Mtambo mkubwa duniani wa kusafisha mafuta - Ras Tanura umefungwa, Afrika Mashariki tujiandae kisaikolojia

Mtambo mkubwa duniani wa kusafisha mafuta - Ras Tanura umefungwa, Afrika Mashariki tujiandae kisaikolojia

Fascinating

Member
Joined
May 14, 2025
Posts
93
Reaction score
224
Hali ya upatikanaji wa nishati duniani imekuwa ikitabiliwa kuwa hatarini baada ya kuanza mgogoro wa Iran, lakini hatua iliyochukuliwa leo na Saudi Arabia inaweza kuharakisha zaidi hali haliyo, hii ni kufuatia shambulio la ndege zisizo na rubani (drones) lililosababisha kusimama kwa shughuli katika kitalu cha kusafishia mafuta cha Ras Tanura nchini Saudi Arabia ambao ndio mtambo mkubwa zaidi wa kusafishia mafuta Mashariki ya Kati, kusimama kwa uzalishaji wake kunaondaoa kwenye soko zaidi ya pipa 550,000 za mafuta kwa siku. Kukosekana kwa idadi hii kunaweza kusababisha bei ya mafuta ghafi ya Brent kupanda kwa 10%, hali inayozua hofu ya kupanda kwa gharama za maisha katika sehemu mbali mbali duniani ikiwemo ukanda wa Afrika Mashariki.


rt-clean-fuel-safety-manhours.jpg


Kwa nchi kama Tanzania, Kenya, na Uganda, mtikisiko huu umekuja wakati mbaya. Uchumi wa nchi hizi unategemea kwa kiasi kikubwa mafuta yaliyosafishwa kutoka Ghuba ya Uajemi kwa ajili ya usafiri, viwanda, na sekta ya kilimo.

Mtambo wa Ras Tanura si kiwanda tu; ni mhimili mkuu wa usambazaji wa nishati duniani. Kusimama kwa uzalishaji wake, kukiambatana na hali tete ya usalama katika Mlango wa Bahari wa Hormuz, kumerudisha hali ya wasiwasi kwenye soko la mafuta duniani.

Ingawa kampuni ya Saudi Aramco imetoa hakikisho kuwa akiba ya ndani iko salama, soko la dunia linahofia kuwa akiba hiyo inaweza kuwa ya muda mfupi tu na hali inaweza kuwatete hivi karibuni kama mtamnbo hup utaendela kusitisha uzalishaji. Ikiwa matengenezo yatachukua muda mrefu, dunia itakabiliwa na uhaba mkubwa wa petroli na dizeli, bidhaa ambazo mahitaji yake ni zaidi ya asilimia 30 nishati yote ya matumizi ya kilasiku kufikia 2024.

Afrika Mashariki inaweza kuwa hatarini zaidi kutokana na kuu sababu tatu:
Gharama ya Bidhaa Tayari (Landed Cost)

Tofauti na mataifa makubwa yanayosafisha mafuta yao yenyewe, nchi za Afrika Mashariki huagiza mafuta ambayo tayari yameshasafishwa (petroli, dizeli, na mafuta ya ndege). Mtambo kama wa Ras Tanura unaposimama, bei ya mafuta haya yaliyosafishwa hupanda kwa kasi kubwa zaidi kuliko hata bei ya mafuta ghafi.

Shinikizo la Bei nchini Kenya
Nchini Kenya, Mamlaka ya EPRA inatarajiwa kutangaza bei mpya za mafuta ifikapo Machi 14. Baada ya unafuu kidogo uliopatikana mwezi Februari, kupanda huku kwa bei duniani ni wazi kutafuta faida hizo. Wachambuzi wanatabiri kuwa bila ruzuku ya serikali, mzigo huu wa bei utahamishiwa moja kwa moja kwa mlaji (mwananchi).

Gharama za Usafirishaji na Bima
Kwa bandari za Dar es Salaam na Mombasa, changamoto si bei ya mafuta pekee, bali ni gharama ya kuyafikisha bandarini. Hali ya kivita katika Ghuba ya Uhajemi inasababisha bima za meli kupanda (war risk surcharges). Gharama hizi za ziada mwisho wa siku huishia kuongeza bei ya lita moja ya mafuta kwenye kituo cha mafuta mtaani kwako.

Kwa mwananchi wa kawaida wa Dar es Salaam au Nairobi, kufungwa kwa mtambo wa Ras Tanura si habari tu ya kimataifa bali ni tishio la moja kwa moja kwa gharama zake za maisha. Kihistoria, kupanda kwa bei ya mafuta husababisha:
  • Kupanda kwa Nauli: Ongezeko la gharama za daladala, matatu na mabasi.
  • Mfumuko wa Bei ya Chakula: Gharama za kusafirisha mazao kutoka mashambani kwenda mijini huongezeka.
  • Kuteteleka kwa shaghuri za Viwanda: Gharama za uendeshaji hupanda kwa viwanda vinavyotegemea majenereta ya dizeli.
Wakati wahandisi wa Saudia wakikagua uharibifu leo, watunga sera wa Afrika Mashariki watakuwa wakifuatilia kwa karibu, wakijiandaa kwa mtikisiko wa kiuchumi ambao unaweza kudumu kwa miezi kadhaa.

Reuters
 
Na hii serikali ina vichwa panzi...
Hakuna viongozi wanaoweza kuwaza nje ya box ili kukabiliana na hii changamoto..
Samuya utasikia 'sio sisi tu hali hii inatukuta, hata mataifa mengine' , imeisha hio.
 
02 March 2026

Gordon Chang: Kwa Nini Barabara Zote Huelekea Uchina

View: https://m.youtube.com/watch?v=e-3cRrquknc
China imekuwa mhanga mkuu, washikaji zake Nicolas Maduro wa Venezuela na Ali Khamenei wote walikuwa chanzo kikuu cha mafuta kwa China na sasa vyanzo hivyo vimekata, hii ina maana gani kwa uchumi wa China

Viongozi kadhaa wa Iran, akiwemo Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Khamenei, wameuawa katika mashambulizi ya pamoja ya Marekani na Israeli dhidi ya Iran.

Katika kipindi hiki, nimekaa tena na mchambuzi mzoefu wa China Gordon Chang, mwandishi wa "Plan Red," ili kuelewa jinsi hii inavyobadilisha matukio ya Venezuela na Iran athari zake kwa mazingira ya kijiografia ya kimataifa—hasa kwa Beijing.

Ikijumuisha uvamizi wa Venezuela uliomkamata kiongozi wa serikali Nicolás Maduro, hii ni mara ya pili Rais Donald Trump anaonekana kumzuia mshirika muhimu wa Beijing
 
Back
Top Bottom