Mtambo wa kuchenjua Makinikia wakamilika kwa asilimia 95%. Watoa suluhu kwa wachimbaji wadogo na wakubwa na kudhibiti wizi wa dhahabu

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
Mtambo wa Kuchenjua dhahabu uko mbioni kukamilika baada ya kufikia asilimia 95%. Mtambo huo unajengwa katika eneo la Lwamugasa, mkoani Geita.

Waziri wa Madini, Angela Kairuki alisema kuwa, lengo la mtambo huo ni kusaidia wachimbaji wadogo na wa kati lakini pia hata kwa kampuni kubwa zitajazohitaji kuchenjuliwa madini ya dhahabu.

Mtambo huo uliojengwa na Serikali utakuwa chini ya Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) ambao watakuwa wasimamizi wakuu wa mtambo huo.

Hayo ni matokeo ya maagizo ya Rais Magufuli kufuatia mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Kuchunguza Makinikia chini ya Profesa Mruma, iliyoshauri Serikali kujenga mtambo wake wa kuchenjua makinikia ili kuepuka kupoteza kiwango kikubwa cha dhahabu.

IMG_0280.JPG
 
Sisi wengine wenye kalamu ya wino mwekundugu hapa tunatolea wapi mapendekezo yetu
 
mbona hii Wachina wanayo hapahapa Lakezone, Tanzania siielewi kabisa!
 
“Lengo ni kusaidia wachimbaji wadogo na wa kati lakini pia hata kwa kampuni kubwa zitakazohitaji kuchenjuliwa madini ya dhahabu

Nilidhani kutokana na yale yaliyotokea kwenye sakata la makinikia huo mtambo utakuwa suluhisho... kumbe ni hadi hizo kampuni kubwa zitapohitaji?

Hivi kwa akili ya kawaida hizo kampuni kubwa zinaweza kuhitaji huo mtambo wetu?
 
Sio mbaya na sisi kama nchi tukiwa na mtambo wetu Mkuu,kimsingi tumechelewa ila bado haiondoi umuhimu wa huo mtambo kwa Taifa.
Walidai Tanzania hakuna but this chinese wanahizi mashine
 
“Lengo ni kusaidia wachimbaji wadogo na wa kati lakini pia hata kwa kampuni kubwa zitazohitaji kuchenjuliwa madini ya dhahabu

Nilidhani kutokana na yale yaliyotokea kwenye sakata la makinikia huo mtambo utakuwa suluhisho... kumbe ni hadi hizo kampuni kubwa zitapohitaji?

Hivi kwa akili ya kawaida hizo kampuni kubwa zinaweza kuhitaji huo mtambo wetu?
Ni shauri yao, wasipokuja kwenye mtambo huo itakula kwao kwani kwa sasa hatutaruhusu kupeleka makinikia nje ya Nchi. So wao wataamua ama kusuka au kunyoa.
 
Wange yapitisha yale makinikia yetu yalio zuiwa huko ili sisi wakina Tomaso tujue ukweli wa nini na kiasi gani cha dhahabu etc viko kwenye makinikia hayo ujulikane. Ni maprofessa au Acacia walikuwa wanasema ukeli? Professorial rubbish or Acacia thievery!!!!!! Washushe na data za kiuchumi.
 
Walidai Tanzania hakuna but this chinese wanahizi mashine
Wachina wana za kuchenjua dhahabu lakini ni ndogo haziwezi kufanya uchenjuaji wa makinikia. Kumbuka makinikia karibia yote huzalishwa katika Mgodi wa Bulyanhulu
 
View attachment 951163
Mineral concentrates smelting plant.

Mtambo wa Kuchenjua dhahabu uko mbioni kukamilika baada ya kufikia asilimia 95%. Mtambo huo unajengwa katika eneo la Lwamugasa, mkoani Geita.

Waziri wa Madini, Angela Kairuki alisema kuwa, lengo la mtambo huo ni kusaidia wachimbaji wadogo na wa kati lakini pia hata kwa kampuni kubwa zitajazohitaji kuchenjuliwa madini ya dhahabu.

Mtambo huo uliojengwa na Serikali utakuwa chini ya Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) ambao watakuwa wasimamizi wakuu wa mtambo huo.

Hayo ni matokeo ya maagizo ya Rais Magufuli kufuatia mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Kuchunguza Makinikia chini ya Profesa Mruma, iliyoshauri Serikali kujenga mtambo wake wa kuchenjua makinikia ili kuepuka kupoteza kiwango kikubwa cha dhahabu.

View attachment 951068
Hii ndio yaitwa smelter au sio. . . .mi nadhani tusubirie ikamilike then ianze kufanya kazi afu ndio tuanze kujudge kuanzia hapo. Hofu yangu kuu ni sabotage tu kwa lengo la kukwamisha malengo ya huu mtambo/mashine
 
Mwenzenu muse7 alishajenga African gold processing plant!
Entebe hapo

Ova
 
Mtambo wa Kuchenjua dhahabu uko mbioni kukamilika baada ya kufikia asilimia 95%. Mtambo huo unajengwa katika eneo la Lwamugasa, mkoani Geita.

Waziri wa Madini, Angela Kairuki alisema kuwa, lengo la mtambo huo ni kusaidia wachimbaji wadogo na wa kati lakini pia hata kwa kampuni kubwa zitajazohitaji kuchenjuliwa madini ya dhahabu.

Mtambo huo uliojengwa na Serikali utakuwa chini ya Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) ambao watakuwa wasimamizi wakuu wa mtambo huo.

Hayo ni matokeo ya maagizo ya Rais Magufuli kufuatia mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Kuchunguza Makinikia chini ya Profesa Mruma, iliyoshauri Serikali kujenga mtambo wake wa kuchenjua makinikia ili kuepuka kupoteza kiwango kikubwa cha dhahabu.

View attachment 951068
Nyie mnafurahisha sana hebu, tuambie capacity ya huo mtambo, unajengwa na nani? Tends ya kumpata mjenzi ilitangazwa wapi? Bugeti ,yake ilipitishwa na nani??
Hiyo dhahabu mtamuuzia nani?
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom