Mtambuzi mie, nishageuka Simba Mzee mchezewa sharubu...!

Mtambuzi mie, nishageuka Simba Mzee mchezewa sharubu...!

Kwa mnyamanyi

Kama huko mbali tukutane hata Thai Village sawa? Nimekumisije

Lucas poa zaidi,si unajua samaki wao wa kuchoma alivyo mtam?
I miss you too.
Kopi aione zombie...ujumbe: imekula kwako chezeiya bilionea la kihaya likitia timu vidampa wote mnapeperuka....dadadadeki!
 
afadhali tupumuwe,maana tungekuwa tunagongana mara leaders club,mara bilicana,mara maisha club sijui ingekuwaje?
 
Mtambuzi nashukuru kwa chansi nyenginewd maridhawa ulonipatia kuchezea sharubu hizo...

Wewe Paloma wewe.. Hebu njoo ulale huku.. Nshakuambia huyo Mtambuzi anatumia mbinu ya kujifanya Simba zee kumbe ndo anaekula nyama.. Unadhani kwamba kuna ukweli ati anachezewa sharubu halafu asiumizwe huyo azichezeae..
 
Last edited by a moderator:
03_01_89346b.jpg


Ama kweli siku hazigandi, alijiimbia Lady JD.
Nikikumbuka miaka ile nikiwa kijana shababi mwenye siha nzuri, kipindi hicho, mkate wa Boflo kwa mpemba ulikuwa unauzwa hela kumi. Wakati huo sijakutana na Mama Ngina, wala hawa wanangu King'asti na Asnam hawajulikani duniani nilitesa sana na vibinti.

Nakumbuka wakati huo mabinti walikuwa wanatokelezea na magauni yao ya vitambaa vya Polister, Criplin au Chirmen walivyonunua kwa washihiri, wakati huo vitambaa vilikuwa vinapimwa kwa kipimo maarufu cha ZIRAA.

Nilikuwa kama Helikopter ndege isiyochagua mahali pa kutua. mambo yangu yalikuwa bambam na vijisenti mfukoni havikuwa vya kujibana, yaani nilikuwa nikimhonga mwanamke shilingi kumi atatangaza mtaa mzima. "Baba ana pesa yule kama njugu...!" Atasema kwa mashoga zake, kumbe ndio alikuwa ananipigia upatu, mabinti kuniwania.....

Sasa kiko wapi?

Mtambuzi nishageuka Simba Mzee aliyeshiba mizoga, vitoweo vinanichezea sharubu, mwenyewe nimebaki kuvikodolea macho. Nitoe wapi nguvu ya kuhimili sarakasi za mabinti wa siku hizi ambao wanataka kugeuzwa geuzwa kama samaki kikaangoni.

Kwa bahati mbaya sana mazingira ya kazi yangu achilia mbali hapa kazini kwangu kazi ninayofanya hunikutanisha na vimwana walioumbwa wakaumbika, na kujipamba na lebasi za ulimbwende pamoja na makochokocho chungu mzima. Ukichanganya na vivazi wanavyovaa, Oh mai.........! Utashangazwa na uumbaji wa Mwenye enzi Mungu.

Kutokana na macho yangu kukaa kihayawani. Ama kweli macho ya muasherati yana hila mbaya, hivi sasa nina bahati mbaya ya kusingiziwa na mabinti kuwa nawatongoza. Yaani nikizungumza na binti yeyote hapa kazini au popote pale huishia kunisingizia eti nimemtongoza...!

Hivi sasa hapa kazini kuna vita baridi miongoni mwa mabinti wakitupiana vijembe. Si mnawajua wanawake kwa mipasho...! Hivi majuzi wawili wametiana vidole vya macho, lahaula, kesi imefika kwa Meneja Rasilimali Watu. Mara simu hiyo napigiwa, mie huyo kwa Meneja Rasilimali Watu, nikijua tunaenda kuzungumzia mambo ya mafunzo kazini. He! Nafika, nakutana na mabinti wametumbuliana macho kama kuku mitetea inayogombea Koo (Jogoo).

