Mtandao wamuweka Kikwete njia panda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtandao wamuweka Kikwete njia panda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nguvumali, Dec 16, 2009.

 1. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #1
  Dec 16, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Chanzo: Raia Mwema


  WAKATI Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikisubiri matokeo ya kamati teule ya rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, habari zinasema kwamba Rais Jakaya Kikwete anajipanga kuingia katika uchaguzi wa mwakani bila ya mtandao 'uliomsaidia' mwaka 2005 kwa vile amegundua unaweza kumponza. Hiyo inafuatia mtafaruku ndani ya CCM unaoelezwa unachochewa zaidi na Katibu Mkuu wake, Yusuf Makamba kwa upande mmoja, mivutano ya makundi ndani ya mtandao wa 2005 na mfumo wa Rais wa kuchelea kuwaudhi baadhi ya watu, Raia Mwema imeambiwa.

  Taarifa zilizothibitishwa na baadhi ya watendaji wa karibu na Rais zinaeleza kuwa, hakuna uwezekano wowote kwa Rais Kikwete kubwaga manyanga katika Uchaguzi Mkuu mwakani na ameanza harakati za kujihakikishia kurejea Ikulu, akikwepa rekodi ya kuwa Rais aliyekaa madarakani muda mfupi kuliko masharti ya Katiba.

  Taarifa za kiintelijensia zinaeleza kwamba tayari Kikwete amekwisha kuanza kufanya mikakati ya chini kwa chini ikiwa ni pamoja na kuandaa makundi ya vijana ambao wameanza kuahidiwa nafasi kadhaa za kisiasa na kiutendaji baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2010 kama njia ya kuwafanya wawe watiifu kwake..."

  kwa maoni yangu JK HAWEZI KUINGIA KWENYE UCHAGUZI BILA KUTEGEMEA HIVI VIKUNDI NA BADALA YAKE AKATUMIA MAKADA WA PALE MAKAO MAKUU ILI KUEOUSHA KULIPANA FADHILA HUKO MBELENI, je taifa linamuhitaji Rais mwenye ubia na wakora bado ?
   
 2. l

  libaba PM Senior Member

  #2
  Dec 16, 2009
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nguvumali nakuambia Nguvu za Kikwete ni marafiki zake, nahisi ni muoga sana huyu jamaa.
   
 3. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145


  Teh teh teh wangwana sina shaka kwa yeye kuanza kujidhatiti nyakati hizi, ila kama kweli unayoyasema now now ndio anayotaka kuyafanya kulipa fadhili atakuwa karudia kosa lile lile la wanamtandao, weka mtu toka na utendaji kazi wake na si tuu ati alikuwa kada mzuri katika kampeni na ukashinda katka jimbo lake sasa anstahili kupewa ukatibu wizarani.

  Kwanini this time watu wasisimame bila pesa wajinadi na kuangalia elimu zao na utendaji kazi wao na nidhamu zao na maadili yao ya uongozi tuone kama nchi itaenda kubaya hapa bila sahau kulekebishwa kwa katiba kuwe mstari wa mbele ili sheria ifuate mkondo wake.
   
 4. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Without UFISADI, No kikwete
   
 5. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kwa kuanza kuandaa vijana na kuwaahidi madaraka, haitatofautiana na alichokifanya mwaka 2005, akatuongezea umaskini nchini. Yeye afanye kazi yake vizuri, wananchi waone mchango wake, ili watu ndo wamchague, na viongozi wa kumsaidia awachague kutoka kokote, bila kujali alimsaidia kupata urais or not, bali azingatie ukweli kwamba anayemuweka madarakani ni mchapa kazi. I think hiyo itasaidia.
   
 6. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  "ameanza harakati za kujihakikishia kurejea Ikulu, akikwepa rekodi ya kuwa Rais aliyekaa madarakani muda mfupi kuliko masharti ya Katiba."

  Kwani masharti ya katiba yamesema muda gani? Au ni katiba ipi inayo ongelea(ya nchi au CCM?)? Maana kwa nijuavyo katiba ya nchi inasema raisi ana ongoza kwa muda wa miaka mitano halafu agombee kipindi cha pili. Hata kwa CCM sidhani kama katiba inasema raisi lazima atapewa kugombea kipindi cha pili bali ni utaratibu tu.
   
 7. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  just discussing the obvious does not change anything

  Kila mtu anajua kwamba hakuna kitu kitamzuia rais kugombea mwakani zaidi ya kifo finito

  wapinzani wamwandae mtu wao wapambane kelele hazisaidii
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Dec 17, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  "Tanzania Daima linatoa taarifa ya kuwapo kundi jipya linalodhamiria kuchukua nafasi ya mtandao wa 2005 ili kuhakikisha kua JK anarejea madarakani, na wameanza tayari harakati za kushambulia kila anayeonekana kuleta upinzani, wanayatumia sana magazeti , radio na TV ambazo zitzwapumbaza watu kua JK NI MTU WAAKURUDI MADARAKANI....."

  Sasa kinachonishangaza bado ni kweli JK hajajifunza athari za makundi haya katika maendeleo ya TZ, Mpaka leo hajaona nnchi alivyoiweka rehani kwasababu ya fadhila ilizompasa kulipa kwa marafiki na washikaji zake, kweli sielewi uwezo wakuyatazama mambo ya bwana mkubwa wetu pale kitalu namba 1.
   
 9. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #9
  Dec 17, 2009
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  anatengeneza kundi jinginie!!!??? aisee,kuna kitu atajifunza soon.
   
