Mtanzania anusurika kufa moto Marekani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtanzania anusurika kufa moto Marekani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Nov 29, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,403
  Likes Received: 81,427
  Trophy Points: 280
  Mungu ashukuriwe.

  Mtanzania anusurika kufa moto Marekani
  HOUSTON, MAREKANI
  Daily News; Saturday,November 29, 2008 @20:00

  Mwanamke Mtanzania amenusurika kufa wakati moto ulipounguza sehemu ya jengo analoishi katika kitongoji cha Dairy Ashford, Houston nchini Marekani. Mwanamke huyo, Honeymoon Aljabri (33), alikuwa amelala katika kochi wakati moto ulipokuwa ukiunguza nyumba ya jirani yake katika ghorofa wanaloishi kwenye Mtaa wa Charleston, 2800 S jirani na Westheimer.

  Wakati moto huo ukiendelea, mtu ambaye hajafahamika alifungua mlango kwa nguvu na kumweleza Aljabri atoke nje; alipofungua macho akaona moshi mzito ukiingia sebuleni kwake kutoka sehemu ya juu ya sehemu anayoishi. Baada ya kuona hivyo, Mtanzania huyo alijaribu kutafuta pasipoti yake na pochi ndogo ya kuhifadhia fedha na vitu vidogo vidogo, lakini moshi na joto vilisababisha atoke nje haraka.

  Mtanzania huyo alishuka chini akaenda kusimama kwenye eneo la kuegeshea magari akiwa amejitanda nguo nyepesi ya kulalia, kabla ya msamaria kumpa fulana na nguo ya ndani, akazivaa papo hapo huku akitazama wafanyakazi wa zimamoto wakizima moto huo. "Moshi ulikuwa mweusi, nilikuwa natetemeka, niliogopa sana," gazeti la Houston Chronicle lilimkariri Mtanzania huyo akisema.

  Taarifa zimebainisha kwamba, taarifa za kutokea kwa moto huo zilitolewa dakika chache kabla ya saa saba usiku wa Jumapili iliyopita. Kwa mujibu wa taarifa hizo, moto ulianzia katika moja ya makazi yaliyopo ghorofa ya pili ya jengo hilo na ukasambaa haraka kwenye sehemu nyingine.

  Mkuu wa Kitengo cha Zimamoto mjini Houston, Calvin Petrosky alisema sehemu yote ya juu ya ghorofa hilo iliharibika, nyumba za sehemu ya chini zilipata madhara ya moto na maji. Moto huo uliharibu makazi manane kwenye jengo hilo liitwalo Alief Complex.
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Dec 2, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,080
  Likes Received: 5,556
  Trophy Points: 280
  Embu tuambieni na nyie mliokuwa huko!!!kila siku motomoto
  majuzi mmemleta mdogo wwetu nae kafia kwa moto!!!huko usa
  wanawashamoto walipwe na bima au!!!!ndio yale yale????????
  Pole bibie hnysabri!!1mungu akulinde milele
  amin
   
Loading...