Kesi iko Kilingeni.......

Hivi hawa mabinti wananitafutiani...?

Salaam hizi ziwafikie wapendwa wote wanaonitakia mema.... Raiza, Paloma, Zion Daughter, Asnam, Kipipi, King'asti, Lisa, Nivea, cacico, Elizabeth Dominic, charminglady, lara 1, Mrembo by Nature, vivian, Lusile, Jeska, Binti.com, Remmy, sweetlady, FirstLady1, FirstLady, MwanajamiiOne, Husninyo, Mamndenyi, mwaJ, Swts, Madame B, MadameX, Angel Msoffe, snowhite, gfsonwin, Preta, Nyamayao, marejesho, Asprin, Mwita Maranya, SnowBall, Roulette, jouneGwalu, HorsePower, Mungi, Erickb52, Don Mangi, Thomas Odera, Kipaji Halisi, Mentor, Kiranga, Nyani Ngabu, Bujibuji, Arushaone, Mzee mwenzangu Babu DC Dark City

salamu pia zinifikie na mimi kalou
 
Hahaaaa,
Mkuu umenifanya ncheke sana. Siwezi kuvumilia mzee wangu ukichezewa namna hii. Hakuna nafasi ya kujitolea hapo mkuu nikaribie?

Bcc:snowhite

[Mtambuzi nishageuka Simba Mzee aliyeshiba mizoga, vitoweo vinanichezea sharubu, mwenyewe nimebaki kuvikodolea macho. Nitoe wapi nguvu ya kuhimili sarakasi za mabinti wa siku hizi ambao wanataka kugeuzwa geuzwa kama samaki kikaangoni]
 
Hahahahaaa.......Simba zee halina nyimbo. Viswala vyajipitisha viliwe shuti kupigana vyenyewe kwa vyenyewe

:A S shade::A S shade::A S shade:

Sema jamani Kaizer.....mi mwenzenu nyie misimba msioweza hata kuunguruma naipenda.......lini utakuja nichezee sharubu

khaaaa Elizabeth Dominic mi kwani nimesema ni kama simba.. Mtambuzi peke yake....ila kama kuchezea sharubu sawa ninazo za kuchezea..in two weeks time...okay? LOL

Hahaha....utasema?......anyways karibuu.....ntazichezeaje.........yeeeey

:A S-coffee:................:lalala:

:welcome::focus:
 
baba mkwe mtambuzi pole
ujana walo ulishaufaidi vizuri
kwa sasa ni zamu yetu na sie,
nimecheka sana kujua vimbwanga vyako
 
Ndio maana sipuuzi hizi semi kuwa vunja mifupa ukiwa na meno...
Siku hizi vijana tumekalia sijui site, sijui kujenga... sijui tukishachoka tutakuwa tunafanya nini...
 
Mtambuzi nishageuka Simba Mzee aliyeshiba mizoga, vitoweo vinanichezea sharubu, mwenyewe nimebaki kuvikodolea macho. Nitoe wapi nguvu ya kuhimili sarakasi za mabinti wa siku hizi ambao wanataka kugeuzwa geuzwa kama samaki kikaangoni.

Kutokana na macho yangu kukaa kihayawani. Ama kweli macho ya muasherati yana hila mbaya, hivi sasa nina bahati mbaya ya kusingiziwa na mabinti kuwa nawatongoza. Yaani nikizungumza na binti yeyote hapa kazini au popote pale huishia kunisingizia eti nimemtongoza...!

ngoja hao mabinti waje wadhibitishe kupinduliwa pinduliwa kama chapati

hayo macho ulizaliwa yakiwa kiyahawani hivyo hivyo au baada ya kukua ndio umeyageuza ya kihayawani??
 
Back
Top Bottom