Mtambo wa kuchenjua Makinikia wakamilika kwa asilimia 95%. Watoa suluhu kwa wachimbaji wadogo na wakubwa na kudhibiti wizi wa dhahabu

Hivi si ilisemekana kujenga huo mtambo ni gharama mno na inahitaji muda mrefu,inakuwaje huo uwe tayari mapema hivi?
Waliosema hivyo ni akina Zitto ambao sayansi iliwapita mbali na wakaamua kusomea digrii ya uwongo, Bachelor of Lies in Economics (BLE) degree.
 
Gold smelter syo issue.....
Soon ntafungua Kiwanda kidogo special kwa kuyeyusha tu gold

Siyo utani !

Ova
 
Kudos - Ila kama ka mfano hivi.. Mtambo unatakiwa uwe mkuuubwaa.

Kuna kitu hakiko sawa hapa.

Nadhani taarifa haiko kamili. Inasisitizwa ni mtambo wa kuchenjua dhahabu.

Makinikia, sio dhahabu pekee, kuna slver, copper, cobalt na madini mengine. Kama huu ni wa kuyeyusha dhahabu pekee, ina maana hayo madini mengine, ambayo ndiyo yalikuwa tatizo na makinikia ya Accacia, yatabaki bado hayana mtambo wenye joto zaidi la kuyachenjua.
 
Yenye triple nine? 99.9%? Kama ndio. Hongera.
Serious Nna smelter inachoma mpka nyuzi joto 1800 ......najipanga mdg mdg

Ova
20180915_133617.jpg
 
Mtambo wa Kuchenjua dhahabu uko mbioni kukamilika baada ya kufikia asilimia 95%. Mtambo huo unajengwa katika eneo la Lwamugasa, mkoani Geita.

Waziri wa Madini, Angela Kairuki alisema kuwa, lengo la mtambo huo ni kusaidia wachimbaji wadogo na wa kati lakini pia hata kwa kampuni kubwa zitajazohitaji kuchenjuliwa madini ya dhahabu.

Mtambo huo uliojengwa na Serikali utakuwa chini ya Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) ambao watakuwa wasimamizi wakuu wa mtambo huo.

Hayo ni matokeo ya maagizo ya Rais Magufuli kufuatia mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Kuchunguza Makinikia chini ya Profesa Mruma, iliyoshauri Serikali kujenga mtambo wake wa kuchenjua makinikia ili kuepuka kupoteza kiwango kikubwa cha dhahabu.

View attachment 951068
Hii habari ina ukakasi.....kampuni ya Tan Discovery ndio inajenga?? Smelter imekamilika 95% ndani ya miaka?? Kama Great Thinker bado haijaniingia kichwani.
 
Nyie mnafurahisha sana hebu, tuambie capacity ya huo mtambo, unajengwa na nani? Tends ya kumpata mjenzi ilitangazwa wapi? Bugeti ,yake ilipitishwa na nani??
Hiyo dhahabu mtamuuzia nani?
We jamaa n wewe mawazo yako?
 
“Lengo ni kusaidia wachimbaji wadogo na wa kati lakini pia hata kwa kampuni kubwa zitakazohitaji kuchenjuliwa madini ya dhahabu

Nilidhani kutokana na yale yaliyotokea kwenye sakata la makinikia huo mtambo utakuwa suluhisho... kumbe ni hadi hizo kampuni kubwa zitapohitaji?

Hivi kwa akili ya kawaida hizo kampuni kubwa zinaweza kuhitaji huo mtambo wetu?
Umepotelea wapi au unanyemelea u dc
 
Usiwasikilize hawa waouuzi. Hitaji la kuchanjua makinikia ikikiwa kwaajili ya madini yote na hasa yale yenye dhamani zaidi, na sio dhahabu pekee.

Hii wanayotaka kuifanyia siasa ni ujinga flani. Hiyo mitambo ipo Mara na Mwanza pia.

Propaganda za kishenzi tu hizi.
 
