Mtangazaji ITV uliyehabarisha wizi wa box la kura Magomeni uwe makini, unatafutwa na "kuwindwa" kwa muda mrefu

Maskini, wasimpoteze tu kijana wa watu. Boss ameshaomba radhi kwa kilichotokea jana hope msamaha umekubaliwa na wanye ñjiii hii
 
Acha mambo ya Kizamani Uchaguzi ulishaisha na tuheshimu maamuzi ya wana Kinondoni. [HASHTAG]#KinondoniDecided[/HASHTAG]. Kila Uchaguzi mkidondokea pua mnasingizia kuibiwa kura.
hahahaha umekunywa chai?

Sasa wapi kumeandikwa kura zimeibwa?
 
Hilo la box la kura eti kuibiwa ni uzushi mkubwa mno....Chadema hiki hakikukosi kutunga uongo kila siku...box liibiwe ili iwe nini??? Tanzania hii hatujafikia hukokuiba box la kura....
khaaa we muogope mungu mbona kila kiti kilikuwa wazi ITV jana. hahahahah kweli nimeamini kuwa ccm lazima ujitoe akili
 
Ukawa Kwa habari Za kufikirika na kujitungia! Asa huyo dogo awindwe Kwa lipi. Bora ungemwambia mbowe aliyesababisha Fujo Hadi mtu kafa
Hivi anayesababisha kifo ni mtu anayetembea au ni anayefyatua risasi? Kwani kutembea mkiwa wengi au kuandamana ni kosa? Aliyepigwa risasi alikuwa anaandamana? Hakuna sababu yoyote ya kuhalalisha mauaji haya. Kama wangeachwa watembee waende wanakokwenda kungekuwa na madhara gani? Polisi wetu busara ni ziro kabisa wala hawakujifunza kwa wenzao wa Kenya wakati wa kujiapisha Odinga.
 
Kwanini atangaze watu kubeba Box la kura, Mkuu barafu jambo la kukimbia na Box la kura ni kawaida huko mikoani

Tatizo DSM hamjui Ndio mmejifunza, Kuna kipindi huwa kura zinafichwa kwenye siti ya dereva pale chini

Sisi wazee wa Political vote Impact analysis ndio watoa mbinu

Tuna mbinu nyingi Sana nyingine tunawatumia akina Mama wajawazito kama maofisa wa kusimamia kumbe wanavaa nguo ndani wamejaza kura

Haya mambo sisi tumesomea, Tunaangalia kama Risk italeta faida tunatekeleza mtalia Sana

Nitawapa mbinu zaidi
siyo kitu kizuri ila nimecheka sana
 
Ukawa Kwa habari Za kufikirika na kujitungia! Asa huyo dogo awindwe Kwa lipi. Bora ungemwambia mbowe aliyesababisha Fujo Hadi mtu kafa

we nae akili huna kabisa yn...Umewah kuona Duniani Fujo zikitatuliwa na risasi??? Hv unajua ni mazingira gani yanayo mruhusu askari kutumia risasi??? Acha ushabiki
 
Hilo la box la kura eti kuibiwa ni uzushi mkubwa mno....Chadema hiki hakikukosi kutunga uongo kila siku...box liibiwe ili iwe nini??? Tanzania hii hatujafikia hukokuiba box la kura....

Hilo la kuibiwa kwa box la kura sio kwamba hapa tunauliza ni ukweli ama uongo bali ndio ukweli wenyewe, ila haikutakiwa kusemwa maana wananchi watazidi kupoteza hata imani ndogo waliyo nayo. Halafu sio hilo tu la box la kura, bali kuna mengi mengine ya hivyo yalitokea na hayakuruhusiwa kuripotiwa. Usipoteze muda wako kudhani utapotosha ukweli ulio wazi we dingi.
 
Spencer Lameck kuwa makini kuanzia sasa na nyendo zako,kuna watu "wanakuwinda".Sina namna ya kukupata ili nikupe ujumbe huu,lakini napitia JF kukupa "tetesi" kuwa uwe makini,kuna watu "wanakuwinda".

Hawajaanza jana kukuona kama ni "kauzibe" kwao,walianza kuona hauko upande wao toka wakati wa uchaguzi mkuu,team ya kampeni ya "chama dume" kitengo cha Habari na Mawasiliano kilichokuwa kionaongozwa na Mkuu wa Wilaya wa sasa wa Longido,katika majumuisho yao ya kila siku juu ya mwenendo wa kampeni,iliona mtangazaji wa ITV aliyeambatana na Mzee wa Monduli ndio "kikwazo" kwao.

Namna ulivyouhabarisha umma,kwa "mbwembwe" na "bashasha" juu ya kuchanja mbuga katika milima na mabonde kwa mgombea wa chama kingine,ilikuwa kikwazo kwa upande wa pili.

