Mtanzania aliyebaguliwa kwa rangi yake Uingereza alipwa fidia sh. mil. 60

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054

Mtanzania aliyebaguliwa kwa rangi yake Uingereza alipwa fidia sh. mil. 60

Mtanzania aliyebaguliwa kutokana na rangi ya ngozi yake na kusimamishwa kazi isivyo halali ili kuwapa nafasi wazungu nchini Uingereza ameshinda kesi yake na imeamuriwa alipwe fidia takribani shilingi milioni 60.

Mtanzania Zaina Ukwaju amelipwa kiasi cha pound 30,000 sawa na takribani shilingi milioni 60 za Tanzania kama fidia ya kubaguliwa kazini akiwa kwenye Baraza la wakimbizi la Uingereza.

Zaina ameshinda kesi yake aliyofungua baada ya kufukuzwa kazi kama mshauri wa mahabusu kutokana na ubaguzi wa rangi aliofanyiwa katika kituo cha uhamiaji cha Oakington kilichopo Cambridge.

Zaina alifukuzwa kazi isivyo halali na kubaguliwa kutokana na rangi ya ngozi yake.

Zaina aliyezaliwa Tanzania alisimamiswa kazi baada ya shirika alilokuwa akilifanyia kazi kutangaza kufunga kituo chake cha kusaidia wahamiaji mwaka 2006.

Lakini baada ya mipango ya kufungwa kwa kituo hicho kusimamishwa Zaina na mfanyakazi mwenzake toka Nigeria hawakurudishwa kazini na kukaa bila kazi kwa miezi mitano baadae.

Kuondolewa kwao kazini kuliacha wazungu tu wakiendelea na kazi huku kukiwa hakuna mweusi yoyote kazini hapo.

Mwenyekiti wa kamati ya ajira iliyokuwa ikisimamia kesi hiyo alisema kuwa wafanyakazi wazungu walibakishwa huku wakiwa na ufanisi mdogo wa kazi kulinganisha na wafanyakazi weusi waliokuwa wakifanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa.

kamati hiyo iligundua kuwa meneja wa Oakington Anne-Marie Leach aliwapendelea rafiki zake wa karibu huku wafanyakazi wengine waliohudhuria sherehe aliyofanya nyumbani kwake wakinusurika kusimamishwa kazi kutokana na kuhudhuria sherehe ya meneja huyo.

Kamati hiyo iliamuru baraza la wakimbizi limlipe Zaina pound 15,000 kwa kumuumiza kihisia kutokana na ubaguzi wa rangi waliomfanyia, pound 8,000 kwa kumsimamisha kazi isivyo halali , pound 5,000 kwa kumbagua na pound 2,643 kwa kumsababishia kukosa kipato kwa kipindi chote alichokaa bila kazi.

Fidia atakayolipwa mfanyakazi mwenza wa Zaina Mnigeria Emanuel Obikwu ambaye naye ameshinda kesi yake itaamuliwa baadae.

Source: News Agencies

Eeh! Na wazungu wanapokuja hapa na kupandishiwa bei za vitu hata mara 10 au zaidi ya bei ya kawaida kwa vile ni wazungu wanaweza nao wakawa wanashitaki wafidiwe. Nachukia ubaguzi sana na vilevile huwa naona na sisi tuna ubaguzi wa namna hiyo dhidi ya wazungu au watu wa mataifa mengine.
 
Back
Top Bottom