Mtanzania auawa kikatili Dubai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtanzania auawa kikatili Dubai

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Mar 4, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,746
  Likes Received: 82,686
  Trophy Points: 280
  Mtanzania auawa kikatili Dubai

  2009-03-04 10:56:04
  Na Mashaka Mgeta

  Raia wa Tanzania ameuawa kinyama kwa kutupwa katika mashine za kusaga vyakula huko Dubai, Falme za Kiarabu na mwili wake kukatwa vipande vipande.

  Taarifa zilizolifikia gazeti hili zimemtaja Mtanzania huyo kwa jina la Eric William Maige ambaye wazazi wake wanaishi Gezaulole, jijini Dar es Salaam.

  Marehemu Eric anadaiwa kuwa mfanyakazi wa kampuni ya Gulf Import and Export Limited wakati wa uhai wake.

  Akiwa katika kampuni hiyo, taarifa zinadai kuwa Eric alikuwa msimamizi katika kitengo cha G.G Department Al-Guair Food.

  Maofisa wa habari katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, hawakuwa tayari kuzungumzia kifo hicho, kutokana na kile walichokieleza kuwa kutopata taarifa hizo.

  Hata hivyo, maofisa hao wamethibitisha kupata taarifa hizo kutoka kwa watu waliojitambulisha kuwa ndugu wa marehemu Eric.

  Baba mzazi wa marehemu Eric, William Maige, aliliambia Nipashe jana kwa mujibu wa taarifa zilizopo, mwanae alipoteza maisha kwa kuuawa na watu waliokuwa chini yake kiutendaji.

  ``Mwanangu alikuwa msimamizi katika eneo lake la kazi, sasa kuna taarifa kwamba waliokuwa chini yake kimajukumu, walimtupa kwenye mashine za kusagia chakula, akafa,`` alisema.

  Kwa mujibu wa Mzee Maige, taarifa hizo zilitolewa na mdogo wa marehemu Eric, Raymond Maige, anayefanya kazi katika kampuni alipokuwa marehemu.

  ``Tuna uhakika kwamba mtoto wetu amekufa kwa sababu taarifa za kifo chake tumezipata kutoka kwa mdogo wake aitwaye Raymond, walikuwa wote huko Dubai,`` alisema.

  Alisema Raymond alifikisha taarifa nyumbani kwao kwa njia ya simu, kwamba Eric aliuawa asubuhi ya Jumatatu wiki hii.

  Mzee Maige alisema kutokana na hali hiyo, familia inatafuta uwezekano wa kupata msaada utakaofanikisha kurejeshwa nyumbani kwa mabaki ya mwili wa Eric.

  Alipoulizwa kwa njia ya simu jana, mmoja wa maofisa habari katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Assah Mwambene, alisema hakuna taarifa kuhusu tukio hilo.

  Mwambene alitoa namba kwa ajili ya mawasiliano na Balozi Mohamed Musa aliyepo Abu Dhabi, ambapo simu moja kati mbili zilizotolewa ilikuwa inaita bila kupokewa.

  Hadi tunaingia mitamboni jana jioni, jitihada za kumtafuta Balozi Musa na taarifa zaidi kuhusu mauaji hayo, zilikuwa zinaendelea.

  SOURCE: Nipashe
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwake tumetoka na kwake ndio marejeo yote. Nawapa pole sana wazazi, ndugu jamaa na marafiki wa huyu kijana wetu.

  Kwa UAE hao walomfanyia unyama huyu ndugu yetu wakipatikana na wao ni kifo tu.
   
 3. R

  Rodelite JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2009
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 320
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Na huyo Balozi mbona hapokei simu yake....???
  Hayo ndio matokeo ya kupeleka ndugu au rafiki
  kwenye balozi bila kufuatilia ujuzi na uchapaji
  kazi.
   
 4. Z

  Zungu Pule JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2009
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 2,139
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Na hata akipokea simu atasema hana taarifa. So, he will be as good as useless!
   
 5. 3

  3 kids Member

  #5
  Mar 5, 2009
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yes akipokea atasema hana taarifa yoyote,ndio wawakilishi wa Taifa letu hao,wanachotaka wao ni kujaza matumbo tu,hayo mengine ni km wamelala usingizi, nadhani angeuwawa mtt wa kigogo habari zingefika haraka sana na boss mkubwa hapo UAE asingepata usingizi kabisa ila kwa kapuku mmhhhh!!!!!???? POLENI SANA WAFIWA NA FUATILIENI MPATE UKWELI WA JAMBO HILI.
   
 6. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2009
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Na Mashaka Mgeta
  Nipashe


  Maofisa wa habari katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, hawakuwa tayari kuzungumzia kifo hicho, kutokana na kile walichokieleza kuwa kutopata taarifa hizo.

