Mtangazaji Shafii Dauda vs Msemaji wa Simba, Haji Manara

Jamaa kasahau majukumu yake kama msemaji wa Simba na sasa hivi anachofanya ni kujibizana mipasho tuu na watu baki

Msemaji wa Klabu kazi yako ni kutuhabarisha taarifa za timu,mipango,mikakati,habari za wachezaji,maendeleo ya timu kwa ujmla nk

Sasa msemaji unaanza vijembe na ushabiki wa kiboya boya kama bwege bhana!!

Mie Simba, ila manara ananiboa to some extent!
Pole sana Mtani.
 
Kuna vita inaendelea kwenye social media kati ya watu wawili ambao wanajulikana ni wana Msimbazi kinda kindakindaki.

Kila kijembe cha Dauda kinajibiwa kwa kuikashfu Yanga ambayo haina uhusiano na ugomvi wao.

Kila kombora la Shafii linajibiwa kwa kuikejeli Yanga. Vyema Haji akajua namna ya kupigana vita yake.

Au Shafii anaiwakilisha Yanga kwenye ugomvi wao? Kwenye vita, kwanza mjue adui yako.
Dauda si mwanaYanga?
 
Bifu la haji manara na shafii dauda ni ugovi wametengeneza wao tu hasa baada ya dauda kuibiwa account yake 1million followers so naona wameamua kupigana tafu kukuza account yake dauda maana wanajua wabongo wapenda ubuyu sana . naona hii mbinu imesadia maana dauda sasa hivi account imekua fasta sana kwa muda mfupi tu 95k
Logopit_1546278731088.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bifu la haji manara na shafii dauda ni ugovi wametengeneza wao tu hasa baada ya dauda kuibiwa account yake 1million followers so naona wameamua kupigana tafu kukuza account yake dauda maana wanajua wabongo wapenda ubuyu sana . naona hii mbinu imesadia maana dauda sasa hivi account imekua fasta sana kwa muda mfupi tu 95kView attachment 985604

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimekuelewa sana Mkuu hasa kutokana na hii kauli ya Manara hapo nyuma.
20190104_112535.jpg

Hii ni movie wanatuchezea sababu haiwezekani mtu mwenye ugomvi naye halafu aombe watu wamfollow.
 
Na zani una jua au fahamu kuwa manara ni mhamasishaji... kuhamasisha kwake kuna leta morali kiushindani kwa washabiki na wachezaji wasijisikie wanyonge...

Ndio maana mara nyingi timu zina tumia nguvu kubwa kuomba nguvu ya washabiki kwa kujitokeza kwa wingi kuwapa nguvu wachezaji na kuwa discourage wapinzani kwa kuwa tia hofu...

sasa ukianza kuwa na hofu wewe mwenyewe ukiwa kwako una tegemea nini?? Nyumbani ni Nyumbani hata kama hamnywi chai...!

Simba si underdog, Simba ni timu ya ushindani...! na Manara ana pigana leo kesho kupeleka morali kwa washabiki na wachezaji, una ona ana wafunga kamba za viatu wachezaji, yupo kama mjinga mjinga lakini ana fahamu analo lifanya, nikama alivyo kuwa ana fanya ndg. Jerry

nazani swala la morali kwa wachezaji nenda kamuulize Mourinho... si alikuwa na timu ya wana saikolojia sasa ilikuwaje akawa ana hamasisha timu, na baadae akawa ana wavunja moyo wachezaji wake yeye mwenyewe, Je wana saikolojia walikuwa wapi kufanya kazi yao kipindi wanapo vunjwa moyo na kocha...

Mf. sasa hivi Man Utd wachezaji wana amani wana furaha... wana saikoloji walikuwa likizo ya mwaka mpya na chrismas??
Lakini hayo yote hayajajibu maswala yangu mawili ya msingi: 1. Benchi la Ufundi halina mtaalamu wa kuwatuliza wachezaji kisaikolojia hadi kazi hiyo ifanywe na mhamasishaji? 2. Kuna uhakika gani kuwa uhamasishaji huo wa njia ya mipasho dhidi ya Shafii utawafikia wachezaji na kwa namna itayowajenga ipasavyo?
 
Hatua ya Simba kuwa kampuni bila shaka ni ya maendeleo.

Je ile dhana ya msemaji wa club kama ilivyokuwa zamani bado ina nafasi kwenye kampuni? Nadahni kampuni hata club nyingine kubwa zinatakiwa kuwa na Afisa Habari mwenye taaluma ya IT ambaye kazi yake kubwa ni kumanage vitu kama tovuti ya club.
Duu! Mpaka we mnazi wa Yanga unaishauri Simba? Kweli Manara ni mwiba uliokomea kwenye Koromeo la Yanga. Poleni watani mtazoea tu japo mwanzo mgumu
 
Lakini hayo yote hayajajibu maswala yangu mawili ya msingi: 1. Benchi la Ufundi halina mtaalamu wa kuwatuliza wachezaji kisaikolojia hadi kazi hiyo ifanywe na mhamasishaji? 2. Kuna uhakika gani kuwa uhamasishaji huo wa njia ya mipasho dhidi ya Shafii utawafikia wachezaji na kwa namna itayowajenga ipasavyo?
Mkuu ebu jaribu kufikiri zaidi na zaidi... usi ishie hapo ktk kufikiri...
 
tatizo ni mifumo yetu ambayo tuna wasemaji wa timu kwa wasio na maamuzi kwenye timu,mfano manara ndani ya simba ni kama loud speaker tu,ona wenzetu walioendelea kocha ndiye msemaji wa timu(mfano real madrid,man utd,ac milan,n.k)lazima tuachane na mifumo isiyo na tija ili tuelekee kule kwenye maendeleo ya kweli na sio kwa hawa wapiga domo tumbo lishibe
 
Back
Top Bottom