 10. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #10
  Dec 17, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  ..."

  Ukishafanya kosa moja ni rahisi kufanya la pili na la tatu. Kazi ipo! Haya makundi wanayoyaunda haya huwa hayana interest na Taifa. Yana interest zao binafsi ingawa gharama yake ni Taifa zima huwa linalipia.JK angalia tena strategies zako..zisije zikafanana na zile za Hitler kule Stanligrad.
   
 11. b

  bigilankana Senior Member

  #11
  Dec 17, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  uvivu wetu tu wa kujisomea. Duniani kote hakuna chama cha siasa kisicho na factions - mitandao. Soni la maana katika hili la JK. Makundi ya CCM yanashindana tu kuwa nyuma ya JK kwa ajili ya kujipanga kuelekea 2015. Hiyo ndio common denominator.

  Waliapa watamfanya ashindwe kutawala na wamefanikiwa. Sasa wanajipanga. Uzushi mwingiiiiiiiiii. Eti hawataki agombee tena, ajabu kweli. Kama humtaki mtu si mnanyima kura tu badala kumzuia kugombea. Kumzuia kugombea ni kumwogopa.

  Eti hata CUF wanasema, CCM wasimteue Kikwete. Sasa kama kashindwa kazi si wamteue huyo ili Lipumba amshinde? Siasa za Tanzania vituko vitupu
   
 12. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #12
  Dec 17, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  hapa kuna mambo mawili ambayo Jk kama hajakuwa makini yatatokea1) siku zote kama unatatizo inabidi utulie na kuja ulishemsha wapi na hata kama ukiomba ushauri sio shida, lakini unaweza ukakurupika na solution ambazo zitasababisha matatizo kuliko hata yale ya mwanzo, Naona JK ndio yupo kwenye hii stage ya kutatua matatizo kwa kucreate matatizo zaidi, maana kama kulipa fadhira ndio kukubari kuzaririshwa namna ile na kina Simba, Makamba nk, sasa baada ya kujisafisha anataka kutafuta tope jingine ili ajipake zaidi2) cha pili ambacho nina wasiwasi nacho ni hiki cha kuanza kampeni na kuandaa makundi wakati kuna issue serious za kuzisolve, jamaa ana miaka minne hakuna hata kimoja anachoweza kutuonyesha alichokifanya, hali ya maisha inazidi kuwa ngumu, shule , matibabu vyote ni karaa, nadhani kama hajakuwa makini anauwezo wa kuripeleka taifa kwenye stage ambayo sidhani kama watu watakuja kumsahau</p>
   
 13. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #13
  Dec 17, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
 14. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #14
  Dec 17, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Inawezekana ni kweli kua WaTz ni wavivu kujisomea,
  ninachowaza ni kua JK AMESHINDWA KUJINASUA NA NGUVU ZA MITANDAO ALIYOIUNDA 2004/05, Kilichotokea kipindi chote kuanzia lile baraza la mawaziri kubwa kuliko yote tangu UHURU hadi sasa ni kulipana fadhila kwa kila juhudi na jitihada zilizofanywa katika kampeni, na hiyo ndio iliowaleta kina NNCNIMBI,Bangusilo,Kingunge,Mahanga,Sofia Simba nawengine madarakani.
  Obama alikua na mtandao, lakini hata mara moja hakuna anaehoji uteuzi wa watendaji wake, JK tangu mara ya kwanza tu alipotaja baraza lile kituko watu walishangaa namna alivyotapanya vyeo kwa misingi ya fadhila, hebu nambie Adam Malima anasifa ipi kustahili kushika wadhifa ule, ni moja kati ya teuzi za ovyo.
  sasa WATZ wanapohoji juu ya kuendekeza makundi ya hivi unawez kwa akili ya haraka haraka usione athari yake, ila nnchi hii imefika hapa kwa athari kubwa za kimtandao....
  mwangalie Mkurugenzi wa habari wa Ikulu Salva RWEYEMAMU, alikua katibu wa mtandao, akamteua kuwa mkurugenzi wa habari Ikulu wakati toka mtaani, wakati katika system kuna watu kadhaa wenye sifa wamebaki wakishangazwa na uteuzi huo hadi leo, nenda pale Wizara ya Habari kaulize.
  hayo yote ni matokeo ya kulipa fadhila.
  Mtandao bado naamini utamuingiza matatizoni zaidi yeye mwenyewe na Tanzania yetu iwapo tu ataingia madarakani tena 2010..maana hana ubavu wakukemea marafiki hivyo ni bora akajitenga nao.
   
 15. l

  libaba PM Senior Member

  #15
  Dec 18, 2009
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  i agree with u Nguvumali
   
 16. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #16
  Dec 18, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mtandao ndo nguvu ya JK kwani umemwezesha kuwa RAISI WA JAMHURI YETU PENDWA YA TANZANIA..

  Kumbuka Dodoma baada ya kutangazwa mshindi alitoa machozi ya furahaa akielekeza mikono yake juu na kuwatizama wanamtandao waliokuwa wanamshangilia kwa KUKAMILISHA KAZI...Kwa jeuri alitamka sasa KURA ZIMETOSHA...
   
 17. l

  libaba PM Senior Member

  #17
  Dec 18, 2009
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hapo ndipo penye shida ambapo WaTz wanapaswa kugundua kua Rais wao hajiwezi bila nguvu za hawa watu wanaojiita mtandao
   
Loading...