Ukimaliza kuchunfuza Azam TV hamia ukachunguze na TBC kuna dada mmoja kila siku habadilishi wigi, kila siku anavaa hilo hilo tu ni mwaka wa kumi sasa...
Ivona hana makuu.Anapenda maisha ya kawaida.Kuonekana kwenye tv kila siku hakujampa mchecheto wa kuvaa nguo mpya kila siku.Anachukulia kawaida..kinyume na tabia za vidada vingi vinavyopenda maisha ya kuigiza.
Mleta Uzi wewe ni mpuuzi kweli,
Labda nikukumbushe tu kuna watu wanashona nguo ya rangi moja,mtindo mmoja kwa wingi kadiri apendavyo.
Mfano jirani yangu utazitambua siku anafua .
Jamani msema kweli mpenzi wa Mungu....Binti yangu yuko darasa la saba anampenda saana huyu mtangazaji Kamuntu pamoja na Bebi Kabae wa Clouds na anataka kuwaona mubashara.Namuambia mama yake ampeleke pale Azam Tv na Clouds lakini anaogopa.....ipi njia rahisi ya yeye kuwaona....
Natamani ningekuwa na uwezo ya kuwaambia wamiliki na wasimamizi wa JF kuweka kumbi za watoto ili tuchague cha kusoma na mahali pa kusoma.Gauni la Ivona Kamuntu linakufanya uwe na cha kuandika na Jamii Forum wanaona huo ni uhuru wa habari