Himalaya
Senior Member
- Mar 27, 2019
- 174
- 276
NAHISI KUNA BAADHI YA KUMPUNI NI CHUMA ULETE
Jana nilishawishika kununua Router kwa ajili ya matumizi ya kiofisi. Katika zunguka zunguka nikatumbukia kwenye kampuni ya Smile. Nikaelimishwa juu ya routers zao nikashawishika kununua moja. Kwakweli Routers zao ni nzuri sana na ni 4G. Zina kasi ya kufa mtu na kwahakika zinafaa sana kwa matumizi ya kiofisi. Lakini tatizo leo hawa jamaa wako so expensive kwenye Bundle zao kwa mfano bundle ya GB1 inauzwa kwa TZS 5000 na ukiweka bundle hilo utastaajabu ndani ya saa moja kwisha kabisa na ni matumizi ya kawaida tu.
Jana nililazimika kununua kifaa hiki kwa ajili ya matumizi ya kiofisi. Nikapewa GB 1 ya ofa, na mimi nikanunua bundle ya mwezi ya TZS 25000 na nikapewa GB 5 ukiplus na ile GB 1 ya offer nikapata GB 6. Sasa cha ajabu nilipoanza tu kuitumia chini ya masaa 24 bundle lote kwisha. Wakati mimi nilijua nitatumia mwezi mzima lakini wapi hola. Nikawaendea wakaniambia eti matumizi yangu ni makubwa wakati matumizi yangu ni yaleyale ya kiofisi tu kutuma email, kutafuta taarifa mbalimbali kwenye mitandao na wakati mwingine kurefresh youtube kidogo kitu ambacho nilikuwa nikikifanya before nikiwa na line yangu ya airtel ikiwa na GB 1 tu. Siku nikiamua kununua bundle la mwezi la GB 5 kwa TZS 15000 inakwenda mwezi mzima lakini kwa Smile licha ya bundle zao kuwa ghali hazikai zinawahi sana kuisha.
Baada ya kuisha lie bundle Mwezi, nikasema nifumbe macho, nijiribu tena kununua bundle la GB 1 kwa TZS 5000, ilikuwa majira ya saa 11: 02 lakini ilipofikia saa 12: 30 jioni ya leo bundle lote limekatika na sijaingia hata youtube zaidi ya matumizi ya kawaida tu ya kuperuzi kwenye mtandao wa Internet na kujifunza mambo kadhaa bila kudownload japo pdf poja.
Kwa siku mbili za matumizi ya kifaa hiki kwa hakika nimwanyoshea mikoni na siwataki tena, na nitakapi kwenye draw hadi watakapojirekebisha vinginevyo sitatoa tena hela yangu kununua bundle mana naona hawa jamaa wana kila dalili ya uchuma ulete.
Byebye Smile, sina hela ya kuchezea.
Aman Ng'oma
0767989713
DODOMA
C&P