Iliundwa team maalumu kuhakikisha kuwa katika vyombo vya habari vinavyotazamwa sana kama ITV(kwa wakati ule wa 2015),habari za mgombea wao zipate zishereheshwe sana wakati wa taarifa ya habari.

Kwa upande wa "chama dume" mwandishi wa ITV alikuwa Emmanuel Buhohela na upande wa pili alikuwa Spencer Lameck.Huyu Buhohela "alikamatwa" vizuri sana na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Habari wa CCM wa wakati huo ambaye kwa sasa ni mkuu wa Wilaya ya Longido Mh.Daniel Chongolo.Baada ya uchaguzi,Emanuel Buhohela akapata kazi Ikulu,na sasa yupo kwenye kitengo cha Kurugenzi ya Habari Ikulu iliyo chini ya Msigwa na Jaffari Hanyuu(?) ambaye wakati wa uchaguzi alikuwa anaripoti toka TBC One.

Ahadi kubwa kwa Buhohela ilikuwa ni kuhakikisha anampamba na kumremba vizuri mgombea wao,na baada ya uchaguzi "atafikiriwa",na kweli alifikiriwa.Huyu Spencer Lameck hakutoa ushirikiano kila alipojaribiwa "kuhujumu" taarifa za upande aliokuwepo.Huyu Spencer ndio aliibuka na msamiati wa "mafuriko"...Kila ikifika saa mbili,alitupasha juu ya "mafuriko" ya EL.Mafuriko yalehumtesa mtu fulani mpaka kesho.

Huyu Lameck aliwaudhi watu kwa muda mrefu,walikuwa wanakosa sababu ya haraka(immediate Cause),ila sasa wameipata.

Mkutano wa kwanza wa waandishi wa habari na Raia namba moja,Spencer Lameck alipata nafasi ya kumuuliza Mheshimiwa swali,na swali lake lilikuwa kwamba,ni vigezo vipi Rais ametumia kuchagua mawaziri katika baraza lake la mawaziri??Mheshimiwa akamjibu kuwa; "Vigezo nilivyotumia ndio vilevile ambavyo boss wako na chombo chako cha habari kimekuteua wewe kuja Ikulu kuchukua hii habari"...lakini "off Camera",jamaa akaongezewa jibu kuwa unaniuliza vigezo??ni vilevile vilivyofanya wewe uchaguliwa ku-report habari za UKAWA.

Habari ya ITV siku ya uchaguzi Kinondoni ya kuonyesha jinsi mtu alivyokimbia na kasha la kura kituo cha Idrissa-Magomeni,limewakasirisha sana watu,limewaudhi na wamedhamiria kumuadabisha mtu,hawakuta ukweli ule ujulikane.Wanataka kumshikisha mtu adabu...Bwana mdogo usidharau,kuwa makini na nyendo zako,jilinde,kuwa na tahadhari.Tumeamua kuandika hapa,ili waone aibu kufanya kile walichopanga kufanya.

ITV wameomba radhi kwa mtangazaji wao Spencer Lameck kutangaza habari ya makasha ya kura kuibiwa pale Magomeni.Si kwamba ni habari ya uwongo,ila wanasema ni habari iliyoleta "usumbufu" kwa watu wengine.

Mwanangu na kijana wangu Spencer Lameck,tangu sasa...Chunga mienendo na maeneo unayotembelea.Tupo katika kipindi cha kupeana tahadhari kwa kila tunalolitenda.Ubarikiwe.
Huyu alikuwepo kwenye ile list niliyoipata 2015 'wanted' akiwemo na John Mrema
 
Mtangazaji kama yule nani atamlinda? Ni raia kama mimi na wewe ...kama bosi wake kaomba radhi then yeye atakuwa na hali gani? Tunajenga Taifa gani?

Mmmhh, mkuu kuna jipya kwa hili la haya aliyosema barafu!!!? Mkuu hili taifa kwa sasa ndio linajengwa kwa usahihi kwa haya yanayoendelea.
 
Kwa kweli Spsncer anakera .Anajifanya mjuaji sana pamoja na mwanadada Jackline Silemu.Hawa ni sumu kwa usalama wetu wa ndani.Walikuwa wamedhamiria hasa kulipaka taifa matope na huku wakitumia wachambuzi wao waliowapanga akina Dr. G.Kahangwa ili kutimiza azma yao na kuituhumu tume ya uchaguzi kwamba ni ya ovyo mbele ya macho na masikio ya watanzania.Watangazaji hawa na jazba zao za kisiasa hawafai.Wasifukuzwe kazi ila wapewe kazi nyingine kwenye hiyo kampuni yao .Naamini kazi zipo nyingi huko.
 
Ww ni wa kitengo, tume au tokea chamani uliye zamu kuhakikisha unapotosha kila ukweli unaosemwa humu jukwaani? Taifa linapakwa matope au lina matope tayari? Mkuu hakuna kitu kigumu kama kuvuta riziki kwa kamba.
 
Back
Top Bottom