mbunga wakiwaeleza wananchi umuhimu wa kuwa na katiba mpya. Wanazungumza lugha wanazopenda kuzisikia wananchi kama kushusha bei ya mfuko wa saruji, bati na kilo ya misumari isizidi Sh 5,000.

Wiki hii Chadema wanazungumza kukata posho za wabunge, ambapo wanasema wabunge wanalipwa mara mbili kwa kazi ile ile. Hapa hoja ni sahihi kabisa. Kwamba mbunge analipwa mshahara kwa kazi ya ubunge, analipwa posho ya kujikimu Sh 80,000 kila siku anapokuwa Dodoma, kisha analipwa Sh 70,000 kila siku anapoingia kwenye ukumbi wa Bunge. Hili ndilo lenye kuleta mgogoro. Kila awaye anajiuliza hawa wanatutumikia sisi walala hoi au wamekwenda kuchuma utajiri bungeni?

Sitanii, hii ni fursa nyingine kwa Chadema kuzidi kukonga nyoyo za wapigakura. Na haya ndiyo magamba halisi kwa CCM. Hesabu zilizopigwa ni kwamba posho zilizotengwa zikikatwa nchi hii inaweza kuokoa zaidi ya Sh bilioni 900. Kiasi hiki cha fedha kingeelekezwa katika ununuzi wa mashinde za kufua umeme, kwa wastani wa megawati moja Sh bilioni moja, ndani ya mwaka huu pekee tungezalisha megawati 900.
Ikwia kiasi hiki cha Sh bilioni 900 kingeelekezwa kwenye ujenzi wa miundombinu kama barabara, reli, usambazaji wa umeme vijijini au kununua madawati shuleni, kila mwanafunzi angekalia dawati. Lakini uliza. Hawa wabunge wakizipata hizi hela zinafanyiwa nini? Sitaki kusema ila ni aibu. Mwishoni mwa wiki nilikwua Dodoma, nilishuhudia maajabu. Wapo wabunge wanokesha baa wakinywa pombe na kuchoma nyama. Wengine wanafanya matendo ya kumuudhi Mungu, kwani karibu machangudoa wote wa Dar es Salaam na Mwanza sasa wamehamia Dodoma. Unadhani kama kusingekuwa na biashara machangudoa wangethubutu kulipa nauli kwenda Dodoma? Jibu mwenyewe.

MKUU HAPA KIDOGO KUNA POINT ILA HUKO KWINGINE NIMELAZIMIKA KUTOKUKUELEWA.

 
Waandishi Wote Wanajua Ukweli Uko Wapi Ila wanafisadiwa na hao Wamiliki ya hayo Magazeti; Waandishi wetu wanajua Mabaya isipukuw Ufisadi unawaweka matumbo njaa
 
Sisi wala hatutii neno malizaneni kwanza mpaka 2015 ndiyo tutatoa tamko.RAHA TUPU MAGAMBA MKIUANA WENYEWE KWA WENYEWE.
 
Wednesday, June 15, 2011
Na Deodatus Balile

Lakini uliza. Hawa wabunge wakizipata hizi hela zinafanyiwa nini?

Tuonane wiki ijayo
deobalile@yahoo.com au 0784 404827

Mkuu hukumsikia Pinda, alisema hizo pesa za posho wala mbunge hazitumii, bali ni kwa ajili ya kuwapa watu wanaowapiga wabunge vizinga na vibomu pale nje ya bunge!!!

Hakika tuna waziri mkuu makini!!!!!!!!
 
Macho hayashiba kuona na masikio hayachoki kusikia, hii ndo faraja kuu. Tutaona na kusikia mengi kabla ya ukombozi kufika.
 
Gamba limegoma kutoka, linaanza kuota upya juu ya jingine - hapo lazima nyoka aoze - inakuwa kansa na dawa na kansa ni kifo.
 
Back
Top Bottom