Mtanzania aliyepo Congo Kinshasa

Mtanzania aliyepo Congo Kinshasa

Ninaomba kama kuna Mtanzania yeyote aliyepo nchi tajwa hapo juu na ana connection na kampuni yeyote inayojihusisha na uchimbaji wa madini anisaidie kunishika mkono nipate kazi huko.
Nina shahada ya uhandisi wa Mitambo na nina uzoefu wa mwaka mmoja katika kusimamia, kuzikarabati na pia kukagua engine na mitambo mingine midogomidogo.
Ninathamini kazi na pia huwa niko mbele ya muda kuhakisha nafikia mpango mkakati wa taasisi husika.
Natanguliza shukrani zangu kwa mtoaji au atakayesaidia kupatikana kwa msaada. Unaweza ukanifikia kwa PM.
Kama umepata tuambie mkuu
 
Sikupata Mkuu, naona watu wako kimya
Wabongo sijui tunakwama wapi kwenye kushikana mkono, unakuta mtu hahitaji msaada wa kifedha lakini anashindwa kusaidiwa.

Kama unaweza kujilipua fanya ivo mkuu. Wakati fulani nilihitaji kwenda Nairobi kuchukua mzigo fulani hv, nilikosa msaada kabisa kwa watu ninaowafaham ikabidi nijilipue nikaenda sijuani na mtu hata mmoja huko, lakini nashukuru Mungu nilifika nikapata marafiki wapya huko na siku hizi naenda bila shida.
 
Tatizo ni yeye connection ya kazi ni ngumu kwa maisha ya sasa km ni biashara njoo tuko wengi tu tulio kimbia njaa ya bongo.
 
Natamani sana kujilipua ila nilihitaji tu walao ramani nisije ishia kwenye mikono isiyo salama, ingekuwa ni nchi ambayo iko bayana kidogo kama ilivyo Kenya ambayo unajua nikipita hapa natokea mji fulani ningefanya hivyo, ila ninavyojiona itabidi tu nihiari ama niishie kwenye mikono hatari ama nifike ninakotaka.
 
Tatizo ni yeye connection ya kazi ni ngumu kwa maisha ya sasa km ni biashara njoo tuko wengi tu tulio kimbia njaa ya bongo.
Mkuu hiyo biashara natamani sana ila mtaji ndo unakuwa nongwa, ila kama utakuwa unajua biashara ambayo itahitaji mtaji kidogo nielekeze tu nije niipiganie
 
Back
Top Bottom