hizi ndio hoja sio kulalamika tu ooh waziri waziri ila naona watu wanachelewa kuchangia hoja hii kwa sababu aliyeanzisha sio member mwenye jina wanasubiri mwanakijiji aandike hata upuuzi wajibu.Big hizi ndio hoja na ntakuja na tathmini yangu jinsi gani mtanzania wa kwaida anvyoweza kujiondoa kwenye lindi hili la umasikini
Nimeonelea niiache kwakuwa nshatoa maelezo, nitaihamisha endapo kutakuwa na ulazima wa kufanya vile. Nawakaribisha wachangiaji kuweza kudadavua hoja iliyowasilishwa.Ni kwa sababu hiyo basi, naihamisha hoja hii kwenda Jukwaa la Uchumi kwakuwa naona inafaa sana kuwa kule.
Tanzania ni moja kati ya nchi masikini duniani ambayo zaidi ya asilimia 50 ya watu wake wanaishi katika umasikini ambao unachangiwa na ukosefu wa Ajira, Uzalishaji Kidogo, Ujinga, uchanga wa Sayansi na Technolojia na ukosefu wa Uwiano wa Biashara unaosababishwa na Madeni Makubwa ya Nje, na Usawa wa Biashara katika Masoko ya Nje na Sera sizizo nzuri.
. . . . Kwa kuzingatia hali halisi ya nchi yetu na jinsi inavyokosa uongozi thabiti wenye kutetea maslahi ya taifa kwa nguvu zote na uzalendo wa hali ya juu katika ubunifu wa sera nzuri . . .
. . . . Pia kwa kuzingatia kuwa katika Jambo Forum wengi wameonyesha uzalendo wa juu katika kutetea maslai ya taifa na kuwa wana uwezo wa hali ya juu katika kuyachambua mambo kwa kuzingatia hali halisi . . .
. . . . Na pia kwa kuzingatia kuwa kuna baadhi ya watanzania mijini na vijijini wamweza kujikwamua katika lindi la umasikini katika mazingira ya sasa tuliyomo kwa njia halali na zinazokubalika . . .
Napenda kutoa hoja ya kudumu sasa kuwa JF ijadili kwa kina na umakini wa hali ya juu ni namna gani Mtanzania Masikini na Kawaida katika Mazingira ya sasa hivi anaweza akabadili hali yake ya kawaida na kuondoka katika lindi la umasikini na hatimaye kujitengenezea utajiri kwa njia halali bila kutumainia siasa.
Maoni na mapendekezo yote yanaweza kuratibiwa baadaye na JF na machapisho kufanywa kwa ajili ya kuweza kuwasaidia watanzania wote kuondokana na umasikini. Ni matumaini yangu kuwa huu utakuwa ni mchango wetu bora hasa kwa watanzania wasio na namna ya kutembelea Jukwaa hili.
Naomba sasa kutoa hoja.
4.Give back to your community- Maendeleo yanaletwa na watu - Tuanze tabia ya kuchangia maendeleo ya nchi bila kutegemea kulipwa...Community service ni muhimu kwa nchi kupunguza gharama za ajabu ajabu.
Sio lazima serikali itegemewe kupeleka maji vijijini...kama mtu unaishi huko una hela peleka maji kwa kijiji, kama mtu una hela fungua library watu wajue kusoma, kama unahela do something for your country...Huku watu wakifa tunaona wills zao kila siku zinasema hela hii iende kusaidia shule hii, hospital hii, kanisa hili etc lakini wabongo kwa uchoyo wills zetu ni watoto wetu tu basi hata kama mtoto wako amebarikiwa tayari na ana uwezo wakuishi mpaka afe bila kutegemea hela yako basi utamwengezea nyingine tu...Wape watu wasio na uwezo na utabarikiwa sana tu ipe kijiji chako kitafanya la maana na hiyo hela....
Superman,
Nimekipenda sana kipengele hiki.
Hivi tujiulize ni Watanzania wangapi wenye uwezo wa kielimu, kifedha, na kimaarifa/kiujuzi wanajitumikisha kwenye community service? Generally, wengi wetu hatuna moyo wa ku-give back to the community. Unajua, hakuna msaada wenye akili wa kumpatia mtanzania mwenzako kama wa kumu-empower with knowledge and skills.
Kama ni kweli watu wanavyosema kuhusu kwamba kuna wataalamu wengi wa kitanzania nchi za nje, then kwa nini hawatumii knowledge na exposure yao kujitolea kuchangia kwenye community zao za nyumbani? Cummunity service ni msaada mmoja makini mtu unaweza kuutoa kwa faida ya taifa.
Mfano, nchi yetu haina entrepreneurs wa kutosha. Na hao wachache waliopo ni wavivu wa explore aina/mbinu mpya za kibiashara. Na matokeo yake wanakesha kuigana kila kitu kwenye biashara. Leo hii ukianzisha biashara yako ya ashikirimu za ukwaju, ukiamka kesho asubuhi utakuta mtaa mzima wanauza ashikirimu za ukwaju. Yani hakuna hata jirani mmoja hatakayefikiria angalau kuuza ashikirimu za maziwa. Sasa basi, ni kwa nini watanzania wenye elimu na/au ujuzi wakibiashara wasijitokeze kwa wingi kuanzisha kongamano za kibishara?
Hivi kuna Watz wowote ambao wanafikiria kuanzisha program ya kutembelea vyuo mbalimbali bongo na kuwa guest speakers madarasani bila ya kutegemea kulipwa posho? I can only imagine, kama mfanyabiashara akitembelea darasa la biashara UDSM na ku-discuss his/her personal business experience, ni wanafunzi wangapi watatoka na real business knowledge at the end of the lecture?
I mean, biashara ni mfano mmoja tu. Lakini kuna sayansi, tech, kilimo, law, mazingira.....the list goes on
Una-give back kwenye community pale unapokuwa na surplus.
Bin Maryam,
Nakubaliana na wewe kama tunazungumzia tangible assets. Lakini ni surplus gani mtu anahitaji kuwa nayo kabla hajahamua ku-give back to the community kwenye masuala ya intangible assets kama elimu na maarifa/ujuzi?
Nadhani kwenye mambo ya maarifa na ujuzi kuna matatizo fulani. Wengi waliopata ujuzi na maarifa waliacha jamii zao wakiwa na miaka 15 kwenda kusoma. Na wanapomaliza masomo wanapangiwa mbali na mikoa yao, hivyo uhusiano wa kurudisha unakuwa umepungua.
Hivyo unapohamua kupiga ukabila au udini kwa kuwapeleka watu mikoa tofauti unaondoa-bond ya watu na sehemu zao na hiyo ni hasara ya kuimeza.