Superman
JF-Expert Member
- Mar 31, 2007
- 5,696
- 1,685
Tanzania ni moja kati ya nchi masikini duniani ambayo zaidi ya asilimia 50 ya watu wake wanaishi katika umasikini ambao unachangiwa na ukosefu wa Ajira, Uzalishaji Kidogo, Ujinga, uchanga wa Sayansi na Technolojia na ukosefu wa Uwiano wa Biashara unaosababishwa na Madeni Makubwa ya Nje, na Usawa wa Biashara katika Masoko ya Nje na Sera sizizo nzuri.
. . . . Kwa kuzingatia hali halisi ya nchi yetu na jinsi inavyokosa uongozi thabiti wenye kutetea maslahi ya taifa kwa nguvu zote na uzalendo wa hali ya juu katika ubunifu wa sera nzuri . . .
. . . . Pia kwa kuzingatia kuwa katika Jambo Forum wengi wameonyesha uzalendo wa juu katika kutetea maslai ya taifa na kuwa wana uwezo wa hali ya juu katika kuyachambua mambo kwa kuzingatia hali halisi . . .
. . . . Na pia kwa kuzingatia kuwa kuna baadhi ya watanzania mijini na vijijini wamweza kujikwamua katika lindi la umasikini katika mazingira ya sasa tuliyomo kwa njia halali na zinazokubalika . . .
Napenda kutoa hoja ya kudumu sasa kuwa JF ijadili kwa kina na umakini wa hali ya juu ni namna gani Mtanzania Masikini na Kawaida katika Mazingira ya sasa hivi anaweza akabadili hali yake ya kawaida na kuondoka katika lindi la umasikini na hatimaye kujitengenezea utajiri kwa njia halali bila kutumainia siasa.
Maoni na mapendekezo yote yanaweza kuratibiwa baadaye na JF na machapisho kufanywa kwa ajili ya kuweza kuwasaidia watanzania wote kuondokana na umasikini. Ni matumaini yangu kuwa huu utakuwa ni mchango wetu bora hasa kwa watanzania wasio na namna ya kutembelea Jukwaa hili.
Naomba sasa kutoa hoja.