Iringa: Ahukumiwa Kifungo cha Maisha na Fidia ya Mil 5 kwa kubaka Mtoto wa Dada yake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemuhukumu kifungo cha maisha jela na kulipa fidia ya Tsh. milioni 5 Joshua Mkwalakwala (35) Mkazi wa kijiji cha Makota kilichopo Wilaya na Mkoa wa Iringa baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka Mtoto wa Dada yake mwenye umri wa miaka 10 aliyekuwa akisoma darasa la nne.

Tukio hili lilitokea Agosti 22 mwaka jana saa tisa mchana ambapo siku ya kwanza Joshua alianza kwa kumuonesha Mtoto huyo sehemu zake za siri (uume) akimwambia "Unaijua hii?" ndipo Mtoto huyo akakimbia, siku ya pili alimfuata Mtoto huyo akiwa na anacheza na wenzake na kumpeleka vichakani kisha kumfanya unyama huo.

Kesi hii ilikuwa na jumla ya Mashahidi watano ikiongozwa na Waendesha mashtaka wawili Nashoni Saimon pamoja na Baton Mayage, akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkuu Said Ally Mkasiwa amesema Mahakama imemkuta na hatia baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo shaka, Mtuhumiwa alipopewa nafasi ya kujitetea aliiomba Mahakama imuonee huruma na imuachie huru ili aweze kulipa fidia.

Kesi za ubakaji na ulawiti zimekuwa zikiripotiwa kwa kasi Mkoa wa Iringa huku imani za kishirikina, ulevi na magonjwa ya afya ya akili vikitajwa kama sababu kuu ya matukio haya.
 
Miss you zomboko ,kule jukwaa la kimataifa where are you?
 
Huyo jamani anaenda kuongeza mzigo tu kwa serikali wangekua wanawamaliza kimya kimya huko gerezani
 
Back
Top Bottom