“Lengo ni kusaidia wachimbaji wadogo na wa kati lakini pia hata kwa kampuni kubwa zitakazohitaji kuchenjuliwa madini ya dhahabu

Nilidhani kutokana na yale yaliyotokea kwenye sakata la makinikia huo mtambo utakuwa suluhisho... kumbe ni hadi hizo kampuni kubwa zitapohitaji?

Hivi kwa akili ya kawaida hizo kampuni kubwa zinaweza kuhitaji huo mtambo wetu?
Kampuni kubwa zilizokuwa zinapeleka makemikia nje ili yachenjuliwe huko hawawezi kukuunga mkono hata kidogo.Hawakushindwa kifedha au kitekinologia kujenga mitambo hio hapa.Wao hawana tofauti na kundi la upigaji na uporaji,wao ni waumini wa Africa dark continent.
 
Wachina wana za kuchenjua dhahabu lakini ni ndogo haziwezi kufanya uchenjuaji wa makinikia. Kumbuka makinikia karibia yote huzalishwa katika Mgodi wa Bulyanhulu
Kwani hii smelter yenu inachenjua copper, cobalt, ect...au ninachenjua dhahabu tu?

Kuna vitu havifai kutetea. Ni aibu tu.
 
Nafikiri nimeelewa kuwa mtambo huu ni wa kuchenjua madini ya dhahabu na sii kwa ajili ya makinikia ili kupata zile ingredients nyingine. Kwa hiyo tusichanganye madesa hapa.
Usiwasikilize hawa ngedere....hiyo smelter ipo hata Mwanza na Mara kama sikosei, ni kwa ajili ya dhahabu tu.
 
Ni shauri yao, wasipokuja kwenye mtambo huo itakula kwao kwani kwa sasa hatutaruhusu kupeleka makinikia nje ya Nchi. So wao wataamua ama kusuka au kunyoa.
Huo mtambo umejua uwezo wake??? Stamico kweli wanayopesa ya kuwekeza kitu cha maana kwa muda huu mfupi huu si ujazz band wanatuletea. Mapendekezo ya tipper za dhahabu na Noah vipi.
 
Daaah hizi siasa hizi zinatupeleka vibaya,i know the place na mtambo pia,mtambo ni mdgo na wa kawaida ,old mexican type CIP tanks....hamna kampuni kubwa itakayoenda eti kuchenjua...yaan hawa wanasiasa waongo waongo...mradi ulikuwa under world bank wadhamini wakuu kupitia stamico....hzo CIPs wachimbaji wengi sasa hivi wanazo,umejengwa kama mgodi wa mfano wa wachimbaji wadogo.
 
Mtambo wa Kuchenjua dhahabu uko mbioni kukamilika baada ya kufikia asilimia 95%. Mtambo huo unajengwa katika eneo la Lwamugasa, mkoani Geita.

Waziri wa Madini, Angela Kairuki alisema kuwa, lengo la mtambo huo ni kusaidia wachimbaji wadogo na wa kati lakini pia hata kwa kampuni kubwa zitajazohitaji kuchenjuliwa madini ya dhahabu.

Mtambo huo uliojengwa na Serikali utakuwa chini ya Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) ambao watakuwa wasimamizi wakuu wa mtambo huo.

Hayo ni matokeo ya maagizo ya Rais Magufuli kufuatia mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Kuchunguza Makinikia chini ya Profesa Mruma, iliyoshauri Serikali kujenga mtambo wake wa kuchenjua makinikia ili kuepuka kupoteza kiwango kikubwa cha dhahabu.

View attachment 951068
Kuna kitu bado sijakielewa,huo mtambo utachenjua makinikia ya wachimbaji wadogo pia, hivi mchimbaji mdogo anayo teknolojia ya kuyapata makinikia? Nijuavyo mimi Makinikia yanachenjuliwa ktk mtambo uitwao FLOTATION ambao kwa Tanzania mitambo hiyo ipo ktk Migodi miwili tu ya Bulyanhulu na Buzwagi, Labda mimi ndo sielewi maana ya Makinikia
 
Back
Top Bottom