Mtangazaji wa RTD Abisae Steven afariki dunia

Barubaru

JF-Expert Member
Apr 6, 2009
7,161
2,318
Amani iwe nanyi,

Nimepokea habari za msiba wa Mzee wetu Abisae Stephen aliyekuwa mtangazaji mkongwe sana na mwandamizi wa Radio Tanzania.

Nimeelezewa amefariki dunia Juzi hospitali akiwa anasumbuliwa na maradhi. Na maiti yake imesafirishwa jana 12 aug kwenda kuzikwa kwao Moshi.

Hakika Tanzania wamepoteza mwanahabari mahiri sana na mzoefu katika tasnia ya habari nchini humo.
Kwa tuliowahi kufanya nae kazi japo kwa kipindi kifupi, Alikuwa ni mtu mcheshi sana na alikuwa mahiri sana kwa lugha mbalimbali za kigeni. Aliweza kuongea lugha zaidi ya tano ukiondoa lugha yake ya kikabila ya kichaga.

Wengi tulizoea kumwita Kaka au hata Mz wa Lugha.

Hakika ni msiba mkubwa na nashangaa mpaka leo waandishi wa habari huko Tz wameacha kuandika msiba huu.

Hakika Mola amlaze pahala panapo stahiki.

Ni Mimi
Bi Nasriyah Saleh Al Nahdi.
Doha
 

sinafungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
1,522
860
INNALILAH WAINNAHYRAJGHUUN, kwa sisi vizazi vya SLP tumepoteza mtu mahiri sana, ahasante kwa taarifa yako, lkn hivi hata (RTD) TBC nao kimyaaaaaaa?
 

Lokissa

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
7,444
2,475
ndio anazikwa mchana huu huko kwao najara wilaya ya hai mkoa wa kilimanjaro, mungu amrehemu apunzike kwa amani.
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom