Mtambuzi mie, nishageuka Simba Mzee mchezewa sharubu...!

Mtambuzi mie, nishageuka Simba Mzee mchezewa sharubu...!

You dont make any sense!!! unahitaji kurudia mtihani pia wa fomfoo!

next kweshen - unapata script gani KakaKiiza?!?!
Nilete fomu nijaze!ila wewe umekalili kuwa lazima mtu ale ndo aishi wakati sikuizi ni ishi ndo ule!
 
Nilete fomu nijaze!ila wewe umekalili kuwa lazima mtu ale ndo aishi wakati sikuizi ni ishi ndo ule!

si ndo mana nikasema izi ni asali za hamimu mulugo............natakiwa niludie mtiani wa dalatha la thaba, na elowai (fom foo) kujaza fomu pia utata!
 
Last edited by a moderator:
03_01_89346b.jpg

Ama kweli siku hazigandi, alijiimbia Lady JD.
Nikikumbuka miaka ile nikiwa kijana shababi mwenye siha nzuri, kipindi hicho, mkate wa Boflo kwa mpemba ulikuwa unauzwa hela kumi. Wakati huo sijakutana na Mama Ngina, wala hawa wanangu King'asti na Asnam hawajulikani duniani nilitesa sana na vibinti.

Nakumbuka wakati huo mabinti walikuwa wanatokelezea na magauni yao ya vitambaa vya Polister, Criplin au Chirmen walivyonunua kwa washihiri, wakati huo vitamba vilikuwa vinapimwa kwa kipimo maarufu cha ZIRAA.

Nilikuwa kama Helikopter ndege isiyochagua mahali pa kutua. mambo yangu yalikuwa bambam na vijisenti mfukoni havikuwa vya kujibana, yaani nilikuwa nikimhonga mwanamke shilingi kumi atatangaza mtaa mzima. "Baba ana pesa yule kama njugu...!" Atasema kwa mashoga zake, kumbe ndio alikuwa ananipigia upatu, mabinti kuniwania.....

Sasa kiko wapi?

Mtambuzi nishageuka Simba Mzee aliyeshiba mizoga, vitoweo vinanichezea sharubu, mwenyewe nimebaki kuvikodolea macho. Nitoe wapi nguvu ya kuhiminili sarakasi za mabinti wa siku hizi ambao wanataka kugeuzwa geuzwa kama samaki kikaangoni.

Kwa bahati mbaya sana mazingira ya kazi yangu achilia mbali hapa kazini kwangu kazi ninayofanya hunikutanisha na vimwana walioumbwa wakaumbika, na kujipamba na lebasi za ulimbwende pamoja na makochokocho chungu mzima. Ukichanganya na vivazi wanavyovaa, Oh mai.........! Utashangazwa na uumbaji wa Mwenye enzi Mungu.

Kutokana na macho yangu kukaa kihayawani. Ama kweli macho ya muasherati yana hila mbaya, hivi sasa nina bahati mbaya ya kusingiziwa na mabinti kuwa nawatongoza. Yaani nikizungumza na binti yeyote hapa kazini au popote pale huishia kunisingizia eti nimemtongoza...!

Hivi sasa hapa kazini kuna vita baridi miongoni mwa mabinti wakitupiana vijembe. Si mnawajua wanawake kwa mipasho...! Hivi majuzi wawili wametiana vidole vya macho, lahaula, kesi imefika kwa Meneja Rasilimali Watu. Mara simu hiyo napigiwa, mie huyo kwa Meneja Rasilimali Watu, nikijua tunaenda kuzungumzia mambo ya mafunzo kazini. He! Nafika, nakutana na mabinti wametumbuliana macho kama kuku mitetea inayogombea Koo (Jogoo).

Kesi iko Kilingeni.......

Hivi hawa mabinti wananitafutiani...?

Salaam hizi ziwafikie wapendwa wote wanaonitakia mema.... Raiza, Paloma, Zion Daughter, Asnam, Kipipi, King'asti, Lisa, Nivea, cacico, Elizabeth Dominic, charminglady, lara 1, Mrembo by Nature, vivian, Lusile, Jeska, Binti.com, Remmy, sweetlady, FirstLady1, FirstLady, MwanajamiiOne, Husninyo, Mamndenyi, mwaJ, Swts, Madame B, MadameX, Angel Msoffe, snowhite, gfsonwin, Preta, Nyamayao, marejesho, Asprin, Mwita Maranya, SnowBall, Roulette, jouneGwalu, HorsePower, Mungi, Erickb52, Don Mangi, Thomas Odera, Kipaji Halisi, Mentor, Kiranga, Nyani Ngabu, Bujibuji, Arushaone, Mzee mwenzangu Babu DC Dark City

Mkuu Mtambuzi nimequote yote kuonyesha furaha yangu kwa lugha iliyotumika . Yaani imeshiba sana na imejaa nahau na misemo ya kufurahisha, kufikirisha, kufundisha nk.

