Dahafrazeril
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 1,500
- 2,061
Nobody is perfect.Polini = Porini
Afu = Alafu
Unaijua tafsiri ya alama ya sawa sawa(=)?.Yaani hapo umemaanisha neno polini ni sawasawa na neno porini, pia neno afu ni sawasawa na neno alafu.
Hatuna neno alafu, tuna halafu.
Back to the topic.
Matangazo yote ya Television hayana ubunifu hata kidogo.Huwa nikiliona tangazo lolote nazima Tv.
Lile tangazo la P.S.P.F, anauliza "Shosti ni kwa mshahara wako ninaoujua au shemeji kakopa mkopo kugharamia shughuli yote hii"?."Aaah unakumbuka.....blaa blaa kibao (ujinga mtupu)".
Tangazo la BIKO, Mpoki anapiga simu anamwambia mtu "Yaani nimekuwa mweupe...", "Zungika dunia nzima mama hakuna mkate mgumu mbele ya chai", serious?.
Tangazo la Magodoro Dodoma, yule mzungu sijui muhindi huwa ananiacha hoi pale anaposema "Magodoro Dodoma is the best in Tanzania".Sifahamu kilichozingatiwa hadi yeye kuingia katika Tangazo lile.Non sense.
Matangazo yote ni Joti na Mzee majuto, hakuna wengine zaidi yao?.Inakera sana.
Bongo ubunifu sufuri.