Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,441
Ama kweli siku hazigandi, alijiimbia Lady JD.
Nikikumbuka miaka ile nikiwa kijana shababi mwenye siha nzuri, kipindi hicho, mkate wa Boflo kwa mpemba ulikuwa unauzwa hela kumi. Wakati huo sijakutana na Mama Ngina, wala hawa wanangu King'asti na Asnam hawajulikani duniani nilitesa sana na vibinti.
Nakumbuka wakati huo mabinti walikuwa wanatokelezea na magauni yao ya vitambaa vya Polister, Criplin au Chirmen walivyonunua kwa washihiri, wakati huo vitambaa vilikuwa vinapimwa kwa kipimo maarufu cha ZIRAA.
Nilikuwa kama Helikopter ndege isiyochagua mahali pa kutua. mambo yangu yalikuwa bambam na vijisenti mfukoni havikuwa vya kujibana, yaani nilikuwa nikimhonga mwanamke shilingi kumi atatangaza mtaa mzima. "Baba ana pesa yule kama njugu...!" Atasema kwa mashoga zake, kumbe ndio alikuwa ananipigia upatu, mabinti kuniwania.....
Sasa kiko wapi?
Mtambuzi nishageuka Simba Mzee aliyeshiba mizoga, vitoweo vinanichezea sharubu, mwenyewe nimebaki kuvikodolea macho. Nitoe wapi nguvu ya kuhimili sarakasi za mabinti wa siku hizi ambao wanataka kugeuzwa geuzwa kama samaki kikaangoni.
Kwa bahati mbaya sana mazingira ya kazi yangu achilia mbali hapa kazini kwangu kazi ninayofanya hunikutanisha na vimwana walioumbwa wakaumbika, na kujipamba na lebasi za ulimbwende pamoja na makochokocho chungu mzima. Ukichanganya na vivazi wanavyovaa, Oh mai.........! Utashangazwa na uumbaji wa Mwenye enzi Mungu.
Kutokana na macho yangu kukaa kihayawani. Ama kweli macho ya muasherati yana hila mbaya, hivi sasa nina bahati mbaya ya kusingiziwa na mabinti kuwa nawatongoza. Yaani nikizungumza na binti yeyote hapa kazini au popote pale huishia kunisingizia eti nimemtongoza...!
Hivi sasa hapa kazini kuna vita baridi miongoni mwa mabinti wakitupiana vijembe. Si mnawajua wanawake kwa mipasho...! Hivi majuzi wawili wametiana vidole vya macho, lahaula, kesi imefika kwa Meneja Rasilimali Watu. Mara simu hiyo napigiwa, mie huyo kwa Meneja Rasilimali Watu, nikijua tunaenda kuzungumzia mambo ya mafunzo kazini. He! Nafika, nakutana na mabinti wametumbuliana macho kama kuku mitetea inayogombea Koo (Jogoo).
Kesi iko Kilingeni.......
Hivi hawa mabinti wananitafutiani...?
Salaam hizi ziwafikie wapendwa wote wanaonitakia mema.... Raiza, Paloma, Zion Daughter, Asnam, Kipipi, King'asti, Lisa, Nivea, cacico, Elizabeth Dominic, charminglady, lara 1, Mrembo by Nature, vivian, Lusile, Jeska, Binti.com, Remmy, sweetlady, FirstLady1, FirstLady, MwanajamiiOne, Husninyo, Mamndenyi, mwaJ, Swts, Madame B, MadameX, Angel Msoffe, snowhite, gfsonwin, Preta, Nyamayao, marejesho, Asprin, Mwita Maranya, SnowBall, Roulette, jouneGwalu, HorsePower, Mungi, Erickb52, Don Mangi, Thomas Odera, Kipaji Halisi, Mentor, Kiranga, Nyani Ngabu, Bujibuji, Arushaone, Mzee mwenzangu Babu DC Dark City