  Hata hivyo, maofisa hao wamethibitisha kupata taarifa hizo kutoka kwa watu waliojitambulisha kuwa ndugu wa marehemu Eric.  Sasa hapo ni kwamba tunaambiwa wamepata taarifa au hawajapata taarifa? Jamani jamani wasemaji wa serikali yetu na magazeti yetu jamani. Hivi mbona Kiswahili ni lugha nyepesi mno? Umezaliwa Tanzania kweli unafanya kazi kama msemaji serikalini au mwandishi wa gazeti la Kiswahili huwezi andika sentensi mbili zikaleta maana?
   
 7. C

  Chuma JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kuna kazi ktk kufanya ripoti....

  Nimebahatika kupigiwa simu na moja wa watanzania wanaofanya kazi na marehem kampuni moja vitengo tofauti. Ni kweli marehemu anafanya kazi na mdogo wake kampuni moja, na pia ni kweli Marehem pia alikuwa supervisor.

  Nilimuuliza Huyu mdau tukio lilikuwaje...lkn hata wao hadi sasa hakuna alie na taarifa kamili juu ya sababu kilichopelekea kifo chake

  kwa anavyosema huyu mdau ni kuwa Marehem alikwenda ku-supervise hizo machine...haileweki ni kwa namna gani aliingia ktk hizo machine zikamsaga saga,...Hapa kuna uwezekano wa sababu 2.

  1. Moja inawezekana Marehemu wakati anaangalia machine..akateleza ktk belt wakati huo machine zinawaka...hviyo zikamsaga saga...!!

  2. Kuna uwezekano pia wakati Marehemu anafanya ukaguzi, mfanyakazi mwingine ambae alikuwa duty alikuja kuwasha machine bila kujua kuna mtu anafanya ukaguzi.

  Kwa hili la pili ambalo huyu mfanyakazi atakuwa anaogopa au hadi uchunguzi ufanye...

  Sijashawishika kusema marehem kauwawa kiasi cha kutupwa ktk machine imsage....kwa tukio hili maana yake kuna wafanyakazi wengi wamekuwa involved...lkn pia itakuwa lazima ugomvi ungetokea. kwa watu wanaowajua wahindi walivyodhaifu hata kupigana na mtu MTZ wanaogopa!!!

  pia Kuna tukio lilitokea mwaka Jana hukohuko dubai, niliarifiwa na Mdau aliekuwa anafanyakazi Melini. ambae alirudi likizo mwisho wa mwaka jana....ambae yeye anasema kuwa Kuna MTZ mwingine ambae alikwenda ktk propelar za Engine ya meli kusafisha..na akaweka Alert zote...Bendera na other signs...ikatokea kuna mfanyakazi mwingine ambae ali-ignore hizo signs, akaenda kuwasha Engine ikamsaga saga kabisa huyu Mbongo...kesi wahusika wote walikamatwa na wapo Jela...

  otherwise tusubiri Taarifa rasmi ya Police wa Dubai kutuarifu hili jambo.
   
 8. B

  Bull JF-Expert Member

  #8
  Mar 5, 2009
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi hawa jamaa hapa mambo ya nje wanafanya kazi gani?

  sielewi ofisa habar, Assah Mwambene badala ya kusaidia familia kuwasiliana na balozi wanatoa namba za Simu kwamba victim wajishughulikie wenyewe, kumbe wao mambo ya Nje ndo walitakiwa wapate maelezo toka kwa balozi walie mtuma wao huk UAE

  Tunaitaji changes wizara ya Nje watu hawajui wafanyalo, sisi ndo tunalipa kodi mambo kamahaya yakitokea niwajibu wao watoe maelezo, hii wizara imeozaaaaa inanukaaa!!!
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Mar 5, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Kwanza sijui kwa nini umesema Wahindi na sio watu wengine. Unataka ku imply kwamba aligombana na Wahindi na ndio wakamweka humo kwenye mashine kwa kuogopa kuzipiga naye kwa vile yeye 'alikuwa' MTZ?

  Pili, hiyo ya udhaifu wa Wahindi ni dhana potofu. Siku ukija kupigwa na mhindi sidhani kama utaendelea kuishikilia hiyo dhana.
   
 10. r

  rolemodel Member

  #10
  Mar 6, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 11
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  May God rest his soul in eternal peace.
   
 11. M

  Mbwajira Member

  #11
  Mar 6, 2009
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  umangani hakufai, ndugu zetu wanafanyiwa mambo ya kinyama sana. Pole kwa wafiwa.
   
 12. paulsifa

  paulsifa Member

  #12
  Mar 6, 2009
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  kweli sisi katika utumishi we sacks.kama ndugu wamekuja kukueleza au kufuatilia habari za ngugu zao walio nje badala ya wizara kufanya jitihada kuwasiliana na balozi wao wanatoa simu basi ndugu ndo wapige.ningetaka simu si ningeingia mtandaoni ningeipata hata mie mwenyewe?
   
Loading...