Waalimu wa kiswahili mumwombe Mtambuzi awaruhusu kuitumia hii kufundishia tupunguzw F za kiswahili jamani.
KakaKiiza ameongelea uhalali wa maudhui mimi huko sitaki kabisa.

Cc: gfsonwin snowhite Madame B Baba V Asprin Paloma Raiza
 
Last edited by a moderator:
[B Paloma, nadhani mzee wa experience a.k.a uzoefu atakusaidia zaidi, mimi ni mwanafunzi wa Asprin kwenye masuala ya ukaguzi..unless zat is wat yu nid:-*
[/B]

sosoliso, akitajwa 'mkeo' ni sawa na wewe umetajwa...

na mbona hiyo 'mkeo' imekaa kiutata Mentor..? bado sijamuelewa Mtambuzi kuniweka kwenye ubaya na wakati huo huo kumuweka mai waifu Paloma kwenye uzuri..! hapa lazima kuna jungu linatengenezwa.. Mtambuzi haaminiki wala kukubalika na ndo maana amekuja kuomba suluhu hapa..
 
Mkuu sosoliso, mbona una NONGWA hivi kama KakaKiiza...
Hebu tulizana basi, nipate kupumuwa maana ukiona mtu mzima anapiga mayowe basi ujue wamemshika pabaya..

Ngona nikahudhurie kikao cha kesi yangu kwa Meneja Rasilimali Watu ili kulinda kibarua changu kisije niponyoka..

Naomba mniombee..... LOL
 
Last edited by a moderator:
na mbona hiyo 'mkeo' imekaa kiutata Mentor..? bado sijamuelewa Mtambuzi kuniweka kwenye ubaya na wakati huo huo kumuweka mai waifu Paloma kwenye uzuri..! hapa lazima kuna jungu linatengenezwa.. Mtambuzi haaminiki wala kukubalika na ndo maana amekuja kuomba suluhu hapa..

Sasa wasiwasi wako ni nini ndugu maana mwenyewe ameshakiri kuwa anaishiwa kushikiwa sharubu, kwaiyo 'mkeo' yuko salama akiwa na Mtambuzi.

Be really worried siku akikuambia yuko na mimi, halafu umuulize mnafanya nini akujibu, "nothing"...BE REALLY WORRIED!!!

We are experts in doing nothing.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mtambuzi nimequote yote kuonyesha furaha yangu kwa lugha iliyotumika . Yaani imeshiba sana na imejaa nahau na misemo ya kufurahisha, kufikirisha, kufundisha nk.

Waalimu wa kiswahili mumwombe Mtambuzi awaruhusu kuitumia hii kufundishia tupunguzw F za kiswahili jamani.
KakaKiiza ameongelea uhalali wa maudhui mimi huko sitaki kabisa.

Cc: gfsonwin snowhite Madame B Baba V Asprin Paloma Raiza

Mkuu Kaizer nilikuwa naandika utadhani naandika ngano za kale....

Hata hivyo naamini ujumbe utakuwa umemfikia Meneja Rasilimali Watu hapa kazini kwangu, maana kwa jinsi hali ilivyo naweza kujikuta hata Mimba nasingiziwa.

Ee Mnyazi Mungu niepushie hili balaa...LOL
 
Last edited by a moderator:
Ngoja niendelee na maongezi ya kibiashara na Mkurugenzi wako asije akapita hapo akakuta umesimamishwa na meneja rasilimali watu ikawa tabu.
 
Mkuu Mtambuzi nimequote yote kuonyesha furaha yangu kwa lugha iliyotumika . Yaani imeshiba sana na imejaa nahau na misemo ya kufurahisha, kufikirisha, kufundisha nk.

Waalimu wa kiswahili mumwombe Mtambuzi awaruhusu kuitumia hii kufundishia tupunguzw F za kiswahili jamani.
KakaKiiza ameongelea uhalali wa maudhui mimi huko sitaki kabisa.

Cc: gfsonwin snowhite Madame B Baba V Asprin Paloma Raiza

Mwanafunzi wangu Kaizer, Copy yako nimeipata na nimeihifadhi kwa matumizi ya baadae.

CC: Mdogo wangu Mentor, Usifuate nyayo za kaka yako mkubwa Mtambuzi.
 
Last edited by a moderator:
Sitaki kusema mengi kwa kuwa wewe Mtambuzi ni mzee mwenzangu,

Ila kweli hii ngoma inahitaji wachezaji zaidi ili tujue kulikoni retired officer analia kilioa cha akina dogo...

Nilikuwepo,

Babu DC!!
 
Kaka mkubwa hebu tueleze vizuri aisee.
Mimi huwa ninajua kitu kimoja tu, ni kuwa wanawake wamgombeao mwanaume huwa wanagombea vitu viwili vikubwa.
1. Mali (Fedha inaingia humu)
2. Mpini

Sasa kijogoo wewe wagombewa kwa lipi???
 
Back
Top Bottom