Pia ilisemekana et unahitaji umeme mwingi ss c jui kama MWT tulizonazo ztatosha.Hivi si ilisemekana kujenga huo mtambo ni gharama mno na inahitaji muda mrefu,inakuwaje huo uwe tayari mapema hivi?
Maswali gani haya ndugu yangu? Nyie ndio wapenzi wenu wanapowapa style mpya mnaanza kuwapiga kwa kudai wamelala nje na kujifunza hizo style, right? Hamna shukrani.Nyie mnafurahisha sana hebu, tuambie capacity ya huo mtambo, unajengwa na nani? Tends ya kumpata mjenzi ilitangazwa wapi? Bugeti ,yake ilipitishwa na nani??
Hiyo dhahabu mtamuuzia nani?
mnataka kuchenjulia makinikia mtachimba kwa machepeo ? wawekezaji wamejiondokea mmeachiwa mchimbe kwa sululu .Hongera watanzani sote tunaoitakia mema nchi yetu.
Sio mbaya na sisi kama nchi tukiwa na mtambo wetu Mkuu,kimsingi tumechelewa ila bado haiondoi umuhimu wa huo mtambo kwa Taifa.
Hivi siku hizi umeamuakuwa raia wa nchi gani?mnataka kuchenjulia makinikia mtachimba kwa machepeo ? wawekezaji wamejiondokea mmeachiwa mchimbe kwa sululu .
Hivi sheria yetu si-imekataza kubeba mchanga na kwenda kuuza nje bila kuchenjuliwa? Ama nilisikia vibaya.Nilidhani kutokana na yale yaliyotokea kwenye sakata la makinikia huo mtambo utakuwa suluhisho... kumbe ni hadi hizo kampuni kubwa zitapohitaji?
Nendeni mkatolee ufipa.Sisi wengine wenye kalamu ya wino mwekundugu hapa tunatolea wapi mapendekezo yetu
Mtambo wa Kuchenjua dhahabu uko mbioni kukamilika baada ya kufikia asilimia 95%. Mtambo huo unajengwa katika eneo la Lwamugasa, mkoani Geita.
Waziri wa Madini, Angela Kairuki alisema kuwa, lengo la mtambo huo ni kusaidia wachimbaji wadogo na wa kati lakini pia hata kwa kampuni kubwa zitajazohitaji kuchenjuliwa madini ya dhahabu.
Mtambo huo uliojengwa na Serikali utakuwa chini ya Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) ambao watakuwa wasimamizi wakuu wa mtambo huo.
Hayo ni matokeo ya maagizo ya Rais Magufuli kufuatia mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Kuchunguza Makinikia chini ya Profesa Mruma, iliyoshauri Serikali kujenga mtambo wake wa kuchenjua makinikia ili kuepuka kupoteza kiwango kikubwa cha dhahabu.
View attachment 951068
Huelewi unachoongea. Kwa sasa hakuna kampuni hata moja inayozalisha makinikia. Inavyoelekea hujui makinikia ni nini.Ni shauri yao, wasipokuja kwenye mtambo huo itakula kwao kwani kwa sasa hatutaruhusu kupeleka makinikia nje ya Nchi. So wao wataamua ama kusuka au kunyoa.
Usiamini maneno ya mleta mada. Mpaka sasa, hatuna mtambo hata mmoja Tanzania wa kuprocess makinikia. Huyu anachoongelea ni mtambo wa kuyeyushia dhahabu (Gold Elution) kutoka kwenye carbon.Wange yapitisha yale makinikia yetu yalio zuiwa huko ili sisi wakina Tomaso tujue ukweli wa nini na kiasi gani cha dhahabu etc viko kwenye makinikia hayo ujulikane. Ni maprofessa au Acacia walikuwa wanasema ukeli? Professorial rubbish or Acacia thievery!!!!!! Washushe na data za kiuchumi.
Tunataka kujua yale matrilioni mlio twambia mtalipwa yameishia wapi?Mtambo wa Kuchenjua dhahabu uko mbioni kukamilika baada ya kufikia asilimia 95%. Mtambo huo unajengwa katika eneo la Lwamugasa, mkoani Geita.
Waziri wa Madini, Angela Kairuki alisema kuwa, lengo la mtambo huo ni kusaidia wachimbaji wadogo na wa kati lakini pia hata kwa kampuni kubwa zitajazohitaji kuchenjuliwa madini ya dhahabu.
Mtambo huo uliojengwa na Serikali utakuwa chini ya Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) ambao watakuwa wasimamizi wakuu wa mtambo huo.
Hayo ni matokeo ya maagizo ya Rais Magufuli kufuatia mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Kuchunguza Makinikia chini ya Profesa Mruma, iliyoshauri Serikali kujenga mtambo wake wa kuchenjua makinikia ili kuepuka kupoteza kiwango kikubwa cha dhahabu.
View attachment 951068
Hongera watanzania sote tunaoitakia mema nchi yetu.
Pole.Punguza usukununu